Nini cha kufanya endapo utakuta dhahabu kwenye shamba au kiwanja chako?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,695
6,398
Kwa Sheria za Tanzania, unaweza kumiliki ardhi lakini sio kilichopo chini ya ardhi kama madini. Ndivyo nijuavyo, labda kama utaratibu umeshabadilika. Inamaanisha kuwa hata ukigundua dhahabu kwenye shamba lako au kiwanja chako, hutaruhusiwa kuchimba mpaka uwe na leseni.

Sasa chukulia ulikuwa unachimba shimo la choo, na ghafla ukakutana na bonge la dhahabu (nugget) kubwa kama kichwa cha ng'ombe, nini utakachopaswa kufanya Kisheria?

1. Kwenda kuripoti Polisi?

2. Kwenda kutoa taarifa wizarani?

3. Kuujulisha uongozi wa Serikali ya Mtaa?

4. Kwenda kuiuza na kisha kuwasilisha TRA stahiki za Serikali?

Ni hatua gani sahihi utakayopsawa kuchukua?

Nani atakuwa mmiliki halali wa hiyo dhahabu?

Ukijimilikisha bila kutoa taarifa Serikalini utakuwa umetenda kosa, hasa ikizingatiwa kuwa umeichimbua bila kutarajia?
 
Attachments

  • MGODI_WA_DHAHABU_WAIBUKA_KATIKATI_YA_MAKAZI_YA_WATU_NI_BAADA_YA_MWANA_KIJIJI_KUCHIMBA_CHOO(360p).mp4
    12.1 MB
  • Ghana_Teens_Find_Enormous_Gold_Nugget_Possibly_Biggest_in_Countries_History(360p).mp4
    7.8 MB
  • Nearly!_70_Kilograms_of_Gold_Nugget;_Huge_Actually(360p).mp4
    79.2 MB
Yote yanaweza yakawa majibu sahihi. Bahati humwendea aliyejiandaa. Nimeshajiandaa kwa hilo tokea "Jana".
Ukiipeleka kwa Serekali sio ya kwako tena hio na hupati hata Mia mbovu na mbaya zaidi unaweza ukashtakiwa na ukafungwa juu au ukalipishwa faini na fidia juu, nisiseme mengi labda wakukute na bangi ndio watakwambia hii bangi ni yako unalima bangi
 
Kwa hiyo kumbe ni bora ujinyamazie zako na kuiuza kimya kimya.

Lakini Serikali imetoa wapi huo utaratibu? Mbona inawashawishi raia kusema uongo?
 
Uliza ilichomkuta yule Jamaa wa Shinyanga.
Muhimu ni kutuliza munkari.
Chukua sehemu kauze kaboreshe mahali pako kwa kuweka hata kiwanda cha unga wa sembe then usiku unangurumisha machine watu wanajua unaasaga sembe kumbe unaasaga mawe.
Ukijiroga tu utauwawa . Usicheze na pesa
1699026277730.jpg
 
Ushauri wangu kama ni eneo ambalo halina history ya dhahabu (probability ya uwepo wa leseni ni mdogo) nenda tume ya madini usiseme umeiona au kugundua dhahabu we kata kipande kikubwa Hadi kwa watu ambao bado hawajastuka lipia leseni (watakupa utaratibu) baada ya hapo we tangaza Kuna mzigo. Wadau watakuja ruhusu wachimbe we kula asilimia tu......
 
Aisee!

Watu wengine mmekaa ki - CIA!

Hizo mbinu siyo za layman😃
 
Uliza ilichomkuta yule Jamaa wa Shinyanga.
Muhimu ni kutuliza munkari.
Chukua sehemu kauze kaboreshe mahali pako kwa kuweka hata kiwanda cha unga wa sembe then usiku unangurumisha machine watu wanajua unaasaga sembe kumbe unaasaga mawe.
Ukijiroga tu utauwawa . Usicheze na pesa
View attachment 2823887
Jamaa yupi huyo? Yule aliyepata almasi ya bilioni tatu?
 
Ushauri wangu kama ni eneo ambalo halina history ya dhahabu (probability ya uwepo wa leseni ni mdogo) nenda tume ya madini usiseme umeiona au kugundua dhahabu we kata kipande kikubwa Hadi kwa watu ambao bado hawajastuka lipia leseni (watakupa utaratibu) baada ya hapo we tangaza Kuna mzigo. Wadau watakuja ruhusu wachimbe we kula asilimia tu......
✅🙏
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom