Nina wasiwasi na hizi gesi

wakurochi

JF-Expert Member
Dec 4, 2017
2,647
2,938
Moja kwa moja kwenye wasiwasi wangu.

Ni kwamba natumia gas kupikia, siku zote hamna tatizo. Ila huu mtungi nilio nunua safari hii nimeshatumia kama mwezi, karibia 2, sasa naona harufu ya gas imebadilika sana ni kama harufu ya gesi ya kienyeji na pia ule moto mkali wa blue hamna, badala yake unatoka moto mwingi mpaka sufuria inakuwa na jivu na inabidi mpaka nirudishe kipimo karibu na 0 ili kupata moto wa blue, hata hivyo inakuwa bado.

Kabla sijawasingizia hawa watu wa gesi naona nipate ujuzi wa watu wengine kwenye jambo hili, kwani sijui wanajaza wapi wao. Usije ikawa ujanja mpya.

Nawasilisha bungeni JF
 
wakurochi,
Yawezekana gesi inakaribia kuisha. Pili pengine kabureta ya jiko lako haijakaa vizuri. Kabureta inachanganya gesi na hewa kwa uwiano mzuri, kama hewa ni kidogo mno basi moto huwa mwekundu na moshi huwa mwingi.
 
Unakumbuka hii????
EWURA yabaini kiwanda bubu cha kujanza gesi katika yadi moja iliyopo Mbagala Zakiem jijini Dar es Salaam.

1581420901091.png
 
Jaribu kubadilisha hivyo vipitisha moto inawezekana matundu yamekuwa makubwa, kama mpira wa kuunganisha jiko na mtungi umetumika kwa miaka 2 fikiria kuubadilisha.
 
Back
Top Bottom