Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,595
- 215,272
Babu yangu alikuwa Muislamu, alibahatika kupata elimu enzi za Mjerumani,akiwa shule abadili dini na kubatizwa. Alifanya kazi kwenyel serikali ya Wajerumani pia Waingereza.
Alipopata mchumba ilibidi mchumba abadili dini na walifunga ndoa kanisani. Ingawa alikuwa Mkristu, bibi alitufundisha Juzuu tukiwa wadogo. Alifariki akiwa na 100+, kabla mauti kumfika aliomba sana aitiwe Imamu lakini watoto wake Wakristu walimpuuza.
Sasa hivi familia ni kama imegawanyika, binamu zangu wanabadili dini kwa kasi ya umeme. Wengi wanapata wachumba Waislamu. Si wanaume si wanawake.
Sasa hivi hata kwenye misiba hatuli tena kiti moto hata misa ikifanyika wengi wanabaki pembeni.
Ndoa inaweza kufungwa kicserikali ina maana haina dini, sasa msiba usio na dini tutaufanya vipi?