Nina wasiwasi na mke wangu...

Mkuu nilimruhusu sababu yakusema ameitwa na dadazake but haijulikani nini shida kwakuwa ni familia yake nikamruhu aende ili tujue nini shida huko
Hata kama ni ndugu zake sio ki rahisi hivyo huyo ni mkeo na hizo sababu za kuitwa ulipaswa uzielewe.

Bro inaonyesha sijui kama kweli unawafahamu ndugu zake, suala la kumwita tu mke wa mtu bila mwenye mke kupewa taarifa pia!! Mmmmh sidhani?

Hiyo ilikuwa ni safari ya kwenda kuliwa na inawezekana sio singida wala Dom, ni karibu karibu tu.

Pole sana ila.mambo ya ndoa yunakutana na mitihani sana.
 
Mapenzi yanaumiza sana,mie kuna binti nipo nae kwenye mahusiano ni Mwaka sasa-anaishi na Dada yake huwa ananieleza hawezi kutoka kwai mwisho kutoka kwao ni SAA 12 jioni.Mungu sio mzee mkumba Jana nimekutana nae katika grocery moja mida ya SAA 4 usiku akiwa na majamaa 2.Badaye namuuliza ananiambia ni marafiki zake kwa kweli nilihisi kuzimia mwili wote ulikosa nguvu ,Leo siku nzima sijalala kwa kweli.
Acha tu mie saizi upendo wangu najua nitapeleka wapi wabongo wanachoshaga sana
 
Dah!!! , wamejua kukujaza upepo umu ndani. Nahisi akirudi unaweza kuua Mana si kwa hasira ulizojazwa . ..ushauri ni bure Ila akili ni kumkichwa....vya kuambiwa changanya na mawazo yako....

Chonde chonde, punguza jazba...usije ukachukua maamuzi magumu, jela hautakuwa na mtu humu, utapambana mwenyewe .....kuwa na hekima tafadhali.
Yasikie kwa watu tu niliwahi kumpeleka shule binti Mmoja form 2 Hadi form six yupo fresh to ile amefika university niliona rangi zote
 
Hapana mkuu huwa naamua lakini hii sikutaka ku doubt coz nikimkataliga safar analalamika na kuona namuonea lakini pia nikwasababu tu kaeleza kuwa kaitwa na hajui nini shida kwa heshima tu za mashemeji nikamuacha aende ili akirud anieleze vizur hicho kilichomfanya akaitwa huko
Umefeli sana hujakomaa kiakili na mkeo anakumudu sana, badala ya kuchukua namba ya waliomuita uulize, kimsingi mwenye shida na mkeo anapaswa akupigie wewe ndio uambiwe shida, mkeo yuko ndani ya himaya yako, huyo mwanamke anakumudu sana, pole sana sana. Usikute hujatrack location ya simu ya mkeo muda wote unadanganywa.

Kmmmdake ndiomana kuoa ni ungese mtupu.
 
Usiongee mengi mkuu, tena sio dom tu huo mchepuko ametoka nao hapo dar kufika dom akaliwa akaenda singida kuzuga akarudi dom akapigwa mpaka vidonda vya tumbo vikasimama wahi stand ya basi bila ye kujua bana pembeni utaona anaagana na mume mwenzio..
 
Kudadeki ukitaka kujua jinsi watu wanavyopigiwa angalia Uzi huu unavotembea, hisia kama zote, huu ndio Uzi wa kusoma comments mume nguvu yake ikoje na anapaswa kuwa namna gani.
 
Bado hujachelewa unaweza kutrack ndani ya masaa 72 au 96 unaweza kujua simu ya mkeo imetumika ikawa minara ya sehemu gani technology Haidanganyi
 
Habar wana JF,
Naimani mko wazima.

Kiukweli nimekuwa na wasiwasi na safari ya wife, sijui kwanini lakini ni safari ambayo siielewi kabsa wakuu. Nina mashaka nayo coz naona mapicha picha tu.

Ni kwamba wife kasafiri juzi ijumaa kuelekea Singida lakini safari yake sielewi elewi kabisa, kwasabubu kwanza ni safari ya kushtukiza lakini pia mpaka now sielewi aim ya safari ni nini mpaka now.

Alhamisi amerudi kutoka kazini usiku tunalala ndiyo ananipa taarifa ya kuwa kesho Ijumaa anasafiri, nikamuuliza unaenda wap? Akaniambia kapigiwa simu na dada zake wamemuita ambao wanakaa Singida. Nikamuuliza kunatatizo akasema hapana, ila sijui wanashida gani na mimi ndiyo wamenipigia simu niende.

Kiukweli nilikuwa nimechoka nahitaji kupumzika, sikutaka ku complicate kitu, nikamjibu sawa nikalala. Then asubuhi nikajiandaa nikaenda kazini vizur. Niko job ananipigia simu kuwa ndiyo anatoka home anaelekea stendi kupanda bus. Iikuwa almost kama saa 7 hivi mchana nikamjibu haya na nikamuuliza kama kunakitu chochote anahtaji akasema hapana yuko powa.

Basi nikakata simu lakini kiukweli ghafla akili yangu ilishikwa na wasiwasi juu ya safari yake but sikutaka ku doubt anything nikapotezea. Baadaya kupita kama lisaa akanitumia message kuwa amepata basi but akifika Dodoma atashuka kuna ndugu yake anamchuka then wanaenda wote.

Daah, sikutaka pia ku doubt wala mambo mengi nikamjibu sawa, nikaachana naye nikaendelea na kazi zangu, but bado sikuona sababu ya yeye kushuka Dodoma. By saa 2 ndiyo ananiambia ndiyo wanaondoka Dodoma nikamjibu sawa safari njema tukaacha hivyo. Basi mi nikarud home usiku kwakuwa nilishapita somewhere nikapata chakula nikafika home niko good, nikaoga nikaingia kwa bed nikampigia ananiambia kashafika ila kachoka na safari nikamuacha nikapumzika.

Sasa leo Jpili tumeongea asubuh vizur tu na tukaagana baadae by saa 7 mchana ananiambia ndiyo anataka kurudi leo. Nikamuuliza mbona hukuniambia asubuhi na kwanini usingeondoka asubuhi? Sijaona cha maana anachonijibu, basi nikamwambia haya kama unarudi leo. Tuakaacha baada ya kama nusu saa ananipigia simu ananiambia kuwa yupo stendi, mara gari sijui hakuna, mara zimejaa, mara nimechoka nasikia usingizi, nikamwambia sasa siungebaki ili uondoke kesho asubuhi akasema sawa tukaacha.

Baadae ananitumia message eti amepata gari ila linaishia Dodoma kwaiyo atashuka Dodoma. Aloo nikasema kimoyomoyo hapo Dodoma hapo siyo bure, coz kwenda kashuka Dodoma kurudi baada arud kesho kama kweli kakosa usafiri na tumekubalina anarudi kesho mapema na sidhani kama kweli alikosa usafiri by that time ananiambia kuwa kapata usafiri.

Ila unaishia Dodoma so ataenda kulala Dom, sikutaka ku complicate nikamjibu sawa basi nikaachana nae. Ila cha ajabu baada ya hapo akawa kimya hakusema kama kafika au laa. Yaani ndo ananitumia text saa hii, saa 5 usiku kuwa alifika salama ila alishindwa kuniambia coz vidonda vya tumbo vilimshika akafikia kupumzika. Heheheh nacheka ila najua mwenyewe wakuu but sijamjibu na sitamjibu lakini namsubiri arudi kesho nikitoka kazini anieleze vizuri kuhusu hii safar yake.

Japokuwa mimi siyo mtu wa kumchunguza mwanamke na sipendi kabisa kuchunguza mtu sababu naelewa what’s gonna happen.

Wakuu kama kuna la kuniongezea karibuni sana, uwanja ni wenu.
Kwani mzee baba wewe ukiwa kama mwanamume aliyekamilika hauna kabisa michepuko?

Kama unao basi fresh ngoma droo. Potezea tu
 
Kwa waliosoma Cuba ni kwamba hiyo safari ilikuwa ya Dodoma na hakufika hata huko Singida. We muulize vizuri tu akueleze huko Doeoma alienda kufanya nini
 
Back
Top Bottom