Nina wasiwasi na tabia ya mshikaji wangu

Nina wasiwasi na tabia ya mshikaji wangu

ijoz

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2012
Posts
731
Reaction score
719
Amani kwenu nyote...

Wakuu, kuna tabia ya mtumishi ninayefanya nae kazi ofisi moja inanitatiza kidogo, japo sijapenda niifanye akili yangu iamini mabaya zaidi juu yake.

Huyu mshikaji ni mwanaume mwenzetu, lakini ni mtu anayependa sana mambo ambayo yanakuwa associated na wanawake. Kwanza ni namna anavyozungumza, anatumia zile gestures za kike kama kubinua midomo/lips, na kupenda kuzungumza akiwa kajishika kiuno,kuchezesha mikono na vitu vinavyofanana na hivyo (naamini mnapata picha ya ninachomaanisha).

Pia hupenda sana kusikiliza taarabu, yaani akiingia kwenye computer yeye hupenda nyimbo za taarabu, na anaimba nyimbo hizo mwanzo hadi mwisho, tena kwa hisia kali, na CD zake nyingi ni za taarabu
Kingine, yeye na mambo ya football hana interest nayo hata kidogo...yani anakwambia zaidi ya kaseja na Nizar Khalfan (hawezi kumkumbuka mchezaji mwingine yeyote) na hana timu/club yeyote anayoshabikia.
Hayo yote tisa...

Sasa kuna mtumishi mwenzetu (mwanaume) wa idara tofauti ambaye hawajozoeana zaidi ya kukutana mara chache kwenye vikao, alichoniambia ndicho kilichonifanya nije hapa nisimulie habari hii.

Ni kwamba huyo mshikaji tuliye nae idara moja ameanza tabia ya kumtumia huyo mshikaji mwingine (asiye na mazoea nae) sms za ajabu kama vile g'9t..!!!, I miss u,na nyingine zinazofanana na hizo (hivyo hivyo kama nilivyoandika,kumbuka wote hapo ni wanaume) huku akijua kuwa huyo mshikaji anamke tena wa ndoa...! (Hizo sms nimeziona baada ya mshikaji allyetumiwa kunionesha na kuthibitisha pasipo shaka kuwa namba ni ya yule mshikaji.

Sasa jamaa wa idara nyingine baada ya kunionesha zile sms kanieleza kuwa hataki kufikiria mambo yeyote mabaya kuhusu mshikaji ninayefanya naye kazi idara moja , lakini hapendezwi na hizo sms anazotumiwa.
Baadhi ya akina dada tunaofanya nao kazi walishawahi kutueleza kuwa mwenzetu anatabia za kike, mi niliwakatalia, lakini sasa naelekea kukubaliana nao.

Sasa, yule anaetumiwa sms na huyo mshikaji kaniuliza ninafikiria nini kuhusu huyo jamaa,mi nimeshindwa kutoa hukummu.
Lakini tabia hii ikiendelea naona itatuchafua watumishi wenzake wa idara, hasa wanaume.
Mwenye msaada wowote wa mawazo please, anakaribishwa[/SIZE],
 
huyo yawezekana kazoezwa kuliwa na kula tigo,angekuwa hatumi sms ningemfikiria vingine kwa sababu nilishasoma na kaka mmoja kadekezwa mpaka kawa na mapozi ya kike,chakula chake chips,hawezi beba ndoo yuko legelege,anapenda kupiga story na wasichana,kushika kiuno,tembea na ongea yake sasa ndo usiseme lakini alikuwa hana huo mchezo mchafu ila malezi ndo yamemharibu lakini huyo mfanyakazi mwenzio nahisi ana mchezo mchafu mwanaume mwenzie anamtumia visms vya i miss you vya nini,ili iweje??????????????
 
Kudadeki mi dume eti mfanyakazi mwenzangu anitumia i miss you,g9t sijui makitu gani? Huo ugomvi wake angekuja kuamulia RPC/OCD kama sio mwema kabisa
 
Nisikudanganye ndugu yangu ningependa sana kumshauri mliwa tigo mwenyewe...wewe inakuwa ngumu nitakushauri nini sasa aaaaaaah, hapa pagumu mzeee...
 
Maumbile tu! Mungu alimchanganyia homoni, kapewa za ke yaani progesterone badala ya testosterone....nawafahamu vijana kama wawili nilikua nao miaka ya 84, hawakuwa mashoga ila tabia ndio kama za jamaa uliyemtaja, mmoja hadi leo kila akioa anaishia kuachika baada ya muda mfupi.
 
Njia nzuri ya kutatua tatizo ni kulikabili tatizo.
Maadam kuna ushahidi wa SMS na zinatoka kwake, mwekeni kitako chini huyo jamaa na mumueleze aache tabia hiyo ya kutuma hizo SMS.
Kukaa kimya ni kuongeza matatizo zaidi.
 
Nadhani ifike mahali tuheshimu uamuzi wa mtu as long yupo happy that's more important kwake na wewe cha msingi fuatilia vyako tatizo la culture ya tz haiheshimu maauzi binafsi
 
Halafu fikiria ana madevu madevu kama ukoko wa pilau au uchafu wa sumaku....arrrgghhh!!!

napata picha mwanaume anamuandikia mwanaume mwenzie af anamalizia na neno mmwaaaaaaaaaaaaah!
 
Hahahah....umechelewa kushakucha!!
si ndio namaanisha nilikumiss saa ngapi!mwe!habari nzito hii!
mtani hebu twende kumlipa mkoloni muda tuliomuibia jana!
ngastuka!
 
Hebu tumia akili japo kidogo...mwanaume amwandikie mwanaume mwenzake SMS za mahaba na bado unatetea habari za uamuzi wa mtu....!!!!

Nadhani ifike mahali tuheshimu uamuzi wa mtu as long yupo happy that's more important kwake na wewe cha msingi fuatilia vyako tatizo la culture ya tz haiheshimu maauzi binafsi
 
Back
Top Bottom