Suala la umri lisiwape shida, kama mnapendana hapo si ishu. Sababu mojawapo ya watu kependekeza mvulana awe mkubwa kiumri ukilinganisha na msichana ni kwamba baadhi ya wanawake baada ya kujifungua miili yao huchoka (wanakuwa kama wazee ukilinganisha na wanaume walio zaa nao), hivyo ili kubalance ni mapendekezo mwanaume awe mkubwa, pia inasemekana wanaume na wanawake kichwani tuko tofauti, yaani uwezo wa kufikiri, kuwa na upeo mkubwa na kutatua changamoto za kimaisha (sijasoma tafiti zozote bado, ila ni maneno niyasikiayo na nina uhakika yako sahihi: kwa mfano watoto wawili wa miaka saba, mmoja wa kike mmoja wa kiume, endapo watawekewa maji nje ya kuoga na wakaanza kuoga, ghafla akatokea mgeni, mtoto wa kike atajitambua kuwa yuko uchi,anaweza akajificha ila wa kiume hataona tatizo lolote, hivyo hii inatumika hata ukubwani), kwa hiyo inapendekezwa pia msichana awe mdogo kiumri kwa vigezo kuwa kama wana umri sawa, basi kifikra msichana ni mkubwa zaidi ya miaka kadhaa na asilimia kubwa ya wanaume hatupendi kuwa chini. Ila cha msingi ni upendo uliopo kati yenu, na pia jinsi mnavyoendana. Mengine ni ya ziada tu. Kama haya yapo sawa, wala umri kwa upande wangu sioni kama ni tatizo. Usiache penzi la kweli likupite kwa kigezo cha umri. Kama wasemavyo: Age ain't nothing but a number.