Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Watanzania mara nyingi tunakuwa wepesi sana wa kusahau. Raisi Kikwete akijua huu udhaifu wetu, pale ambapo alipata changamoto kutoka kwa wananchi aliwashauri wateule wake kutojishighulisha na mihemuko ya wananchi, akidai ni mambo ambayo yangepita tu kama upepo.
Kwa mfano, juzijuzi hapa mitandao ya jamii ilikuja juu sana kuhusu tukio la Mkurugenzi wa Halmashauri kutuhumiwa kumpiga kijana risasi ndani ya kanisa. Tukio hili lilikuwa na mhemuko mkubwa iliposemekana Mkurugenzi huyo alikuwa ni mtoto wa dada yake Raisi Magufuli. ILisemekana alikamatwa na kuwekwa ndani. Sasa kama bado yuko ndani sijui na ningependa kujua, ukizingatia kwamba hapa Tanzania kesi za mauaji hazina dhamana.
Pili ni yule askari wa FFU alipowekwa ndani kwa kosa la kumuua mwandishi wa habari, Mwangosi. Je nini ilikuwa hatima ya lile suala? Je askari alikukumiwa?
Nadhani kuna matokeo mengi makubwa ambayo wan JF mnayajua, na ni wengi wangependa kujua yalikuja kuishaje. Kuna kesi nyingi sana za Polisi kuua raia katika vituo vya polisi ambazo tumesikia, lakini hata siku moja hatujasikia mwisho wake, au wauaji kuwajibishwa. Juzi hapa IGP alisema anawajua watekaji wa MO na atawatia ndani baada ya siku tatu. Kimya, na hakuna anaejali. Kuna suala la FFU kupiga watu Ukonga, na hata askari na gari zilizotumika zilijulikana na serikali kuahidi kuchukua hatua kali. Kimya.
Je, serikali imegundua kuwa Watanzania ni wepesi kusahau hivyo hata wauaji huachiwa kwa kuwa hakuna tena anaekumbuka mambo maovu waliyofanya? Watanzania tumekuwa ndondocha kiasi hiki?
Wale ambao ndugu au rafiki zenu walikutwa na masahibu kama hayo na habari ikavuja, tuambieni kama waliohusika walichukuliwa hatua. Wengine tunaambiwa mnalipwa ili yaishe kimya.