Ninakwenda mafunzo ya JKT...

Ninakwenda mafunzo ya JKT...

Status
Not open for further replies.

Dr. Mwigulu Nchemba

Tanzania Prime Minister
Joined
Feb 25, 2012
Posts
419
Reaction score
2,185
Wana JF, salam!

Nategemea kushiriki mafunzo ya JKT yatakayoshirikisha wabunge vijana. Nafanya hivyo kwa ajili ya NCHI YANGU, VIJANA WENZANGU NA CHAMA CHANGU.

Nawatakia ujenzi mwema wa taifa kwa kutumia ubao huu/tuition hii ya bure itoayo elimu ya maisha ie JF.
 
Haya bwana kila la kheri 'Kamanda', hope utarudi salama.
 
Hongera mkuu kwa kwenda mafunzoni kwa mujibu wa sheria.
 
Kafunzwe kuishi na watu na kuwa mzalendo wa kwel wa hii nchi na si mshabiki wa chama
 
Barua imeonesha muda wa kuanza tu ila najua sio mwaka mmoja ni kipindi kisichopungua wiki tatu wala si zaidi ya miezi mitatu
hayo ni mafunzo gani ya kijeshi ya wiki tatu!!! huna haja ya kutuaga we nenda tu hiyo ni mipango yako na ujifunze jinsi kutumia na kuifazi Bastola vizuri.
 
Barua imeonesha muda wa kuanza tu ila najua sio mwaka mmoja ni kipindi kisichopungua wiki tatu wala si zaidi ya miezi mitatu
hahaha, you are another! Hata mwenza wako umemjibu hivyo? Kuwa unajua tarehe ya kuanza na haujui ya kumaliza?
Jeshi litakuongezea maarifa kidogo. Kila la kheri. Ukifika tu uulize tarehe ya kumaliza ili utufahamishe tuje graduation yako!
 
Hongera mkuu.
Ila kampeni hii imekaa kibaguzi sana aise.
Huku mitaani kuna watu ambao hawakupitia mafunzo ya kijeshi sasa wana hamu ya kua miongoni mwa jeshi la akiba lakini hawajui wapi waanzie,by the way hongera sana na ukirudi salama usisite kutujuza.
 
Hongera na mafunzo mema ili kufahamu nini maana ya Nidhamu na Uzalendo
 
Kwanza nikukumbushe kuwa wewe siyo kijana, PILI nenda JKT labda utaweza kufumbuliwa macho upate uzalendo ndo ufahamu kuwa CCM ni chama kisichotufaa hata kidogo ktk nchi hii na chapaswa kufutwa ktk ramani ya siasa. TATU labda utajifunza kuongea kwa hoja badala kutukana matusi yalokujaa mdomoni.

Lakini kubwa kuliko yote ni kuwa JASIRI HAACHI ASILI. Utabaki yule yule kwani mbwa mzee hawezi kufundishwa mbinu mpya!
 
Hapa kuna kitu Mwigulu si kawaida yako kabisa kutushirikisha mambo yako hapa JF. Ila utakuwa mjanja sana, haya kila la heri kiongozi tunashukuru umegundua kama ya maana yote yanapatikana JF
 
Nakutakia Mafunzo mema na afya njema ili upate kumaliza salama...ucsahau kuupia updates za huko mkuu Mwigulu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom