Nina Shamba ekari 6 Mkuranga, ni kilimo gani chenye tija

PARADIGM

JF-Expert Member
Sep 9, 2014
2,774
1,815
Hbari ndugu,

Kama nilivyoeleza hapo juu nina ekari 6 na ningependa kuituma kujiongezea kipato kuliko kiwa shamba pori. Naulizia zao ambalo naweza kulima na likawa na tija. Sina tatizo la mtaji.
 
Weka minazi.. Taduta miche ya kisasa ila itakuchukua takriban miaka mitatu kuanza kuvuna matunda
1469118402220.jpg
1469118406007.jpg
 
Hbari ndugu,

Kama nilivyoeleza hapo juu nina ekari 6 na ningependa kuituma kujiongezea kipato kuliko kiwa shamba pori. Naulizia zao ambalo naweza kulima na likawa na tija. Sina tatizo la mtaji.
Liko mkuranga ipi??
Kama huna cha kulifanyia basi niuzie tu tujue moja
 
kwa maeneo ya mkuranga n vema ulime ufuta au kalanga ..kama upo siriazi nitafute0625561992 tuongee zaidi mim n extension officer in proffesion
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Ukipata nafasi tembelea ofisi za balton utapata mwongoo na ikiwezekana agronomist wakuwa anakutembelea
 
Au Kama Hauzi Akupatie Tu Ulifanyie Majaribio Ya Zao Linalostawi Baada Ya Hapo Ndo Atajua Aanzie Wapi Na Aishie Wapi ... !
Kaka mi nataka kulima mazao ya kudumu, sasa akinipa kwa majaribio haitofaa
 
Mkuranga ipi?
Kama ni sehemu ambayo ina mchanga mzuri ambao unafaa kwa ujenzi basi anzisha machimbo ya mchanga utawauzia wenye malori. Kwa siku utaingiza zaidi ya mil kama utasimamia vizuri.
 
Hbari ndugu,

Kama nilivyoeleza hapo juu nina ekari 6 na ningependa kuituma kujiongezea kipato kuliko kiwa shamba pori. Naulizia zao ambalo naweza kulima na likawa na tija. Sina tatizo la mtaji.
Mkuu, habari ya wewe. Mimi pia nina shamba la ekari 10 Kimanzichana so i assume tuko kwenye same zone. Sijajua unataka kufanya kilimo cha aina gani ila nikushauri kama ninavyofanya mimi. Binafsi ninalima mihogo kwa sasa na mwezi wa kumi na moja natarajia kulima ufuta pia. Mihogo mwezi wa tisa ndio msimu mzuri kwa kupanda, ufuta mwezi wa kumi na moja. Kama una mtaji wa kutosha pia unaweza kulima Nanasi, Karanga na Matikiti maji maana hayo mazao yote yanakubali 100%. Karibu kwenye kilimo mkuu
 
mie nina heka 10 kibiti mwezi wa pili ninataka kupanda miche ya mikorosho kama zao la kudumu ambayo nitaanza kuvuna baada ya miaka 2 pia wakati mikorosha inakua nitakuwa nalima mihogo.Fanya hivyo mkuu
 
Hbari ndugu,

Kama nilivyoeleza hapo juu nina ekari 6 na ningependa kuituma kujiongezea kipato kuliko kiwa shamba pori. Naulizia zao ambalo naweza kulima na likawa na tija. Sina tatizo la mtaji.
Kibiashara tunashauri kulima mazao ya muda mfupi yakukupa kipato na kuweza kurudia mara kazaa mfano Tikiti,Nyanya,Tango,Nyanya chungu na pilipili mbuzi
 
Ka mkubwa siwez pata heka kadhaa uko..... kwa project ya ufugaji...

Kina na chanza cha maji tu... aidha kisima... dawasco au mto
 
Back
Top Bottom