Bubu Msemaovyo,
Nakubaliana na wewe kwa yote uliyosema kasoro moja tu; nalo hiyo kutimia kwa heading yako! Sina shaka kabisa kwamba ingekuwa ni Rais mwingine, EAC isingechukua hata miezi sita ijayo!! Lakini kwa JK, I doubt unless movie ianzie bungeni!
Hata tusivyompenda, JK ana busara sana yule mzee! Kwa bahati mbaya, busara zikizidi zinageuka na kuonekana kama udhaifu na ndio maana sikushangaa Mnyika alipomuita JK ni dhaifu! Pamoja na busara, JK ana sifa nyingine isiyo na shaka kabisa! Hii ni ile ya ustahimilivu! Ustahimilivu wake ni too much to the extent ni rahisi ku-conclude kwamba ni udhaifu! JK ana sifa nyingine; sifa hii ndiyo inayowagharimu wana-CHADEMA! Mnamwa-undermine sana yule mzee kumbe yule mzee ni very smart katika ku-beat up external pressures! Hebu rejea mlivyopigwa(au umehakama CHADEMA??!!) changa la macho kwenye suala la katiba hivi karibuni pale akina Lissu walipoenda Ikulu! Kwa hiyo, kwa ujanja wake ule ule wote watatulizwa! Ukichanganya hayo yote; sifa za mtu kama huyo zinakuwa kutofanya maamuzi ya haraka; si kwamba ni slow learner, watu wa aina hii huwa hawayumbishwi na external pressures! Kashikashi anazokutana nazo JK ingekuwa ndo Mkapa; ingekuwa watu wengi hivi sasa wamefungwa na wengine kuuawa kuliko wale ambao inaonekana leo hii wameuawa kipindi cha JK! Mkapa alikuwa anatingishika sana na external pressure; wenyewe tunaita ni ukali; alikuwa hataki masihara kumbe ule nao ni udhaifu; defensive mechanism! likuwa hawawezi how to overcome pressure psychologically!
Kutokana na hayo, sina shaka kwamba JK atajaribu kuvuta vuta kidogo, na ikibidi EAC isife kwenye mikono yako! Na ukiona na yeye anahidhinisha kujitoa EAC leo; basi angekuwa mwingine angefanya hivyo miezi sita kabla! Lakini yote kwa yote; na sisi tusidakwe kati kati ya hii psychological torturing iliyoasisiwa na Kenyatta na kupata uungwaji mkono na akina Kagame ambao tayari waliyakuwa na yao nyoyoni! Hii ni psychological attack anayoifanya Kenyatta ili Tanzania tu-loose focus na kukurupuka kwa kuamini kwamba wenzetu wanatuacha! Wenyewe wanasema tunasuasua, kumbe wanafahamu kusuasua kwetu ni kwa ajili ya kulinda maslahi yetu! wanataka tufanye faster, kwahiyo lazima watushitue!
Bubu Msemaovyo, je jinsi yako ni sawa na hiyo avatar yako? Let me assume so! Je, unajisikiaje pale unapomtisha Boyfriend wako kwa kumwambia kwa ukali "kuanzia leo usinifuate fuate na wala simu usinipigie!" Halafu jamaa ndo kwanza anakuambia "safari njema mama!"
Ulifanya yote ukidhani atatishika, na kwamba pale utakapoanza kuondoka ulitarajia atakushika mkono! Kutahamaki ndo kwanza jamaa anaingia kuoga! Hawa jamaa wanatarajia sisi tu-panic ili tuwashike mkono tuwaambie wasituache!