Nina Shamba ekari 6 Mkuranga, ni kilimo gani chenye tija

mie nina heka 10 kibiti mwezi wa pili ninataka kupanda miche ya mikorosho kama zao la kudumu ambayo nitaanza kuvuna baada ya miaka 2 pia wakati mikorosha inakua nitakuwa nalima mihogo.Fanya hivyo mkuu
Mkuu tunaweza wasiliana na mimi Niko na eka 4 Kimanzichana nataka panda korosho.
 
Mkuu, habari ya wewe. Mimi pia nina shamba la ekari 10 Kimanzichana so i assume tuko kwenye same zone. Sijajua unataka kufanya kilimo cha aina gani ila nikushauri kama ninavyofanya mimi. Binafsi ninalima mihogo kwa sasa na mwezi wa kumi na moja natarajia kulima ufuta pia. Mihogo mwezi wa tisa ndio msimu mzuri kwa kupanda, ufuta mwezi wa kumi na moja. Kama una mtaji wa kutosha pia unaweza kulima Nanasi, Karanga na Matikiti maji maana hayo mazao yote yanakubali 100%. Karibu kwenye kilimo mkuu
Nimevutiwa na maelezo yako, hivi kibiashara zao la mhogo linalipa? Ukilima nusu heka kwa mfano faida (makisio tu) yake yaweza kuwa kiasi gani (mauzo kutoa gharama zake). Natangiliza shukran .
 
Hivi mkoa wa pwani nisehemu gani naweza pata heka kwa bei ya 200,000/= kama kuna mtu mwenye kujua anijuze tafadhali
 
Hbari ndugu,

Kama nilivyoeleza hapo juu nina ekari 6 na ningependa kuituma kujiongezea kipato kuliko kiwa shamba pori. Naulizia zao ambalo naweza kulima na likawa na tija. Sina tatizo la mtaji.

Papai Malaika F1 inafanya vizuri sana na inaanza kuzaa baada ya miezi mitano. Huko ukanda wa pwani zinafanya vizuri sana. Pia butternut inafanya vizuri sana hasa sehemu zenye jua kali kama huo ukanda wa pwani.
 
Butternut ni zao gani mkuu?

kuna vijiboga fulani vya manjano. Ukiviangalia vinakuwa kama vibuyu. Wazungu na wahindi wanayapenda sana kuliko haya maboga ya kawaida. Ukifanikiwa jaribu kununua na uyapike, ni matamu sana na yana unga mwingi kuliko maboga ya kawaida.Fungua hizo picah utoana hayo maboga.
upload_2017-12-23_20-54-53.jpeg
upload_2017-12-23_20-55-22.jpeg
upload_2017-12-23_20-54-53.jpeg
 
Mkuu kilimo cha ganja kinalipa sana, hapa nchini gunia moja inakwenda 1m - 1.5m ukifanikiwa kupeleka nje ndo umetoka kabisa... yani ukifanikiwa kutunza shamba lako vzr unaaga umasikini.!
 
Hbari ndugu,

Kama nilivyoeleza hapo juu nina ekari 6 na ningependa kuituma kujiongezea kipato kuliko kiwa shamba pori. Naulizia zao ambalo naweza kulima na likawa na tija. Sina tatizo la mtaji.
Mkuu Nami naweza pata heka 10 hapo Mkurangu ?
 
Back
Top Bottom