Nini cha kufanya ukipata maambukizi ya covid 19

Inamaana tuachane na maombi tuanze na mizizi?
Yamefanyika maombi hadi ya kuomba mizimu ila wapi!
dw_kiswahili_B_PKmx5Jpd4.jpg
 
Asante sana mkuu.
Siku hizi nimejipa ratiba ya kunywa tangawizi iliyochanganywa na pili pili manga kila ifikapo jioni, najifukiza mwarobaini mara 2 kwa wiki, nakunywa maji mengi zaidi ya nilivyokuwa nakunywa mwanzo, Pia juice ya limao nachanganya na asali.
Kujihami tu.

Andaetini

Afya nzuri

Mazoezi /

Conclusion: Unahangaika bure tu. Korona kwako ni sawa na mafua hafifu na unaweza ukaipata usionyeshe hata dalili (asymptomatic).

Ila yote unayofanya ni mazuri kwa afya kwa ujumla. Jambo la muhimu zaidi kuliko yote hayo, na ambalo nadhani halitiliwi mkazo zaidi katika mapambano haya, ni uimarishaji wa immune system.

- Hakikisha unapata usingizi wa kutosha kila siku (masaa 7-8). Hii ni muhimu sana. Kulala chini ya masaa matano hata kama ni kwa siku moja tu kunadhoofisha immune system sana. Tafiti nyingi sasa zinaonyesha kwamba kutopata usingizi wa kutosha pengine ndiyo chanzo kikuu cha saratani nyingi na magonjwa mengine mengi. Lala !!!

- Kula vyakula vyenye wingi wa Vitamin C na Zinc

- Fanya mazoezi (mepesi) mf. Kutembea/kukimbia. Hakikisha mapigo ya moyo wako yanaongezeka na unapumua kwa kasi. Mbali na faida zinginezo, lengo hapa ni kuimarisha moyo pamoja na mapafu. Kuwa na kifua

- Tumia supplements zenye Vitamin C na Zinc. 1500 mg+. Zimethibitishwa kisayansi kuwa zinaimarisha sana immune system.

- Epuka msongo wa mawazo. Sala na meditation vyafaa hapa. Samehe waliokukosea. Fanya vitu vikupavyo furaha na amani ya moyo na fikra.

- Tenga angalau siku moja kwa wiki ufunge. Usile cho chote isipokuwa maji kwa wingi. Hii inachaji immune system yako upya.

...and stay blessed
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom