Nini cha kufanya, nimeibiwa simu Samsung S6

Risk vs Return

Senior Member
Apr 23, 2012
106
71
Wakuu salama,

Naomba msaada wenu wa haraka kuweza kupata hiyo simu yangu nimeibiwa muda mfupi tu

Polisi nimeshatoa taarifa, kwa sasa ukiipiga haiiti tena kama imezimwa, naomba taratibu za kufanya tafadhali.
 
Duh pole kaka mamana hapo ni sawa na umeibiwa kiwanja mlandizi ambacho baada ya miaka 5 ungekiuza m10.
 
Omba mungu utapata nyingine. Huna cha kufanya hapo.

Duc in Altum
 
Angalia kwanza sehemu hizi

1))unatoaga sadaka kamili sioo legelege

2))unatoaga Zaka kamilii ni muhimu tukatafuta SRC yatatizo

3))unahudumia wazazi wako

Kati yahapo ukiibaa hata mojaa namaanisha usipofanya huwa madumadu wanakwapua via malizako ili uwakumbuke

Angaliawapi ymekosea uweke sawa ili hats ukipata nyingine isiibiwe tenaa
 
Jitahidi ukipata nyingine weka anti thief ili ikusaidie kupatana sim mara inapopotea au kuibiwa. Pole sana.
 
chukua Maristi yako cheki International Mobile Equipment Identity(IMEI No.), halafu check na TCRA wanaiblock forever haitatumika tena. But pia mtandao kama Voda na Tigo pia wanaweza kukuambia iko wapi kama una hiyp IMEI na ukaenda kumkamata huyo mtu kwani si tayari una Criminal Report Book(RB)
 
Pole sana,wapigie kwanza makampuni ya simu wafunge akaunti mfano tigo pesa.Nenda na IMEI wataifunga simu.Yamenikuta juzi tu...inauma sana.
 
Pole sana mkuu, jitahidi tu sasa ununue galaxy s7 maana hamna namna nyingine
 
Ndio shida ya android phones, invalidate iPhone angeenda uza spare parts. Ila Imei Kama unayo Nenda kampuni yako wakupe msaada wa kutrack namba inayotumika kwa Sasa.
 
Kweli wewe ni risk vs return.
Yani s6 umeinunua na ina high risk ya kuibiwa na hajaleta return yoyote.
Chakufanya.
Chukua risiti yako,RB na lost repot na imei Namba yako. Nenda kwenye mtandao wako wa simu waifunge (blacklisted) haitaweza kutumika tena.na akienda kwenye network yoyote kucomplain watamdaka.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom