Nina miaka 7 sijaumwa, wala kumeza Dawa

Nina miaka 7 sijaumwa, wala kumeza Dawa

mkuu wewe unaumwa tena sana,kutokutambua tu uwepo wa Mungu ni maradhi tosha.
halafu hayo mengine ungesema tu hujazidiwa yamejaa tele mwilini humo.

Sio kwel,Kwamba kutokutabua uwepo wa Mungu ni ugonjwa.Je nikisema kutambua uwepo wake pia ni ugijwa ntakuwa nimekosea?? unathibitisha vipi kwamba kutokutambua uwepo wake ni ugonjwa??
 
Mimi sijaugua muda mrefu hata sikumbuki ni lini mwisho wake ila kwa yote hayo ninataka nikuambie kuwa "Ninamshukuru Mungu kwa afya njema, kunipitisha mbali na magonjwa ya aina yoyote ile, ninazidi kumwomba afya njema na kifo chema"
 
wako wengi tu wa aina yako ila hawataki kusema sema kwani wenaona kama ni kuwadhihaki wanaomwa umwa.mshukuru mungu.
 
Usiku kama huu huwa nautumia kutafakati mambo mengi ambayo yanahusu maisha yangu kwa ujumla.,Kuna jambo ambalo binafsi naona kama ni vigumu lakini ndo ukweli wenyewe..,Tangu mwaka 2007/6,nilienda Hospital kwa mara ya mwisho nilipokuwa nasumbuliwa na tumbo,sijawahi kuugua hadi leo hii naandika uzi huu.,Kwa hesabu ya haraka ni kama miaka SABA,sasa imepita.Mimi c mtu wa kufanya mazoezi mara kwa mara ila ni mpenzi wa kusoma vitabu hasa vya history,Falsafa na Sayansi.Japo nikipata muda huwa nafanya mazoezi japo kukimbia.

LEngo la kuandika uzi huu ni kutaka kujua kama kuna wengine pia ambao hali kma hii inawakuta!,Maana kila ninayemwambia jambo hili anashtuka na kusema kwamba sio kweli hata kidogo.,

Em nambie na wewe unachukuliaje hali hii,

Tafadhali usihusishe hili jambo na MUNGU(kama yupo), kwa maana mimi siamini katika chochote!,karibuni.....

Mkuu Free ideas hiyo ni kawawaida tu!
Mwenyewe sinaga mpango wa kuumwa umwa!

Nilijiuliza sana na kuuliza raia wengine but sikupata jibu hadi nilipoamua kwenda hospitali na kupewa majibu ya kitaaluma kwamba hiyo ni kawaida!

Nakumbuka niliwauliza "Nimeskia usipoumwa umwa siku ukiumwa mara unakofa coz maradhi yaliyojificha yote hufichuka kwa pamoja, Jee ni kweli hilo?" nikajibiwa sio kweli na wakanipa maelezo fulani fulani!

Baada ya hapo nikaamua kupima damu (mzunguko, ujazo na kinga) nikaambiwa vyote vipo normal! sikutaka kupima Ukimwi!
 
Ni Jambo jema na nadra. Jishukuru kwa kujiumba hivyo na kujipa askari wenye nguvu katika mwili wako kupambana na maradhi. Umejilinda vyema kwa miaka 7 hiyo. Nguvu ya Kisayansi iwe juu yako milele.

Nimezingatia masharti uliyoyahitaji.
 
Hata mimi, naweza kadirilia miaka 10 na ushee, na kama ikitokea kujiskia hali ya homa sinywi dawa, nakandamiza mzinga wa konyagi tu. walevi wengi ni nadra sana kuumwa, teh teh teh
 
Ni Jambo jema na nadra. Jishukuru kwa kujiumba hivyo na kujipa askari wenye nguvu katika mwili wako kupambana na maradhi. Umejilinda vyema kwa miaka 7 hiyo. Nguvu ya Kisayansi iwe juu yako milele.

Nimezingatia masharti uliyoyahitaji.

mkuu za siku hahah,nakumbuka tumewahi kukutana katika uzi flani humu paliwaka moto.heko kijana unajitahidi
 
Mkuu mimi ni kama wewe,nina miaka 12 sijaumwa zaidi ya mafua.Mkuu nina wiki mbili nipo kitandani.
 
Tafadhali usihusishe hili jambo na MUNGU(kama yupo), kwa maana mimi siamini katika chochote!,karibuni.....

Hapa umeharibu. Mungu anakulinda na kukupa afya nzuri kama mimi endelea kumtukuza la sivyo usiku wa leo unaweza kuanza kusikia maumivu polepole, homa na hatimaye ugonjwa kamili. Ukirudi kuniuliza nitakuambia kamuombe Mungu akurudishie tena afya yako
 
Back
Top Bottom