Nini asili ya neno machinga?

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,134
4,293
MACHINGA ni msemo wa kiswahili unaowakilisha wafanya biashara wadogo wadogo ambao hufanya biashara kwa kuweka bidhaa zao kandokando ya barabara au hata sokoni.
neno MACHINGA limechukuliwa kutoka katika kabila la wamachinga ambao asili yao ni Mtwara katika wilaya ya Kilwa na Lindi.
wamachinga wao ndo watu wa mwanzo kuanza kupanga bidhaa zao barabarani na kutokana na jina la kabila lao,taratibu wafanya biashara hao waliitwa jina la WAMACHINGA.
 
Asili ya neno machinga ni "marching guy" likiwa na maana kijana anaetembea liliwalenga wale wafanyabiashara kutoka mtwara ambao wanafanya biashara kwa kutembea na vitu vyao wakiwa wamevibeba.
Maeneo ya zenji walikuwa wakiitwa mwilini shop
 
Asili ya neno machinga ni "marching guy" likiwa na maana kijana anaetembea liliwalenga wale wafanyabiashara kutoka mtwara ambao wanafanya biashara kwa kutembea na vitu vyao wakiwa wamevibeba.
Maeneo ya zenji walikuwa wakiitwa mwilini shop
Hiyo ya marching guy si kweli. Hii ya marching guy ilizushwa na vijana wa mjini kutokana na wimbo wa Ace of Base All that she wants ambako vijana wa mjini waliianza kuimba oooh matching guy badala ya all that she wants. Hivyo maana sahihi ni kabila la wamachinga ndo walianza biashara ya kutembeza bidhaa mbali mbali wakati wa mzee Ruksa wakitumiwa na Wahindi. Wamachinga wote walikuwa wanaishi mbagala wale waliokuwa wanaaminiwa wanaenda kwa wahindi wanapewa bidhaa kwenda kutembeza mitaani na kurudisha mahesabu jioni
 
Merchant ni kiingereza kikimaanisha mtu ananunua bidhaa na kuuza.
Siku zote najua imetokea hapo
 
Enzi za waarabu walikua wakitembea na bidhaa zao(arab merchants) wanabadilishana na babu zetu.
 
Back
Top Bottom