Ninajuta kwa niliyoyafanya

Ninajuta kwa niliyoyafanya

Hapo mkuu asigwa jipe muda tu, wanasahau haraka sana hizi warning.

She probably wanted to tell us that she is available now.
Kweli mkuu, kuna mtu alinitonya PM za usiku huwa zinafanikisha sana hizi harakati, ukiandika night kali wakati amelala ila anaamka tu anaikuta PM lazima aelekee kibra.

Ngoja na mie nijaribu bahati yangu kwa staili hii mkuu
 
Pole sana, ila ulishakosea na usiendelee kuangalia nyuma, tazama mbele kisha tafuta upenyo wa kutokea. maisha bado yako.

utafanikiwa tu ila kwa sasa somo limekupitia na kwa kuleta humu wengine watajifunza pia. Kuna mambo hutokea kwenye maisha ili tu mtu ajifunze somo fulani ambalo hakuna pengine pa kujifunza ila katika matukio kama hayo.

Fursa bado zipo, punguza stress na usikate tamaa wala usiwe desparate kwani itakufanya usione opportunity na hata akitokea mwingine ukiwa stressed hawezi kukuapproach eagerly kama ambavyo ukiwa huru na bado unatemebea na tabasamu lako.

you are still young and life holds a lot still for you. Be ready to see and receive when it presents to you.

Stay Alive!!!
 
Wewe shida yako ni kukosa tu kazi na maisha kukuzomea ila seem upendo haupo moyoni mwako na hata ukipewa second chance bado utakuja kuishi katika rangi yako halisi! Mwache kaka wa watu aendelee na maisha yake, unapaswa kujitambua sasa na kuwa fundisho kwa wenye tabia kama zako!
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Mbona hakuna cha kujuta hapo.

Hio scenario uliyoitaja ni simple foolish age tu ilikusumbua, ukikuta mtu anajuta kwa aliyoyafanya katika foolish age ujue bado hajatoka kwenye foolish age pia, mtu mzima huwezi kubeba guilty kwa sababu ya foolish age.

Foolish age simply ni foolish age tu, hakunaga kuijutia, labda kama useme unamisi mihela yake na mafanikio yake aliyoipata huyo jamaa.

Shake off the dust and move on lady.............

Mkuu anachojuta ni hiki
"..Maisha yanaonekana magumu sana kwangu soon baada ya kumaliza chuo na kurudi nyumbani, ueklekeo umebadirika kabisa na sijui mwisho wake ni upi,......"

".............Kitu kingine kinachoniumiza zaidi tena sana naskia yule kaka amefanikiwa sana kwa sasa, napata wakati mgumu sana kama nitapata mtu mwenye maisha ya upendo na mazuri kama yeye"


ANAYAMISS MAISHA MAZURI........Aendelee kusali kwa imani yake
 
Unachojuta sio kumuacha huyo mtu..... Unajuta
Huna kazi, huna mtu wa kueleweka, jamaa kaoa tena ana mafanikio so unatamani we ndo ungekua wife

Tafuta kazi, maisha tuendelee shit happens unachojutia hakuna, wengine tumepitia mauza uza hapa hata uhakika wa kuingia peponi haupo!!!! Tunagonga cheers maisha yanaendelea
 
Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 25 na miezi karibu 9, ni mhitimu wa shahada ya kwanza katika chuo kimoja hapa Tanzania, sijaolewa na kwa dini mimi ni mkristo wa kuzakliwa na kubatizwa.

Katika maisha yapo mengi ambayo mtu unaweza kuyafanya na baadae ukajutia kwa nini umeyafanya na akili gani imekutuma uyafanye, binafsi najuta kwani nimekuwa mpumbavu kiasi hiki, najuta kwa nini nilifanya haya yote na kwa akili gani ilinituma niyafanye haya, inawezekana May be it was not planned but why I did this?

Nakumbuka nikiwa secondary nilikutana na handsome boy mmoja ambaye namfahamu hadi kwao, sikujua intention yake by then but I think nilikuwa mtoto. huyu mkaka aliniita sehemu mbalimbali nilikubali kuwa nakutana nae and the guy was very decent til now the guy is decent, hakuwahi kunionesha kama ananitaka kimapenzi kwa kipindi chote ambacho nimekuwa naye, alikuwa ananisaidia sana by then na soon b aada ya kuingia chuo, aliniomba tuwe wapenzi, sikukubali wala sikukataa, nilibaki katikatikati ila nilikuwa naendeshwa na mkumbo wa shule sababu sikujua kama ule muda was right for to make a very huge decesion.

Nilikubali baadae lakini nilibadilishwa sana na upepo wa chuo sababu niliwekeza kwenye bata zaidi bila ya kuangalia mbele yangu, baadae niliamua kumkataa kabisa huyu kaka sababu hakuwa karibu na mimi na kingine nilipata watu wengine ambao walikuwa karibu na mimi na nilikuwa napewa pesa ya kutosha so to me life nililiona zuri sana. yule kaka hakutaka sana malumbano na mimi na baada ya kugundua aliamua kuendelea na maisha yake na naskia ameoa tayari.

Maisha yanaonekana magumu sana kwangu soon baada ya kumaliza chuo na kurudi nyumbani, ueklekeo umebadirika kabisa na sijui mwisho wake ni upi, kama kaka huyu atasoma haya maneno yangu na kuhisi machungu yangu naomba sana anisamehe kwa yote, I wish nirudishe wakati nyuma, kampani na wale wote walionidanganya hawapo tena karibu yangu, nimekaa nyumbani hata kazi sina, sina kitu na sina pakujishikiza, I feel so much pain.

Kitu kingine kinachoniumiza zaidi tena sana naskia yule kaka amefanikiwa sana kwa sasa, napata wakati mgumu sana kama nitapata mtu mwenye maisha ya upendo na mazuri kama yeye, marafiki zangu kila nikiomba ushauri wako wananisema na kunilaumu, najua nishakosea ila naomba ndugu zangu mnishauri nifanye nini? mimi sio wa kwanza kukosea, maisha najua yataendelea lakini je kwa style ipi? najuta sana na kila nikisikia mtu anamuongelea huyu kaka naskia kama nataka kupasuka, nikialikwa harusini nashindwa kwenda sababu nahisi nayeye atakuwepo kwani asilimia kubwa ya watu anaowafahamu nawajua pia, nina wakati mgumu sana naomba mnishauri.
uliyoyafanya umeshayafanya na hayahusiani chochote na huyu jamaa. hili ni la kwanza inabidi ulikubali. Tafakari maisha yako na mbinu za kujikwamua bila ya kuhusisha chochote na huyo mtu. Kama kweli alikuwa mstaarabu basi na wewe mfanyie ustaarabu maana umesema keshaoa, muache akae na ndoa yake. Jamaa hakupaswa kuwa wako na ugumu wa maisha yako kwa sasa hayamaanishi ni ugumu wa milele. Yote yatapita na chukulia hivi vyote ni kama changamoto za maisha zinazokukuza kiakili na kukufanya ujue thamani ya kitu utakapokipata ili usije kujuta tena.
Penye Mungu hakuna linaloshindikana, u are young and educated with a prospective bright future ahead of u muombe Mungu wako akupe wepesi wa kufikia matarajio yako.
 
Hpa Ngoma ya Young Killer ft Banana umebadilika.

Inachukua nafasi
 
Pole sana, ila ulishakosea na usiendelee kuangalia nyuma, tazama mbele kisha tafuta upenyo wa kutokea. maisha bado yako.

utafanikiwa tu ila kwa sasa somo limekupitia na kwa kuleta humu wengine watajifunza pia. Kuna mambo hutokea kwenye maisha ili tu mtu ajifunze somo fulani ambalo hakuna pengine pa kujifunza ila katika matukio kama hayo.

Fursa bado zipo, punguza stress na usikate tamaa wala usiwe desparate kwani itakufanya usione opportunity na hata akitokea mwingine ukiwa stressed hawezi kukuapproach eagerly kama ambavyo ukiwa huru na bado unatembea na tabasamu lako.

you are still young and life holds a lot still for you. Be ready to see and receive when it presents to you.

Stay Alive!!!
 
ndio kawaidamnapendamaterial things bila kuangalia potential ya mtu na anakili gani na malengo gani...mnatuona watu ovyo kwa vile tumeacha magari na maisha ya home mazuri nakuanza maisha yetu kwa kuwa nai wanaume tena ya kuanza from zero kutafuta chako ukipewacha hom ni asante na ziada....sa hapo hatuna gari la home unendesha mara moja moja....sa kuwa kawida unachukuliwa poa hata kama umependa iuna malengo..mwisho wa isku unanotezea nami natumia busara si force ila baada ya muda unaona tofauti ya kutambuamaisha na kula bata...pole sana wa hivo wapo japo iso wote inategemea namakili ya mtu....umejifunza anza upya bahati mbaya age nayo inafanya wanaume tuangalie wa kuoa kutokana na umri wetu pia....usipoteze uarfiki kwa kula bata...rafiki yako wa leo ndio mumeo au mkeo wa kesho....msidharau wanaume wa XXXXX
 
Kwenye maisha ni vizuri ukajitahidi kutumia Akili yako katika kufikia maamuzi. Hili sio funzo kwako tu bali hata kwa kina dada wengine. Msikubali "kushikiwa akili".

Una elimu, una afya njema, pambana. Kama yeye kaweza kuyapata maisha wewe unashindwa nini?
 
I guess huyo kaka asingekuwa amefanikiwa kama ulivyosikia hata usingeumia. Anyway, sometimes we learn things the hard way. Don't blame yourself no more, chukua hilo somo lako, Jisamehe afu yaache maisha yaendelee.

Douta ulipotea sana, pole na majukumu.
 
if
Mbona hakuna cha kujuta hapo.

Hio scenario uliyoitaja ni simple foolish age tu ilikusumbua, ukikuta mtu anajuta kwa aliyoyafanya katika foolish age ujue bado hajatoka kwenye foolish age pia, mtu mzima huwezi kubeba guilty kwa sababu ya foolish age.

Foolish age simply ni foolish age tu, hakunaga kuijutia, labda kama useme unamisi mihela yake na mafanikio yake aliyoipata huyo jamaa.

Shake off the dust and move on lady.............

If I could turn back the hand of time, baby you will be mine...R.Kelly
 
yote hiyo mipango ya sir God. huko mbele amekuandalia mtu ambae mtapendana na mnaendana tabia. acha kufocus on the past. BE POSITIVE
 
Back
Top Bottom