Nina mashaka na uwezo wa CHADEMA kuongoza SERIKALI 2015

Mbona hilo liko wazi kinachotakiwa sasa CDM iongeze mbinu za kukabiriana na serikali si CCM tena, mbinu za jukwaani wameshafuzu sasa watafute mbinu za kukabiliana na vitisho vya serikali ikiwemo polisi na mahakama maana tunajua hulka ya vyama tawala vya kiafrika vikizidiwa huwa vinajificha nyuma ya dola.
 
Hivoo sikujua, kwa hiyo CDM wako juu kimkakati mpaka kuiba kura kuliko ccm?

isitokee uchaguzi fulani hapa CDM wakashindwa, halafu mkasema CCM wameiba kura , wakati KIMKAKATI CDM wako juu ya CCM. Think!
Waberoya za siku,
hapa umechemsha lengo lako lilikuwa kuonyesha Chadema wamekuwa wezi wa kura hukujua unakiumbua CCM.
 
Watanzania hawahitaji propaganda za kipuuzi, sijui udini mara ukabila mara ukanda!! wanahitaji majibu yenye mwelekeo wa kutatua matatizo yao. Watu wanaishi roho juu juu utadhani hawako tena nchini mwao sababu ya kuwa na viongozi wapenda pesa, wabinafsi na wenye kuchukia wakiambiwa ukweli.

Sijui wanawaza nini wanapokutana na watu choka mbaya sababu ya viongozi wenye dhamana kushindwa kutimiza wajibu wao? We don't need vagueness from you leaders, we just need you to fullfill your responsibilities bila kudhihaki watu au vyama. Hata kama wewe ni mpenzi wa chama fulani, kama uko serikalini, toa majibu yenye kujenga siyo kubomoa. Watu wanaona, wanasikia na wanaelewa sana ukikaa nao ukawaeleza/mkajadiliana kwa manufaa ya sehemu husika.
 
Wabunge 23 watainyima vipi serikali usingizi. Nyie endeleeni ya fujo zenu, wananchi wenye akili zao wamesha wasoma. Mtabaki na hilo genge lenu la wavuta bangi wasio jua hata kupiga kura.

Mkuu ni wananchi gani wenye akili zao unaowataja? NI wale amao wanaibiwa na kukaa kimya? au wale wanaotekeleza mahubiri ya kupigwa kulia geuza kushoto? wewe ni ni matanzania kweli unayejua serikali yetu inafanya nini? Unajua kuwa watanzania by nature ni watulivu lakini si wajinga wa kudumu?
 
Hivoo sikujua, kwa hiyo CDM wako juu kimkakati mpaka kuiba kura kuliko ccm?

isitokee uchaguzi fulani hapa CDM wakashindwa, halafu mkasema CCM wameiba kura , wakati KIMKAKATI CDM wako juu ya CCM. Think!

Inaelekea unajua kusoma ila huelewi unachokisoma,jitahidi sana uelimike la sivyo dunia itakupungia mkono.
 
Cdm ni kama nyimbo za Bongo fleva,, zinavuma na kupendwa hata kama hazina ujumbe wowote lakini hudumu kwa muda mfupi2,,, Staili wanayotumia kuuteka umma na kupanda chuki kwa serikari iliyopo itakuja leta hasara kwa wa Tanzania,, Simekuwa cyo saisa tena bali ni vurugu tuu,, chekeleeni tuu, mtakuja juta, Usione mh,Rais ametulia kama haoni lakini cku atakapo tamka jambo kuhusu hili jambo msije mka mlaumu.

We nae ni mtu au..................?
 
Baada ya serikali ya CCM kupoteza imani kwa wananchi Chadema kimeonekana kuwa kimbilio la mwisho kwa wanyonge na wasio wanyonge. Kwa sababu hiyo lazima CDM kitapata wanachama wapya wengi, lakini pamoja na hayo sioni kama CDM kimejiandaa au kinajiandaa kwa ujio huo.

Najua CCM kwa vile wana serikali ina vitengo vingi na uwezo mkubwa hata wa kuwaahidi wanachama wake u-DC nk kitu ambacho CDM hawana. Lakini tunajua CDM ina taasisi yenye muundo wa serikali (serikali ya majimbo), ina vitengo vyake na idara zake kuanzia wilayani, majimboni, mikoani, hadi taifa, kwa hiyo kwa vyovyote vile haiwezi kushidwa kuwa accomodate wageni hasa wanaokuja tayari na CV zao mkononi kama kina Millya.

Lakini cha kujiuliza, CDM kama taasisi, viongozi wa wilaya wako wapi, viongozi wa mikoa ni akina nani, je, sera ya majimbo inaongozwa kwa organs na structure zipi mbona hazijulikani? Chama kama taasisi hakiwezi kukamilika kama hivi vyombo viko dormant vikisubiri ujio wa mtu mmoja (Slaa) kufanya mkutano wa hadhara na kuondoka. Hivi leo nikienda Masasi kwa mfano nimuulize m/kiti wa tawi anaweza kumjua kiongozi wake wa jimbo ni nani? Kama hamjui je CDM wanatekelezaje kwa vitendo sera yao ya serikali za majimbo, au iko vitabuni tu?

What I'm trying to advocate here is that, CDM kipanue wigo wa utawala wake isijibane sana makao makuu, i-practice kwa vitendo sera yake ya majimbo wananchi waanze kuizoea. Hawa wanachama wapya wanaokuja waungane na viongozi wenyeji (of course baada ya kuwa-screened) wagawane hayo majimbo, wajitanabahishe huko kiasi kwamba tukisema jimbo la kanda ya Ziwa kwa mfano tujue nani atakuwa answerable kusimamia uhai wa chama kwa kuanzisha matawi, kuingiza wanachama, kuanzisha miradi n.k. Nafikiri huo ndio mfano mzuri kwa chama kinachojiandaa kushika dola.

Chama hakiongozwi kwa kutegemea head office (ikulu), head office inachotakiwa ni kutoa directives, highest decision-making na support lakini day-to-day activities zinafanywa na na organs zilizo chini yake, lakini kwa CDM the opposite is true, chama ni Mbowe, Slaa, Zitto basi, wanaonekana kana kwamba wao ndio wanaopokea directives na wao ndio wanafanya day-to-day activities.

Chama kinaonekana kama kimepwaya kipo makao makuu na kwa wananchi lakini hapa katikati hakuna kiungo kabisa, wanachama wanaelea elea tu hakuna wa kuwa handle kiasi kwamba siku yeyote wanaweza ku-deflect. Kama bado unapanda majukwaani kuomba watu wajiunge wakati hujajiandaa kuwa accomodate ni uzembe na upungufu wa strategies. Inauma sana chama kama kinapata nguvukazi na kushindwa kuitumia.

CDM wasiishie tu kumfanyia tafrija kubwa Millya na wengine watakaojiunga, wajiandande ni vipi wanatumia hizo nguvu mpya zinazoingia kuimarisha chama na kuandaa makada wake tayari kwa kuongoza serikali. Lakini kama chama kitaendelea kutegemea head office tutarudi kule kule kwa Pinda kutokuwa na uwezo wa maamuzi hadi amsubiri rais arudi toka ziarani.

Luteni.
 
Luteni umejiandaa au utakimbia maana humu umeingia kwenye nyumba yao!! Una hoja lakini watu watakuja kuhoji "elimu yako" "umagamba" "unalipwa shilingi ngapi" utaambiwa unatumia "masaburi" kufikiri. Mimi nimekuelewa!!
 
Post imetulia mkuu!
ila ungeongeza one line ili ikamilike kabisa "Ni ndoto CDM kuunda serikali tanganyika" labda wanajeshi wachukue nchi kama guinea bissau na walazimishe chama cha upinzani kiunde serikali.
Good try
 
Unafikiri magamba wataleta ya Pemba kuioa CDM Kama cuf sahau gamba wewe
 
Luteni umejiandaa au utakimbia maana humu umeingia kwenye nyumba yao!! Una hoja lakini watu watakuja kuhoji "elimu yako" "umagamba" "unalipwa shilingi ngapi" utaambiwa unatumia "masaburi" kufikiri. Mimi nimekuelewa!!
Mawazo yake ni mazuri sana sana na tena sana.
@ Kigarama..... pro mabadiliko (au kama ninyi mnavyojichanganya na kuwaita wana Chadema) huwa hawapingi mawazo ya busara hata siku moja. Watu wamechoka na longolongo zisizo na maana kama za kina Wareboya
 
Wazo zuri, nimelipenda ila umakini unahitajika sana kama vitu havikuwa monitored kwa ukaribu.
Kumbuka CCM inaweza kutumia huo mwanya kuharibu pia.
Tuwape muda kama maeneo yako bado mwamko si mkubwa kanda ya ziwa hali ni tofauti sana tunaona huu utaratibu si mbaya mpaka hapo tutakapokuwa na TOTAL CONTROL:focus:
 
Baada ya serikali ya CCM kupoteza imani kwa wananchi Chadema kimeonekana kuwa kimbilio la mwisho kwa wanyonge na wasio wanyonge. Kwa sababu hiyo lazima CDM kitapata wanachama wapya wengi, lakini pamoja na hayo sioni kama CDM kimejiandaa au kinajiandaa kwa ujio huo.

Najua CCM kwa vile wana serikali ina vitengo vingi na uwezo mkubwa hata wa kuwaahidi wanachama wake u-DC nk kitu ambacho CDM hawana. Lakini tunajua CDM ina taasisi yenye muundo wa serikali (serikali ya majimbo), ina vitengo vyake na idara zake kuanzia wilayani, majimboni, mikoani, hadi taifa, kwa hiyo kwa vyovyote vile haiwezi kushidwa kuwa accomodate wageni hasa wanaokuja tayari na CV zao mkononi kama kina Millya.

Lakini cha kujiuliza, CDM kama taasisi, viongozi wa wilaya wako wapi, viongozi wa mikoa ni akina nani, je, sera ya majimbo inaongozwa kwa organs na structure zipi mbona hazijulikani? Chama kama taasisi hakiwezi kukamilika kama hivi vyombo viko dormant vikisubiri ujio wa mtu mmoja (Slaa) kufanya mkutano wa hadhara na kuondoka. Hivi leo nikienda Masasi kwa mfano nimuulize m/kiti wa tawi anaweza kumjua kiongozi wake wa jimbo ni nani? Kama hamjui je CDM wanatekelezaje kwa vitendo sera yao ya serikali za majimbo, au iko vitabuni tu?

What I'm trying to advocate here is that, CDM kipanue wigo wa utawala wake isijibane sana makao makuu, i-practice kwa vitendo sera yake ya majimbo wananchi waanze kuizoea. Hawa wanachama wapya wanaokuja waungane na viongozi wenyeji (of course baada ya kuwa-screened) wagawane hayo majimbo, wajitanabahishe huko kiasi kwamba tukisema jimbo la kanda ya Ziwa kwa mfano tujue nani atakuwa answerable kusimamia uhai wa chama kwa kuanzisha matawi, kuingiza wanachama, kuanzisha miradi n.k. Nafikiri huo ndio mfano mzuri kwa chama kinachojiandaa kushika dola.

Chama hakiongozwi kwa kutegemea head office (ikulu), head office inachotakiwa ni kutoa directives, highest decision-making na support lakini day-to-day activities zinafanywa na na organs zilizo chini yake, lakini kwa CDM the opposite is true, chama ni Mbowe, Slaa, Zitto basi, wanaonekana kana kwamba wao ndio wanaopokea directives na wao ndio wanafanya day-to-day activities.

Chama kinaonekana kama kimepwaya kipo makao makuu na kwa wananchi lakini hapa katikati hakuna kiungo kabisa, wanachama wanaelea elea tu hakuna wa kuwa handle kiasi kwamba siku yeyote wanaweza ku-deflect. Kama bado unapanda majukwaani kuomba watu wajiunge wakati hujajiandaa kuwa accomodate ni uzembe na upungufu wa strategies. Inauma sana chama kama kinapata nguvukazi na kushindwa kuitumia.

CDM wasiishie tu kumfanyia tafrija kubwa Millya na wengine watakaojiunga, wajiandande ni vipi wanatumia hizo nguvu mpya zinazoingia kuimarisha chama na kuandaa makada wake tayari kwa kuongoza serikali. Lakini kama chama kitaendelea kutegemea head office tutarudi kule kule kwa Pinda kutokuwa na uwezo wa maamuzi hadi amsubiri rais arudi toka ziarani.

Luteni.

Hivi kila mtu inabd aanzishe thread hapa ndo aonekane yupo jf? Yaani unashabikia uongozi wa kupeana UDC na URC? Unajua garama yake na unajua kuwa wananchi hawataki. Kama cdm nacho kitafuata mfumo CCM huu ni heri tubaki na shetani tumjuae. Kwa taarifa yako taasisi za mfumo wa Serikali kwa maana ya watendaji ni ile ile hivo usihadae watu kuwa cdm watakuja na polisi wao, jeshi lao, usalama wao na beuracrats wao. Cdm itaweka mfumo mzuri wa kusimamia taasisi ili ziwajibike kwa wananchi sio kwa madc na ma rc ambao ni makada wa CCM. Cdm wataptumia zaidi wakurugenzi ktk halmshauri ambao watafanyishwa interview na si kupewa kimahaba. Usidanganye je TANU ilikuwa imepata wapi uzoefu na CCM ya 1977 nayo ilipata wapi uzoefu mbona tanganyika ya toka ntyma ya hapo? Jenga hoja kisayansi lkn watz hawadanganyiki na ***** huu
 
Kwani nani anaejidai kwamba amejiandaa kuunda serikali? Hawa ambao kwa miaka 50 wanaishi kwa madeni na bajeti tegemezi. Ambao wameona kujilimbikizia mali bila kujali mslahi ya umma. Au hukusikia wabunge wa CCM leo, waliposema kwamba wana wasiwasi kama kuna serikali. Mawazo mgando ndio yanayokufanya uione CDM hivyo. Hawa jamaa waone hivyo hivyo, utashangaa. Hawa sio mavuvuzela ni watu action. Nimewaona katika vikao vyao, hawana mchezo kabisa.
 
CDM ilishajipanga tangu 2010, nasasa ndiyo inamezidi kujiimarisha. 2010 haikuwa utani kuongoza nchi, wapo wazalendo wengi wenye moyo wa kulitumikia Taifa. Mfumo wa sasa ndiyo umewafumba macho na kufikiri hawa walioshindwa ndiyo pekee wenye uwezo wa kuongoza nchi. Napenda nikutoe wasiwasi, subiri 2015 utaona team nzuri itakayorudisha matumaini yaliyopotea. Wazo lako hili lilishafanyiwa kazi kwa umakini tangu 2000-2005. Natumaini nawe utakuwa ni mzalendo mmojawapo utakayeshiriki kikamilifu katika kurudisha hadhi ya Taifa inayostahili. Kwahilo tumejiandaa kitambo.....
 
Hivi kila mtu inabd aanzishe thread hapa ndo aonekane yupo jf? Yaani unashabikia uongozi wa kupeana UDC na URC? Unajua garama yake na unajua kuwa wananchi hawataki. Kama cdm nacho kitafuata mfumo CCM huu ni heri tubaki na shetani tumjuae. Kwa taarifa yako taasisi za mfumo wa Serikali kwa maana ya watendaji ni ile ile hivo usihadae watu kuwa cdm watakuja na polisi wao, jeshi lao, usalama wao na beuracrats wao. Cdm itaweka mfumo mzuri wa kusimamia taasisi ili ziwajibike kwa wananchi sio kwa madc na ma rc ambao ni makada wa CCM. Cdm wataptumia zaidi wakurugenzi ktk halmshauri ambao watafanyishwa interview na si kupewa kimahaba. Usidanganye je TANU ilikuwa imepata wapi uzoefu na CCM ya 1977 nayo ilipata wapi uzoefu mbona tanganyika ya toka ntyma ya hapo? Jenga hoja kisayansi lkn watz hawadanganyiki na ***** huu
Mfumo gani watakaouweka.
 
Mkuu Luteni, mara baada ya uchaguzi 2010 nilipandisha uzi wa "CCM Imechokwa!", Chadema Haijajipanga!" kilichofuatia nakikumbuka vyema, hivyo naifuatilia kwa makini hii thread hii ili nifanye marejeo ya mimi niliposema Chadema "haijajipanga" na wewe unaposema Chadema "haijajiandaa" utapokelewa vipi?.
 
Jamaa kanena kwa mtazamo wake...ila ni vyema atambue pia yakua wafuasi wa CDM ni wengi sana japo hawajaonekana ukiwemo wewe... tambua mifumo ya kiserikali inaongozwa kulingana na sera ya chama kinachounda SERIKALI. mifumo ya waatalamu inawezatumika zaidi kuliko political ambitions...lazima tukubali pia si kweli kwamba CDM ikichukua hatamu basi matatizo ya watanzania yatatatulika kwa haraka kama tudhinivyo... la hasha... itawahitaji muda kuunda mfumo mpya, kupambana na mfumo upinzani kwa waakati huo CCM na pia kuwafanya na kuwahamasisha watanzania wajitume zaidi ktk kazi na kufuata sheria na wakati huo huo kuongeza fursa na upatikanaji wa huduma za kijamii kwa urahisi zaidi...Vijana lazima pia waandaliwe ktka kuwajibika na kujituma ndani ya sera kazi,sheria haki na wajibu... hapo tutafika.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom