Ninatabiri EAC kuvunjika soon!!!

Ninatabiri EAC kuvunjika soon!!!

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2007
Posts
4,189
Reaction score
3,548
Kama ilivyokuwa mwaka 1977 ambapo wajuaji walikuja na majigambo yao na kuubeza umoja wa Afrika Mashariki leo hii nauona huu wa sasa siyo ushirikiano wa Afrika Mashariki bali ndani yake viongozi hawa wamejaa mate ya hasira kwa Tanzania. Ushauri wa Kikwete kwa Kagame ilikuwa sababu tu lakini fukuto lilishakuwepo pale Tanzania ilipokataa ardhi isiwepo kama kitu halali kwa wanajumuuiya kurithi.

Naunga mkono sana ardhi yetu isiwe shamba la bibi kila mwana Afrika Mashariki akarithi nasema heko Jakaya Kikwete kwa kupinga hilo na hilo ndilo linalowauma sana. Sasa hivi wameanza kubuni mbinu za kupanga uzazi ili kuwe na limit za kuzaa kisa ni uhaba wa ardhi. Niafadhali Tanzania ijitoe katika muungano huu wa mashaka. Wakati Rwanda ikiomba kujiunga Jumuiya ya Afrika Mashariki wengi walitabiri kuwa huu utakuwa ni mwisho wa uwepo wa Jumuiya Halisi ya Afrika Mashariki, sasa nakubali.

Jana katika majarida inasemekana Kikwete alialikwa kuhudhuria mkutano wa wakuu kule Rwanda, hakika Mh. Kikwete alifanya jema kukataa kwenda. Mh. Rais bado tunakupenda sana. Jumuiya hii ya Afrika Mashariki iko ICU hatuna haja nayo, turudi zetu SADC. Yule kiongozi wa waasi M23 amerudi kwao Uganda kujipanga upya nasema karudi kwao kwasababu Uganda na Rwanda wanakifadhili kikundi hiki kuivuruga DRC ya Kabila.

Kama Museveni aliishi hapa Tanzania kule Bukoba na kupatia urais wake kwa msaada wa Tanzania laana itamkuta tu. Kama Kagame aliishi hapa Mtoni Kwa Aziz Ally na kutulia akupanga namna atakavyoitawala Rwanda hapo baadaye basi naye huyu hii laana ya kujitenga haitamuepuka.

Sisi Watanzania hatushangai kamwe kuona tabia hii ya ubaguzi inavyoshamiri kwani HAO WAMEZOEA KUBAGUANA. Hadi sasa wanajaribu kuwa wamoja lakini muziki huu hawatauweza roho zao zimeumbwa zikiwa na vyumba vya uhasama. Tanzania ni nchi ya mfano kwa umoja wake. We are BIG NATION MEEEEEN!!!

Kiburi cha Kagame + Usugu wa Museveni X Uwepo wa Uhuru = Hila, Hasira, Kutiliana Shaka, Viburi na Mwisho wake KUSAMBARATIKA. Muda si mrefu Uhuru Kenyatta ataota kiburi cha kujifanya ndiye mwezeshaji wa utengemao wa Jumuiya yao mpya. Baba yake Mzee Jomo Kenyatta aliiheshimu sana Tanzania.

Mh. Samwel Sitta ametoa tamko zuri sana kwamaba sisi siyo wakupewa talaka bali ni wa kutoa talaka kwa hao wanawali, Tanzania ilikuwa na wazo la kuunda umoja huu Kenyatta akalikubali akafuatia Milton Obote. Hivyo ni sisi tunatakiwa tutoe talaka kwamba hatuwataki.

TANZANIA IS A GREAT NATION FOREVER.
 
Dua la kuku halimpati mwewe kamwe!Au vijana wa siku hizi hamfundishwi methali mashuleni?kama wewe ni Mulugo graduate nakupa pole sana!!!
 
EAC haita vunjika mimi ni nacho ona ni TANZANIA kuondolewa au kujiondoa katika community sio kuvunjika,tatizo watanzania wengi wanafikiri TANZANIA ndio EAC,sio hivyo,naimani kwamba kutoka kwa tanzania itarahisisha mipango ya EAC kwenda kasi kwani mambo ya kusubiri wanao suasua kwa kigezo cha kua na hofu ya washirika wenzake eti wanataka udongo wa tanzania haiwezi jenga EAC,nafikiri hawa viongozi wamaliona hilo,EAC haita vunjika instead sasa ndio inaenda kuonekana kwa vitendo.
 
charity begin at home! nakuunga mkono for sure acha tukae na ujinga wetu! we are proud of who we are!
hata mjinga siku moja huongea point!

Mweshimiwa Rais Hatuko tayari kuburuzwa nao. Watu wenyewe kila siku wana migogoro na mpaka leo hawajaweza kusolve. wasolve kwanza hilo ndipo tuwafikirie. Embu check wanavyowatesa wananchi wa Congo miaka yote hiyo wangapi wamepoteza maisha kwa tamaa wa watu hawa?
 
Tanzania ndiyo EAC Rwanda ni ndogo kama mkoa wa Kilimanjaro tu.

EAC haita vunjika mimi ni nacho ona ni TANZANIA kuondolewa au kujiondoa katika community sio kuvunjika,tatizo watanzania wengi wanafikiri TANZANIA ndio EAC,sio hivyo,naimani kwamba kutoka kwa tanzania itarahisisha mipango ya EAC kwenda kasi kwani mambo ya kusubiri wanao suasua kwa kigezo cha kua na hofu ya washirika wenzake eti wanataka udongo wa tanzania haiwezi jenga EAC,nafikiri hawa viongozi wamaliona hilo,EAC haita vunjika instead sasa ndio inaenda kuonekana kwa vitendo.
 
kutoshikishwa kwa dola kuu kiuchumi, kisiasa, kijeshi na kijamii la TANZANIA katika maamuzi ya msingi ya EAC ni wazi imeshasambaratika! NO EAC WITHOUT TANZANIA
 
EAC haita vunjika mimi ni nacho ona ni TANZANIA kuondolewa au kujiondoa katika community sio kuvunjika,tatizo watanzania wengi wanafikiri TANZANIA ndio EAC,sio hivyo,naimani kwamba kutoka kwa tanzania itarahisisha mipango ya EAC kwenda kasi kwani mambo ya kusubiri wanao suasua kwa kigezo cha kua na hofu ya washirika wenzake eti wanataka udongo wa tanzania haiwezi jenga EAC,nafikiri hawa viongozi wamaliona hilo,EAC haita vunjika instead sasa ndio inaenda kuonekana kwa vitendo.
hata wakiendelea wewe inakuhusu nini? usiposimama wewe kwanza hakuna wa kukusimamisha! we unafikiri watatushika mikono ili tunyanyuke au watatukira zaidi ili tushindwe kusimama milele?
 
it is from tz that all these countries were reached by wazungu and got where they are today.mombasa was part of Zanzibar remember. Tz is EAC period.
 
EAC haita vunjika mimi ni nacho ona ni TANZANIA kuondolewa au kujiondoa katika community sio kuvunjika,tatizo watanzania wengi wanafikiri TANZANIA ndio EAC,sio hivyo,naimani kwamba kutoka kwa tanzania itarahisisha mipango ya EAC kwenda kasi kwani mambo ya kusubiri wanao suasua kwa kigezo cha kua na hofu ya washirika wenzake eti wanataka udongo wa tanzania haiwezi jenga EAC,nafikiri hawa viongozi wamaliona hilo,EAC haita vunjika instead sasa ndio inaenda kuonekana kwa vitendo.
Rudi kwenu Rwanda nani asiejua hila zenu pale Kivu...
 
Wasepe tu wanaonekana wanawivu flani,wakati wa Kibaki mambo yalikuwa fresh ila toka aingie HK naona jamaa kama anakachuki flani na Tz,PK nae anataka maslai yake yasipingwe ila kamu7 kanauma na kupuliza..
Tz sio shamba la bibi,waliyoyafanya Kivu ili tutsi waanzishe kanchi kao wamebugi bongo...
 
EAC haita vunjika mimi ni nacho ona ni TANZANIA kuondolewa au kujiondoa katika community sio kuvunjika,tatizo watanzania wengi wanafikiri TANZANIA ndio EAC,sio hivyo,naimani kwamba kutoka kwa tanzania itarahisisha mipango ya EAC kwenda kasi kwani mambo ya kusubiri wanao suasua kwa kigezo cha kua na hofu ya washirika wenzake eti wanataka udongo wa tanzania haiwezi jenga EAC,nafikiri hawa viongozi wamaliona hilo,EAC haita vunjika instead sasa ndio inaenda kuonekana kwa vitendo.

Wacha ionekane kwa vitendo kwao. Sisi EAC haitufai. I really hate it! Tanzania itoke tu kwani mie sioni cha kupoteza. Ninachokumbia ni kwamba kasi ya maendeleo itakuwa ileile kwa Tanzania. Labda viongozi wetu watuangushe. Hapa tulipo tumefika bila ya EAC. Na bado mipango yetu ni mizuri kutupeleka pazuri. Mimi sioni ubaya wao waliojitenga wakiendelea. Kwani wewe unamuacha mke kwa sababu hutaki aendelee au ni kwa sababu hakufai?
 
Bubu Msemaovyo,
Nakubaliana na wewe kwa yote uliyosema kasoro moja tu; nalo hiyo kutimia kwa heading yako! Sina shaka kabisa kwamba ingekuwa ni Rais mwingine, EAC isingechukua hata miezi sita ijayo!! Lakini kwa JK, I doubt unless movie ianzie bungeni!

Hata tusivyompenda, JK ana busara sana yule mzee! Kwa bahati mbaya, busara zikizidi zinageuka na kuonekana kama udhaifu na ndio maana sikushangaa Mnyika alipomuita JK ni dhaifu! Pamoja na busara, JK ana sifa nyingine isiyo na shaka kabisa! Hii ni ile ya ustahimilivu! Ustahimilivu wake ni too much to the extent ni rahisi ku-conclude kwamba ni udhaifu! JK ana sifa nyingine; sifa hii ndiyo inayowagharimu wana-CHADEMA! Mnamwa-undermine sana yule mzee kumbe yule mzee ni very smart katika ku-beat up external pressures! Hebu rejea mlivyopigwa(au umehakama CHADEMA??!!) changa la macho kwenye suala la katiba hivi karibuni pale akina Lissu walipoenda Ikulu! Kwa hiyo, kwa ujanja wake ule ule wote watatulizwa! Ukichanganya hayo yote; sifa za mtu kama huyo zinakuwa kutofanya maamuzi ya haraka; si kwamba ni slow learner, watu wa aina hii huwa hawayumbishwi na external pressures! Kashikashi anazokutana nazo JK ingekuwa ndo Mkapa; ingekuwa watu wengi hivi sasa wamefungwa na wengine kuuawa kuliko wale ambao inaonekana leo hii wameuawa kipindi cha JK! Mkapa alikuwa anatingishika sana na external pressure; wenyewe tunaita ni ukali; alikuwa hataki masihara kumbe ule nao ni udhaifu; defensive mechanism! likuwa hawawezi how to overcome pressure psychologically!

Kutokana na hayo, sina shaka kwamba JK atajaribu kuvuta vuta kidogo, na ikibidi EAC isife kwenye mikono yako! Na ukiona na yeye anahidhinisha kujitoa EAC leo; basi angekuwa mwingine angefanya hivyo miezi sita kabla! Lakini yote kwa yote; na sisi tusidakwe kati kati ya hii psychological torturing iliyoasisiwa na Kenyatta na kupata uungwaji mkono na akina Kagame ambao tayari waliyakuwa na yao nyoyoni! Hii ni psychological attack anayoifanya Kenyatta ili Tanzania tu-loose focus na kukurupuka kwa kuamini kwamba wenzetu wanatuacha! Wenyewe wanasema tunasuasua, kumbe wanafahamu kusuasua kwetu ni kwa ajili ya kulinda maslahi yetu! wanataka tufanye faster, kwahiyo lazima watushitue!

Bubu Msemaovyo, je jinsi yako ni sawa na hiyo avatar yako? Let me assume so! Je, unajisikiaje pale unapomtisha Boyfriend wako kwa kumwambia kwa ukali "kuanzia leo usinifuate fuate na wala simu usinipigie!" Halafu jamaa ndo kwanza anakuambia "safari njema mama!" Ulifanya yote ukidhani atatishika, na kwamba pale utakapoanza kuondoka ulitarajia atakushika mkono! Kutahamaki ndo kwanza jamaa anaingia kuoga! Hawa jamaa wanatarajia sisi tu-panic ili tuwashike mkono tuwaambie wasituache!
 
Last edited by a moderator:
Ivunjike tu. Wivu, choyo na kijicho dhidi yetu kina wasumbua. Wanatamani ardhi yetu, na kupendwa kwetu ulimwenguni. Tusha wapita hoa, sisi sasa ni second world.
 
EAC haita vunjika mimi ni nacho ona ni TANZANIA kuondolewa au kujiondoa katika community sio kuvunjika,tatizo watanzania wengi wanafikiri TANZANIA ndio EAC,sio hivyo,naimani kwamba kutoka kwa tanzania itarahisisha mipango ya EAC kwenda kasi kwani mambo ya kusubiri wanao suasua kwa kigezo cha kua na hofu ya washirika wenzake eti wanataka udongo wa tanzania haiwezi jenga EAC,nafikiri hawa viongozi wamaliona hilo,EAC haita vunjika instead sasa ndio inaenda kuonekana kwa vitendo.
Kadanganye wengine huko, hakuna anayesuasua; watu wanafanya mambo kwa kuangalia maslahi yao! Hatuwezi kukurupuka ili tuonekane tunaenda kwa kasi bila kuzingatia national interest! Hata vuguvugu linaloendelea sasa ni kwa ajili ya maslahi ya nchi za wahusika; ingawaje pale ni maslahi ya Kenya zaidi! Watanzania hawawezi kuwa wapumbavu wa kushiriki development of nothern corridor wakati haina faida yoyote kwetu! Rwanda na Uganda wanatumiwa tu kama mazuzu; kama wewe ni Mkenya basi utakuwa unaongea la msingi otherwise utakuwa nawe na wananchi wenzako mnatumika tu! Kenyatta alivyo mjanja juzi akawapelekea Sudan ya Kusini ili wajione kwamba wana-expand wakati busara ya kawaida wala haioneshi ni namna gani nchi kama Rwanda wanaweza waka-benefit na uwepo wa South Sudan wakati pamoja na mambo mengine, hana ubavu wa kushindana na Kenya kugombea soko la Sudan!
 
Back
Top Bottom