Je, kwa Kauli hii ya Mkaguzi wa Trafiki bado tu hajatuambia sababu Kuu ya Ajali za Mabasi ya Mikoani na msababishi Mkuu ni nani?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,524
108,805
"Huwa tunafanya Ukaguzi japo siyo mkubwa sana wa haya Mabasi ya Mikoani ila kwa Mwezi huu na Kuelekea hizi Sikukuu za mwisho wa mwaka tumeamua Kuongeza umakini zaidi ili Kupunguza ama Kuzuia kabisa Ajali" alisema Mrakibu wa Ukaguzi wa Mabasi ya Mikoani Trafiki Makao Makuu Dar es Salaam alipokuwa Magufuli Bus Terminal leo Asubuhi na Kuzungumza moja kwa moja na Magic FM katika Kipindi chao cha Morning Magic.

Watanzania tulikuwa tunatafuta mno Chanzo cha Ajali za barabarani mpaka kufikia hatua ya Kumsingizia na Kumbebesha Mzigo usio wake Shetani kuwa Yeye ndiyo sababu na huenda huwa anatushangaa sana tu.
 
Ndugu nakwambia Ajali za Tanzania karibu zote ni uzembe tu.. Angalia jinsi leseni vinavyotolewa kwa rushwa na kuzalisha madereva "Makanjanja 'siku moja niliwai shuhudia Dada mmoja Mlemavu kwa maana ana miguu ya bandia lakini kamuomba Dereva wake kuendesha gari matokeo yake kapata ajali na kufa ha hapo..

Magari mabovu na madereva wengi hawajui sheria za usalama barabarani.

Rushwa imetapakaa kila sehemu kiasi kwamba kila mtu na aneendesha vile anajua yeye
 
Back
Top Bottom