Ninaiomba Serikali ifungue mtandao wa JamiiForums

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
34,054
Reaction score
79,396
Kheri ya Mwaka Mpya!

1. Kwa heshima na taadhima. Ninapenda kuchukua nafasi hii.

2. Kuiomba serikali iufungulie mtandao wa Jamiiforum ili mambo mengine yaendelee.

3. Jamiiforum ni moja ya mambo ambayo serikali ya Tanzania inaweza kujivunia kwa wananchi wake.

4. Malumbano, mivutano na migogoro iwe ya kisiasa au kijamii inaweza kuweko lakini isiwe sababu ya kurudisha jitihada na nguvu zinazoipaisha nchi yetu katika Nyanja kama za kiteknolojia na kidijitali.

5. Watu wengi ikiwemo serikali imefaidika na uwepo wa jamiiforum kuanzia kwenye elimu, habari, maarifa na mawazo mapya, ajira, miongoni mwa mambo mengine.

6. JF kupitia anonymous imesaidia serikali na vyombo vya usalama kupata baadhi ya data ambazo ingetumia nguvu nyingi kuzipata.

7. Ingawaje zipo changamoto za kashfa au tuhuma. Lakini suala hilo lisiwe sababu ya kufungiwa kwa mtandao mzima.

8. Naiomba serikali ifungulie mtandao huu. Hakuna haja ya hasira, chuki, kukomoana, kutunishiana misuli. Kuonyeshana ubabe.

9. Ukubwa ni busses, hekima, unyenyekevu kama sehemu ya kuonyesha njia ya Wema na kuwa mfano Bora wa UTU.

10. Mwaka 2026 mwaka wa UTU WA KALE.
11. No hate. One nation one destination.

Mungu awabariki.
Kwa walio Morogoro. Jioni tutakuwa Pale mjini. Kufurahia mwaka 2026.

TaikonMaster
Kwa sasa Soko la Kingalu, Morogoro Mjini
 
Sema ninaitaka sio ninaiomba,haki yetu haiombwi

Unataka kitu kilichochini ya uwezo wako.

Unaomba kitu ambacho kipo juu ya uwezo. Wako, au kipo Kwa mtu aliyejuu yako.

Mfano ukata kitu ambacho ni haki yako alafu mwenye nguvu akikuambia sikupi utafanyaje?

Kuomba ni hekima, busara, unyenyekevu.
Pia, unaweza kuwa juu lakini ukamwomba aliyechini kama ishara ya unyenyekevu.
 
Tumechoka kuomba haki zetu, sasa ni wakati wa kuzitaka na kuzidai, hii nchi sio mali ya CCM au genge fulani ambao wanajiamulia tu kugawa haki zipi na kunyang'anya zipi kadri wanavyojisikia.
 
Acha kutumia lugha ya kubembeleza kwa majizi ya kura na wauaji. Usiwape uhalali wasiokuwa nao. Inatakiwa waifungulie JF kupatikana Tanzania bila VPN haraka iwezekanavyo.
 
Tumechoka kuomba haki zetu, sasa ni wakati wa kuzitaka na kuzidai, hii nchi sio mali ya CCM au genge fulani ambao wanajiamulia tu kugawa haki zipi na kunyang'anya zipi kadri wanavyojisikia.

Upo sawa Mkuu. Lakini lengo la kuomba na kutaka wote ni kupata kitu Fulani.
 
Hatuombi Sema ni lazima ifungue
 
Acha kutumia lugha ya kubembeleza kwa majizi ya kura na wauaji. Usiwape uhalali wasiokuwa nao. Inatakiwa waifungulie JF kupatikana Tanzania bila VPN haraka iwezekanavyo.

Nifundishe lugha ninayotakiwa kuitumia.
Nipe mfano ningeandikaje.
Embu nipe mfano.
Mfano huo uzingatie heshima, utu, haki, upendo, ukweli, na maarifa
 
Uwe na uhalali kwanza ndio ikibidi uombwe. Yaani ukomoe halafu uombwe, ili iweje kwa mfano? Huu ujinga huwa unafanywa na watu wenye hofu za siasa za kijamaa.
 
Nifundishe lugha ninayotakiwa kuitumia.
Nipe mfano ningeandikaje.
Embu nipe mfano.
Mfano huo uzingatie heshima, utu, haki, upendo, ukweli, na maarifa
Sema ni kwanini Serekali haiifungulii JF kupatikana Tanzania bila VPN? Yaani serekali hii ya majizi haipaswi kupewa lugha kuwa wanafungulia mitandao kama hisani. Acha kujikombokomba boss.
 
Ningeandikaje mkuu?
Wewe mkeo au mtoto wako ukimkosea akata haki yake atakuomba au atakudai kwa njia ipi?
Mahusiano ya raia na serikali yao sio sawa na mahusiano ya mke na mume au wazazi na watoto wao, mahusiano yetu na serikali ni ya "social contract" yanayoongozwa kwa katiba, uhuru, sheria na haki za msingi za binadamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…