Nini chanzo Biashara ya mabasi kufeli?

Nini chanzo Biashara ya mabasi kufeli?

nzalendo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
12,683
Reaction score
14,066
Miaka yote nimejikita katika malori..lakini kwa sasa napata upepo ndoto na maono juu ya biashara ya mabasi....lakini si mabasi ya kifahari....hapana ....la hasha.....ni mabasi kwa ajili ya huduma kwa raia....hasa kwenye njia mbazo ni za vumbi ndani ndani nje ya miji..... kwa daladala pamoja na masafa ya kati.....
Mbali na imani za shirki nini hasa kinapelekea biashara kufeli???
 
sio mzoefu sana ila kwa maoni yangu, biashara imebana kipato, matumizi ni mengi na nauli imewekewa kikomo. Pia, kuna wamiliki ambao wana njaa kiasi kwamba ndo biashara yao ya kula kila siku. Labda pia wanapandisha gharama zao za maisha hivyo gari likija kuhitaji service kubwa, anakuwa hela imembana. Ila ni biashara nzuri ukiwa na usimamizi mzuri na nidhamu ya fedha.
 
shukran sana
 
Biashara ya mabasi ni biashara ya msimu. Kipindi cha sikukuu, wiki end ndefu, msimu wa wanafunzi kutoka na kwenda shule ndio inakuwa nzuri. kwa hiyo matajiri wajanja hutumia fursa hizi.

Kitu kingine ni huduma nzuri na wafanyakazi wanaozingatia customer care. Lakini pia ni ku keep standard ya huduma. Na kuhakikisha muda wote mabasi yapo katika kiwango na good service. basi likiharibika njiani mara moja kuna uwezekano wa kupoteza abiria kadhaa.

Wafanyakazi kwa asilimia kubwa sio waaminifu, wanaibasana na kiasi fulani inategemea na job security yaani hawana uhakika wa kundelea na ajira kwa muda mrefu ujao.

Pia uzoefu wa biashara ya mabasi, kuna watu wanaingia kichwa kichwa baada ya muda wanapotea.
Baadhi ya matajiri kuingia kwenye biashara nyingine baada ya kupata faida kutokana na biashara ya mabasi na kuacha biashara ijiendee.

Succession, tajiri akifa na kampuni inakufa kwa sababu warithi hawana uzoefu na hawakuandaliwa mpaka kufikia hatua yakugawana mabasi, mwishowe.....

Mambo ni mengi......
 
Back
Top Bottom