Ninaacha Ualimu tangu leo

Ninaacha Ualimu tangu leo

Dumelang

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2011
Posts
3,267
Reaction score
5,854
Ndio maamuzi niliayoamua na hapa nafanya mpango kukusanya vyangu huku nilipo, najua life litazonga ila kipimo cha akili ni ugumu wa maisha, ipo siku nitatoka tu. Siwezi kuwa mtumwa kamwe.

Nilisimamia mitihani ya kidato cha pili, mtihani umeisha hatukulipwa hadi jana, jana watu wanalipwa nakuja kufatilia pesa yangu naambiwa jina langu halipo, leo nimuone afisa elimu, namuona leo anasema hakuna fungu nilisahaulika niandike Barua kufungua madai nitalipwa kwa OC (other chages) mafungu ya mkurugenzi.

Tafsiri yake ni kuwa limeshakuwa deni tayari hili, jasho langu, kila siku nilitumia tsh 8000 kwenda na kurudi kusimamia mitihani kwa siku saba. Kuja hapa halimashauri kutoka nnakoishi nakodi pikipiki elf 8 kwenda na kurudi kila siku, hapo bado kula, Nimetumia pesa eti leo nidai tena. HAPANA

Tangu nimeanza kazi nna miaka mitatu sasa ninaidai serikali, alafu leo niongeze tena kudai?

Kwa dhati ya moyo wangu nimeamua na sirudi nyuma, nimeachana na ualimu Rasmi, siwez kuwa mtumwa kwa haki yangu. Nita fight, nitatoka, sio wote wenye kazi ndio wanamudu maisha .
 
Kama ni kweli Hongera kwa kukata minyororo ya kitumwa
 
Hongera sana sana, mimi niliacha zamani kidogo, na niliweka thread miaka ya baadae hapa jamvini na nilitoa sababu, wengi walinipinga lakini kweli sijawahi kujuta! Yalikua maamuzi ya "kijinga" kwa kipindi kile ila nashukuru Mungu naendelea mbele
 
Busara ni pamoja na kukubaliana na hali halisi ya maisha, kupambana kwa njia ya haki na kupata haki yako bila kuchoka, kuteteleka au kuacha.
 
acha uamuzi wa jazba,,,,,,hizo ni taratibu za kawaida za malipo,,,ukianguka jitahidi kuamka tena na tena na tena,,utafanikiwa,,,jitahidi pia kuwa mjasiria mali pamoja na kazi yako maana mimi mwenyewe naitamani sana kazi yako maana inakupa muda wa kufanya ishu zake mtaani,,,kazi ninayoifanya ndugu inabana huna hata muda wako wa kupumzika,,,pia upambanaji....
 
Kama ni kweli Hongera kwa kukata minyororo ya kitumwa

Mkuu sirudi nyuma, kabla ya kuwa mwalimu mie nilikuwa fighter kitaa na nilikuwa silali njaa. Siwezi kuwa mtumwa kwa haki yangu kabisa nnayohistahili.
 
maisha ya kitaa sio mchezo.
utasugua mpaka uta utamani tena ualimu,komaa apo apo huku ukiendelea kupiga ishu nyengne
 
Kaka usikate tamaa, lumbuka nchi jnaongozwa na waalimu, nakusihi pigania haki zako na kwa vile una ujanja wa kuja hadi kweny mitandao.. Unaweza kufikisha ujumbe wako kwa wahusika kirahisi sana.
Fight for your right and never give up!
 
Ndio maamuzi niliayoamua na hapa nafanya mpango kukusanya vyangu huku nilipo, najua life litazonga ila kipimo cha akili ni ugumu wa maisha, ipo siku nitatoka tu. Siwezi kuwa mtumwa kamwe.

Nilisimamia mitihani ya kidato cha pili, mtihani umeisha hatukulipwa hadi jana, jana watu wanalipwa nakuja kufatilia pesa yangu naambiwa jina langu halipo, leo nimuone afisa elimu, namuona leo anasema hakuna fungu nilisahaulika niandike Barua kufungua madai nitalipwa kwa OC (other chages) mafungu ya mkurugenzi.

Tafsiri yake ni kuwa limeshakuwa deni tayari hili, jasho langu, kila siku nilitumia tsh 8000 kwenda na kurudi kusimamia mitihani kwa siku saba. Kuja hapa halimashauri kutoka nnakoishi nakodi pikipiki elf 8 kwenda na kurudi kila siku, hapo bado kula, Nimetumia pesa eti leo nidai tena. HAPANA

Tangu nimeanza kazi nna miaka mitatu sasa ninaidai serikali, alafu leo niongeze tena kudai?

Kwa dhati ya moyo wangu nimeamua na sirudi nyuma, nimeachana na ualimu Rasmi, siwez kuwa mtumwa kwa haki yangu. Nita fight, nitatoka, sio wote wenye kazi ndio wanamudu maisha .

Kiongoz huku mtaan ni kugum sana nakushaur futa kauli yako mapema utakuja juta labda kama una Mishe tayar za kufanya
 
Oke unaonekana umesha amua na haurudi nyuma.

Ili upate kianzio cha kufight huku kitaa nenda pale crdb chukua mkopo wa 15mil then achana na hiyo kazi watakata kwenye mshahara wako kulingana na mkataba wako na benki huku wewe ukiendekeza ambisheni zako huku kitaa

Karibu.
 
Mkuu kweli hili lako lenyewe hilo, ahsante kwa akili. Hapa ndio starting point
 
vijana wanachezea maisha hawa, huku mtaani ni kugumu sana kabla ya kuchukua maamuzi hayo ungeomba kwanza ushauri ili watu tukupe uhalisia wa huku unakotaka kuja. huku kugumu mkuu pambana huko huko. unaweza kuwa mjasiliamali huku bado ukawa mwalimu kwa sababu mwl leo anakopeshwa hadi milion 15 kwa makato ya 5 yrs
 
Nashauri uombe likizo isiyo na mslipo badala ya kuacha kabisa, kakae uswahilini hata miaka miwili, ukishindwa kabisa rudi kazini kwako!
 
Umeshaandika barua kutoa taarifa au unataka comment......!!!
 
Vipi ticha number zinasomeka?
Utajuta kwa nini uliuza haki za watu kwa kusaidia mfumo onevu.
Pongezi kwa kula kile ulichopanda.
Sasa panda mbegu sahihi, usirudie makosa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom