Nina PhD natafuta kazi

Nina PhD natafuta kazi

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2012
Posts
3,401
Reaction score
1,618
Habari zenu ndugu zanguni,

Nimesoma B.A ya economics UD, kwa kuwa mzee wangu alikuwa ana kauwezo mdogo akanishauri nisome masters. Nilipokuwa nasoma Masters niliona tangazo la PhD scholarship ya DAAD-Germany, nikaomba kwa bahati nzuri nikapata hivyo baada ya kumaliza masters nikaenda kusoma Hamburg Ujerumani. Hivi sasa ninapoongea nina PhD ya business administration management na kwa bahati mbaya sana hamna tangazo la kazi wanalotaka mtu mwenye PhD asiye na experience hata kidogo, nimechanganyikiwa mpaka najuta kusoma.

Huu ni mwaka wa pili natafuta ajira, niliomaliza nao degree ya kwanza hivi sasa wana maisha mazuri namimi hali yangu haieleweki. Na wazazi uwezo wao kiuchumi umepungua sana hiyvo hawawezi kunipa hata mtaji nikafanye biashara, maisha haya jamani, sijui ninamfundisha nini mdogo wako anayenifata?

MKINIPA MAWAZO YA KUJENGA NTAWASHUKURU ZAIDI.
.......................................
UPDATE: Nashukuru sana kwa mawazo yenu wakuu, nimepata kazi katika moja ya taasisi za elimu ya juu kama lecturer. Mbarikiwe sana
 
nakushauri kaombe kuwa lecturer kwenye vyuo au nenda kaombe kazi kama unataka kuajiriwa ila usionyeshe hiko cheti chako cha hiyo phd onyesha mwisho cha masters vinginevyo utaendelea kukaa home sana tu.
 
Pole mkuu,
Naona jembe halimtupi mkulima. Very soon you will be blessed. Pia chukuwa ushauri wa clex hapo juu, tumia vyeti vya BA unless masters ni added advantage.
 
nakushauri kaombe kuwa lecturer kwenye vyuo au nenda kaombe kazi kama unataka kuajiriwa ila usionyeshe hiko cheti chako cha hiyo phd onyesha mwisho cha masters vinginevyo utaendelea kukaa home sana tu.

vyuo vingi ili uajiriwe ni lazima uwe na GPA ya 3.8 kwenye degree ya kwanza na mimi nilikuwa na 3.4
 
Naomba nkushauri kuna chuo cha mwenge university kipo mosh karibu na kcmc nina uhakika ukienda pale watakufikiria kaka.
 
pole sana ila usijali fwata ushauri huo mwingine kaombe kazi tumia cheti cha masters na degree ukishapata kazi nakushauri baada ya kupata mtaji wa kutosha jiari uitumie hiyo elimu yako ya phd
 
Ukishakuwa na PHD kazi yako ni kufundisha vyuo vikuu,ni wachache sana wanaopata kazi kwenye makampuni binafsi hata ya serikali....well anza kutafuta kazi ya kufundisha hapo utapata.goodluck
 
namaanisha ujiajiri usiishiwe kuajiriwa tu
 
vyuo vingi ili uajiriwe ni lazima uwe na GPA ya 3.8 kwenye degree ya kwanza na mimi nilikuwa na 3.4

Sio kweli sababun kuna watu tunawajua degree ya kwanza walikuwa na GPA za kawaida wakaenda kusoma masters na saiv wanafundisha..ni channel tu.im sure utapata kazi;ila tujifunze kwamba experience ya kazi nayo matters...Nakutia moyo utafanikiwa wala usijilaumu kabisaa,kama vipi peleka CV zako Tumaini nUniversity ya Dar(hata uombe part time utapata),KIU,Univ of Bagamoyo etc etc
 
Habari zenu ndugu zanguni,
Nimesoma B.A ya economics UD, kwa kuwa mzee wangu alikuwa ana kauwezo mdogo akanishauri nisome masters.
Nilipokuwa nasoma Masters niliona tangazo la phd scholarship ya DAAD-Germany, nikaomba kwa bahati nzuri nikapata hivyo baada ya kumaliza masters nikaenda kusoma hamburg ujerumani. hivi sasa ninapoongea nina phd ya business administration management na kwa bahati mbaya sana hamna tangazo la kazi wanalotaka mtu mwenye phd asiye na experience hata kidogo, nimechanganyikiwa mpaka najuta kusoma. huu ni mwaka wa pili natafuta ajira, niliomaliza nao degree ya kwanza hivi sasa wana maisha mazuri namimi hali yangu haieleweki.Na wazazi uwezo wao kiuchumi umepungua sana hiyvo hawawezi kunipa hata mtaji nikafanye biashara.... maisha haya jamani!!! sijui ninamfundisha nini mdogo wako anayenifata?
MKINIPA MAWAZO YA KUJENGA NTAWASHUKURU ZAIDI.
Mkuu kama umefaulu vizuri PhD yako nenda taasisi za research and academics. Yaani mavyuo yote utitiri hujapata kazi? Pia waweza ficha cheti cha degree ukaombea kazi cha masters ila hapa panaweza kugoma maana watahitaji experience na ulikuwa nje ya nchi. Ila vuta subira kazi utapata tuuu.
 
hii kitu vijana wakiambiwa huwa hawakubali. huna experience, phd hiyo labda ukafundishie na uanze chini kabisa. otherwise jaribu kuangalia research institutions ambazo wanahitaji field people. usiangalie mshahara, lazma uanzie chini. ila ukiomba kazi zingine usipeleke vyeti japo utahitaji kujieleza ulikuwa wapi hapo kati (unaweza kuongelea biashara ya familia hehehe, uongo bongo sio dhambi).

Just out of curiosity, phd yako uli-major nini?
 
Habari zenu ndugu zanguni,
Nimesoma B.A ya economics UD, kwa kuwa mzee wangu alikuwa ana kauwezo mdogo akanishauri nisome masters.
Nilipokuwa nasoma Masters niliona tangazo la phd scholarship ya DAAD-Germany, nikaomba kwa bahati nzuri nikapata hivyo baada ya kumaliza masters nikaenda kusoma hamburg ujerumani. hivi sasa ninapoongea nina phd ya business administration management na kwa bahati mbaya sana hamna tangazo la kazi wanalotaka mtu mwenye phd asiye na experience hata kidogo, nimechanganyikiwa mpaka najuta kusoma. huu ni mwaka wa pili natafuta ajira, niliomaliza nao degree ya kwanza hivi sasa wana maisha mazuri namimi hali yangu haieleweki.Na wazazi uwezo wao kiuchumi umepungua sana hiyvo hawawezi kunipa hata mtaji nikafanye biashara.... maisha haya jamani!!! sijui ninamfundisha nini mdogo wako anayenifata?
MKINIPA MAWAZO YA KUJENGA NTAWASHUKURU ZAIDI.

Vyuo vikuu vya binafsi nao hawakuhitaji? Kazi nyingine hazihitaji kuandika application, kaonane na wasomi wenzako kama Mount Meru University, Makumira University, na hata vyuo vya serikali huchukua "Part time" lecturers. Huku kwenye "industry" hatuandiki vitabu hivyo elimu yako hahitajiki sana
 
Mmmh..majanga yani una phd hata kujiajiri umeshindwa?Umenifanya nione PHD kama cheo cha kugombea uraisi tu kwamba mtu yeyote anaweza kupata.Nakushauri fungua tution centre wanafunzi wapo wengi tu utapata.
 
PHD kabisa afu huna kazi!! Yaaan dah hapana,, mmmmmh! Hatujafika huku kwa Tanzania kama hutuchori tafuta kazi zipi nyingi sana kwa grade yako.

yaan CBE,IFM, TIA kuna ma lecture wana videgree afu wakuu wa vyuo hivyo wanawatafuta watu kama wewe afu useme huna kazi, uko locked au vyeti umevipatia msimbazi!??

Loading,,,,,,,,,,,,
 
aiseee hii ni babkubwa.salamu hizi ziwafikie ma-john kisomo wote wanaodhani kupoteza miaka mingi mfululizo shule ndio mafanikio.PHD holder unatafuta kazi?!!i thought u guys were the most hunted candidates by employers.damn you "EDUCATION".
 
Back
Top Bottom