Ningekuwa Rais Samia Suluhu Hassan

Astrum27

Senior Member
Nov 28, 2016
143
215
Asubuhi nyingine tena hii. Niwasalimu kwa la Jamhuri ya Muungano..Tuseme kwa pamoja kazi iendelee (Sidhani kama kuna kazi inaendelea)

Tumshukuru Mungu kwa Siku nyingine Tena, najua dhahiri katupa nafasi nyingine ya kufanya kilichotuleta hapa duniani. Ukiona hujui kilichokuleta wewe acha mbegu ufe 😂😂. Huenda mbegu ikachipua mtu mwingine bora zaidi.

Nilishtushwa kidogo na kauli ya Raisi kuwa anafuatilia mijadala mingi ya wananchi, na ni ukweli ukiwa magogoni huwezi jua kama Tanzania ni masikini mpaka upitie baadhi za kurasa za mitandao ya kijamii. Hapo awali sikuwa na shaka kuwa mhedhimiwa kasign up Twitter kwa ajili ya pole, hongera na kongole abcd... nimesikitishwa. Niwapongeze.

Ila nimegindua kwa kuwa na cheo cha uongozi mkuu nchini, inashindikana kucomment post ya Zitto Kabwe.

Niende moja kwa moja kwenye mada.

Mosi, ningekuwa rais wa jamhuri Dkt. Samia Suluhu Hassan, kitu cha kwanza nitakacho fanya ni kuwa huru.. uhuru ninayozungumzia hapa ni uhuru haswa (yaani ningekuwa mimi). Kuna muda unakuwa mfungwa huru, kuna vitu vya kuvisemea ila unakuwa kimya. Ningetumia kurasa zangu official kuonesha niko na wapigakura. Ningekuwa naruhusu comments kwa page yangu. Kila nikipata nafasi, basi najibu... niwasikilize wanatatizo gani, niwatoe hofu kuhusiana na usalama kuwa upo kwa ajili yao na si kwa ajili ya Serikali.

Ningekuwa Rais, ningekuwa mama ningekuwa na huruma na watoto wa masikini wanaosoma kwa ela ya vikoba, madeni, baba kakimbia, mtoto kakosa mkopo chuo kikuu, aliyemsaidia (mama) nyumbani nguvu zishaisha, hivyo nimpe ajira kijana yule akomboe jamii yake ya kimaskini. Badala yake tunawapa watoto wa familia tajiri, familia ya viongozi (royal families), walio connected nao wanapewa nafasi wakati kina Kinje wa mbeya asiejuana na mtu hata mmoja anakuwa deni kwa wazazi.

Ningekuwa nafanya tathmini bila kushirikisha wizara kwanini biashara zifungwe Tanzania, zifunguliwe Kenya... Ningefanya Tathmini kwanini gesi yetu mtungi tuuziwe 50,000/-, wenzetu wanunue kwa <7,000/-

Mwisho nimalizie, ningekuwa Rais ningekuwa mzalendo. Ningemtazama mtanzania kama mtoto wa tumbo moja. Ningekunywa maji ya bendera. Ningeacha Siasa za uwongo, ningeachana na porojo za kina Lema. Nisingekubali watu kujiita kwa jina la chawa wangu. Ningekubali kosolewa, ningejiweka nyuma la kundi ninaloongoza. Ningeonesha watu milioni 60 kwamba tuna maliasili kwa ajili yao. Ningekuwa mstari wa mbele kufa kwa ajili ya Taifa.

Natumai kama utapitia uzi huu ningekuomba utoe barakoa puani ili usikie harufu ya umaskini ya kundi unalololiongoza, vua miwani uone, nguo ya kondoo hawa ni mpya, wanaonekana nadhifu lakini wana wiki sasa bila ya kuona chakula kimpasacho mwanadamu.

Nimalize kwa kusema, Mungu ibariki Tanzania, Mungu bariki viongozi wanaotuongoza.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom