Nina mke ananitukana

Nina mke ananitukana

Habari wana JF, Mimi nina mke tumefunga ndoa na tumejaliwa kupata mtoto mmoja kwa sasa ana miezi 8. Mke wangu ni mgomvi mno, kila ukimueleza jambo anapaniki hata kama ni zuri kiasi gani.

Kuna wakati anaaga anaenda sehemu kumbe anadanganya anaenda mahali pengine. Kuna siku baba mkwe akanipigia simu baada ya kujua kadanganya hakwenda alikoaga anaenda, akaniambia niwe namweleza kila uchafu anaofanya mke wangu. Lakini naona siyo poa kumwambia kuwa mwanao ananitukana na ni muongo.

Kipindi cha nyuma aliwahi kunisimulia kuwa alitoroka kwao na kwenda Tabora huko akapata mwanaume wakakaa miaka 2 lakini wakaachana na kurudi kwao hapo ndipo nilipokutana nae na baadae kumuoa, hayo ni machache lkn kifupi si mwaminifu, mgomvi, hana ushauri juu ya maisha na haniheshimu.

Kinachooniuma ni kwamba mimi ni mkristo na ndoa zetu zikifungwa hakuna kuachana. Nifanyeje? Nahitaji ushauri mzuri na wa hekima. Natanguliza shukrani.
Aliyekuambia zikifungw hakuna kuachana ni nani?
 
Huo msalaba ni wako huna budi kuubeba tu, omba Mungu akusaidie au ikishindikana Waite wa simamizi wenu wa ndoa wa kusaidie
 
Mwanamke apigwi mahondaw wangu...

Mimi ushawahi kunichukiza sana, lakini hata siku moja sijawahi kukupiga na sitowahi...
Ndomana always nasemaga am blessed to have you Smart911

Hata nikuchukizajee hunipigiii.. Unanipa psychological punishment tu jiniaz wangu kisha unanielekeza nikitoka hapo nakua nishajifunza kitu

Asanti sana
 
Unanitegaga sana na mambo yako, kuhusu my past... But nangamua mapema na kukwepa vihunzi...
 
Ukitaka mwanamke mwenye mdomo ajidharau wewe muache atukanee atukaneeeee, usijibu, usikasirike baadae muongeleshe kawaida kama hamna kilichotokea?! Nakupa miezi 2 atajiona fala na wanawake tukidharauliwa tunajishtukia sana
 
Kama alikaa miaka 2 na mwingine wakaachana huyo ni mkorofi tengana naye kwa muda kwa afya ya pande zote mbili kwani usipoangalia mtafungana tu
 
Habari wana JF, Mimi nina mke tumefunga ndoa na tumejaliwa kupata mtoto mmoja kwa sasa ana miezi 8. Mke wangu ni mgomvi mno, kila ukimueleza jambo anapaniki hata kama ni zuri kiasi gani.

Kuna wakati anaaga anaenda sehemu kumbe anadanganya anaenda mahali pengine. Kuna siku baba mkwe akanipigia simu baada ya kujua kadanganya hakwenda alikoaga anaenda, akaniambia niwe namweleza kila uchafu anaofanya mke wangu. Lakini naona siyo poa kumwambia kuwa mwanao ananitukana na ni muongo.

Kipindi cha nyuma aliwahi kunisimulia kuwa alitoroka kwao na kwenda Tabora huko akapata mwanaume wakakaa miaka 2 lakini wakaachana na kurudi kwao hapo ndipo nilipokutana nae na baadae kumuoa, hayo ni machache lkn kifupi si mwaminifu, mgomvi, hana ushauri juu ya maisha na haniheshimu.

Kinachooniuma ni kwamba mimi ni mkristo na ndoa zetu zikifungwa hakuna kuachana. Nifanyeje? Nahitaji ushauri mzuri na wa hekima. Natanguliza shukrani.
Babaaaa Kiyumbi Yogaaaaaa....huo ni msala wako komaa nao babaaaaa km vp nipe namba yake nije nimkanye kanyuuuuu
 
Back
Top Bottom