1academ
JF-Expert Member
- Oct 15, 2016
- 2,673
- 4,318
Toka kw pm yangu jamani dah..
Mwaka jana dada yangu alikuja kumtambulisha mwanaume wake, akatoa mahari na mipango ilikuwa ni kufunga ndoa mwaka jana hiyo hiyo mwezi 6. Mimi kipindi hicho nilikuwa niko kwenye mahusiano na mpenzi wangu, baada ya kumwambia kuhusu harusi ya dada yangu nilidokeza kama na mimi nataka kuolewa, nilimuambia vipi kuhusu harusi ya dada ikiisha si ndiyo inafuata yetu.
Cha ajabu alinijibu kwa dharau, mimi sioi leo wala kesho na unatakiwa kujua hata kama nikitaka kuoa basi sijui nitamuoa nani, wewe kama umepata mtu wa kukuoa olewa tu usinisubiri.
Maneno yake yaliniuma sana, nilijikuta nakuwa na hasira, niliumia kwa sababu mara nyingi dada yangu ndiyo anapata vitu vizuri, yeye alisoma akapata kazi huko UN wakati mimi ni mwalimu tu tena wa diploma nasijaairiwa nahangaika mtaani. Akawajengea wazazi wetu nyumba wanamsifia kila siku, mimi nahangaika hapa nyumbani nafanya kila kazi lakini thamani yangu haionekani. Kweli niliumia na nikahisi dada yangu ndiye ananiharibia maisha, mimi ni mzuri kuliko yeye na watu wananambia lakini sina bahati!
Baada ya mchumba wake kujitambulisha alichukua namba yangu hivyo alikuwa anaona status zangu, nilichofanya ni kwa kupost status za mtego na kumblock kila mtu anaona yeye. Akawa anacomment kama utani basi tukajikuta tunakuwa karibu, kuna siku aliniomba tutoke nikatoka naye, nikanywa na kujifanya nimelewa nikafanya naye mapenzi. Ilianza kama utani lakini baadaye niliona kama vile ananijali mimi kuliko dada hivyo nikajiona mzuri, nikaanzisha mahusiano rasmi huku nikihangaika kuona niachane na dada yangu.
Shemu alianza kuniambia mambo mabaya kuhusu dada yangu, akawa ananiambia jinsi ambavyo anamchukia kutokana na kazi yake huko na mambo kibao. Nilikuwa najisikia vizuri kuwa hampendi dada anamvumilia tu hivyo nilijiweka kwenye nafasi ya mimi kuwa karibu zaidi na kweli mahusiano yake na dada yalitibuka sana, nikamuona dada ana mawazo, kila wakati kulalamika, alikuwa haniambii mambo yake sana lakini nilijua kuwa anaumia hivyo niliendelea kufurahia!
Kumkomoa zaidi dada niliamua kubeba ujauzito, malengo yangu ni ili amuache kabisa nikiamini atakuja kunioa mimi. Mwezi wa kwanza mwaka huu nilipambana mpaka nikabeba mimba ya shemeji, lakini nilipokuja kumwambia mwanaume nilimuona kabadilika, akawa mkali na kuniambia nitoe. Nilipanga kutoa kweli kwani baada ya muda niliona kama ni ujinga lakini katika kuongea naye alitamka maneno ambayo yalinifanya kupaniki, akasema sitaki kumuumiza dada yako ni mtu mwema sana kwangu. Akaanza kumsifia na kumpa sifa kibao, kweli nilikasirika kwani niliona anampenda dada kuliko mimi.
Nilimdanganya kuwa mimba nimeshaitoa hivyo tunaendelea na mapenzi yetu lakini kumbe sikutoa na sasa hivi nina ujauzito ni kama miezi 5. Mwanaume alivyojua kuwa sijatoa mimba alikasirika, akabadilika na kuninunia. Nilishangaa baada ya kusema sasa tuongee kuhusu mapenzi yetu, akaendelea na mipangoya kumuoa dada. Mimi nilimuambia usimuoe kama ukimuoa nitasema kila kitu lakini yeye hakujali, mipango inaendelea ndoa kufungwa mwezi 6 na kila kitu kimekamilika.
Nyumbani wanajua nina mimba lakini hawajui ni ya nani? Kweli siko tayari kuwa single mother, sitaki aolewe dada yangu. Natamani kuongea lakini najiuliza akija nikiongea atajirudi na kunipenda mimi? Nimechoka kweli, dada yangu kupata kila kitu kizuri, ananiajali kweli, ananisaidia nikikwama ananipa pesa hata kodi ya nyumba ndiye analipia lakini kwanini yeye apate kila kitu kizuri, anataka nimuambie ili hata kama mwanaume hatanioa tuumie wote nimechoka kuwa mwema kwa watu nimechoka na mimi nataka kuwa na maisha yangu, mwanangu alelewe na baba yake. Nisaidie nifanye nini?