Nchi Kavu
JF-Expert Member
- Sep 11, 2010
- 4,289
- 2,472
Dah! Hii vita ni ngumu. Nimejitutumu kuianzisha nikijua silaha zangu chache ila nikawa mbishi. Nikafanikiwa kumpata mateka mmoja ambaye maadui hawaishi kutuvamia kutaka kumchukua. Wana silaha kali na za kisasa. Wanashambulia kila pande. Nami napiga goti nikiomba huku nikitumia visilaha vichache kujilinda mi na mateka wangu. Mateka keshaanza kupenda silaha zao. Anatamani kwenda upande wao. Namuambia tulia nimeagiza silaha lakini siku zinasogea hazioni, japo anajua ramani zote za mi kupata silaha. Anajua zitakuja ila anaona zitachelewa. Ana hofu tunaweza kushambuliwa na yy akadhurika. Mwambieni mateka wangu anipe muda. Silaha zinakuja nyingi ila zinacheleweshwa tu na wahadidhina. Mateka anapenda ahadi zangu. Anapenda ninavyoweza kupambana japo na silaha chache. Lakini mateka anakaribia kukata kamba. Mwambieni mateka wangu avumilie. Anakotaka kwenda sio. Au basi aende? Yakizidi nitamwambia mateka wangu, basi nenda...