Nini Asili ya neno SOLEMBA ?

PascalFlx

Member
Feb 11, 2009
68
5
Weekend hii nilikuwa nimepumzika nyumbani na nikatembelewa na rafiki yangu mmoja toka Uganda. Huku tukiwa tunapiga porojo za hapa na pale tukiwa tunasikiliza bongo radio mara wakapiga nyimbo ya Bushoke na Yule dada wa kiganda nadhani unaitwa usinde mbalai nami (kama nimekosea mtanirekenisha).
Mara yule dada akaniuliza hivi hili neno SOLEMBA maana yake halisi ni nini na linatokea wapi?.
Nikaanza kucheka kwanza kwani hili swali ukiwauliza vijana wengi waliozaliwa miaka ya 90 watakosa jibu la kukupatia.
Lugha ya kiswahili kama Lugha nyingine zinakuwa (zinaongezeka) kutokana na wakati, kuna lugha ya mitaani, maneno ya muda na maneno mengine hujitokeza na kukaa sana hadi kuingizwa katika kamusi na kupitishwa kama neno halisi na linaweza kutumika katika nyanja zote,. hivi ndio jinsi lugha invyokuwa sasa sielewi kama solemba lilishapitishwa au la.
Kwanza kabisa kabla hatujaenda mbali .. Solemba analopewa mtoto wa kike kama majina mengine Salama, Upendo, Bahati n.k.
Katika miaka ya 80 mwishoni au 90 mwanzoni bendi ya muziki wa dansi Juwata Jazz Band kupitia kwa mwanamuziki wake Nico Zenge Kalla (Mungu amuweke mali pema peponi) alitunga wimbo ulioitwa kwa jina la Solemba, akimlalamikia jinsi alivyovunja miadi yao. (nilijaribu kuutafuta niuweke hapa ila sijaupata) ila ndani ya huo winbo kuna sehemu Nicco analalamika kuwa alipigwa na jua toka Asubuhi hadi saa nane akimngojea Solemba.., na Solemba alikuwa ndani anamchungulia Dirishani. Nicco anendelea kumwambia Solemba katika huo wimbo kuwa Alimpenda kimapenzi ila Dharau Solemba aliweka mbele. Wimbo ulikuwa mzuri na ulivuma sana hivyo tangia hapo ndipo watu walipoanza kulitumia hilo neno wasiachwe Solemba wakimaanisha kuwa wasitendewe kama alivyofanyiwa Nicco, wimbo umekwisha ila Solemba amebakia katika matumizi yake na baada ya neno hilo kuwa maarufu na kuanza kutumika katika Lugha watu wameacha kuwaita watoto wao Solemba, na ndio maana kwa sasa ni vigumu kwa watu hasa Vijana kujua nini Asili ya neno hili.
Kwa leo sina la zaidi nimejitadi kuandika bila kuchanganya Lugha ya kiingereza ili kutia msisitizo wa Lugha yetu.
 
Solemba kama unavyosema unatokana na Juwata Jazz enzi ya marehemu Nico zenge kalla. Yeye alikaa akimsubiri Solemba (MPENZI WAKE) lakini Solemba hakutokea. Sasa sisi waswahili tumechukua jina hilo na kuita kitendo cha kuwekwa kumsubiri mtu kuwa ni "SOLEMBA". hivyo SOLEMBA ni kuachwa kumsubiri mtu ambaye hatokei.
 
..... hivyo "SOLEMBA" ni kuachwa kumsubiri mtu ambaye hatokei.
..................Nice!!!

Kwa maneno mengne ni kama vile kuanikwa au kugandishwa!-Hususan pale unaposubiri mtu ambae una miadi naye halafu asitokee kabisa.
 
Asante, Solemba ni kazi ya Nico Zengekala(RIP) kwenye huo wimbo sasa hili jina limegeuka neno kwa kutoholewa kama jina la Kihiyo linavyomanisha kutosoma na kufoji kufuatia ushindi wa Juma Radhani Kihiyo kwenye ubunge wa Temeke na kutenguliwa na mahakama baada ya kuthibitisha jamaa darasa la saba, kafoji cheti cha form four.
Nimefurahi umemkumbuka Niko, pia kuna wimbo wake wa wa 'Kifuko cha Zambarau'
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom