Chukwu emeka
JF-Expert Member
- Jan 12, 2018
- 23,410
- 36,560
Habari WanaJF,
Niende moja kwa moja kwenye mada,Jiji la Dar es salaam kwa Tanzania ndiyo limeathirika zaidi na ugonjwa wa Corona na kwa mujibu wa waziri wa afya Ummy Mwalimu ugonjwa tayari upo mtaani,inamaana upo Ubungo,Kinondoni,Mwenge,Tegeta Kariakoo,Posta,Temeke,Mbezi,Mbagala,Gongo la mboto nk.
Sasa kuendelea kuruhusu mabasi ya mikoani kuingia na kutoka jiji la Dar es salaam ni hatari ambayo kama taifa hatutaweza kumudu kudhibiti huu ugonjwa maana mabasi karibia yanafika mikoa yote Tanzania,mabasi yanaweza kuwa chanzo cha kuusambaza huu ugonjwa,pamoja na mabasi pia Treni ya Tazara na ya kwenda Kigoma ilitakiwa zisitishwe ili kutousambaza huu ugonjwa.
Pamoja na hayo pia wasafiri wa magari binafsi na malori ilitakiwa kuwe angalau na checkpoint ya kuwapima au kutoruhusiwa pia kutoka DSM ili kuudhibiti huu ugonjwa,lasivyo tunatega bomu ambalo likilipuka hatutakuwa salama.
Kwashughuli nyingine kama masoko,Ibada lazima kuangalia namna ya kuweka vizuri mazingira ya kutokuwa chanzo cha kusambaza huu ugonjwa,nilipita week iliyopita mtaa wa Congo pale Kkoo,bado hatujawa serious sana,japo kuna mwamko wa kunawa mikono na maeneo mengi kuna ndoo za maji kwaajili ya kunawia mikono ila bado msongamano ni mkubwa sana.
Ushauri wangu tusitishe safari za kwenda nje ya DSM ili kutousambaza huu ugonjwa,lasivyo hatutaweza kuuzuia na tutakufa kama kuku wa kideri.
Tuendele kumuomba MUNGU,wakati huohuo tukichukua hatua na kufuata ushauri tunaopewa na wataalamu wetu.
Chikwuemeka
Nyamongo,Tarime