View attachment 592348
Nimeanza kupata shaka na utu wa Rais Magufuli. Sijui yanakuwa matamshi ya bahati mbaya au makusudi.
Rais anazifanya fikra kwamba kina Manji wanandamwa kwa sababu wana raga,zionekane sahihi. Au tuseme kina Mbowe wanahujumiwa miradi yao kwa sababu wana raha? Inaudhi sana. Tazama watu wamefikia kumtukana Rais mitandaoni kwa sababu ya kauli kama hizi
Rais wa nchi anatakiwa afanye kila juhudi ili kila mwananchi aishi kwa raha ya ajabu anavyotaka.
Rais hatakiwi kuwaandamawale waliofanikiwa kuishi kwa raha ya ajabu.
Kuna video moja ya nyumbani kwa mtoto wa Bakhresa inasambazwa. Mzee Bakhressa alipata kufanya kazi sana na Mzee wangu,katikabiashara zao. Kuna siku Mzee wangu alikuwa ananihadithia jinsi Bakhressa alivyotakakufukuzwa benkiUswizi kwa kufikiriwa ni mtu asiyetakiwa kuwa pale katikabenki (kavaa kanzu zake simple anaonekana Muafrikamchafu tu), baada ya kujieleza na kufika kwa meneja na meneja kumtanbuakama mteja wao mwenye mamilioni ya dola hapo, ilibidi meneja aomuombe radhi sana Bakhresa.
Nilivyoona video zile nikasema kuna dhana kwamba pesa zinazovunwa na wazazi humble hutapanywa na watoto ambao hawana hiyohumility,na si ajabu mtu kama Mzee Bakhresa hakupendezewa na kujionyesha kule.Na nikasema, hii humility ya Mzee Bakhressa si tabia nzuri yake binafsi na inayotokana na Uislamu wake safi tu, ni business acumen ukiwa nchi kamaTanzania.
Ukijionyesha tu una ma Rolls Royce kesho serikali inakuona chanzo cha mapato na inakukaba kodi hata ambazo hazipo itakutungia tu.
Ndicho kinachotokea sasa.
Badala ya Rais na serikaliku support wafanyabiashara ili wakuze biashara zao,wakuze ajira na serikaliipate kodi zaidi,serikaliinataka kuandama wafanyabiashara iliiue biashara na kesho ikose kodi kabisa.
Sasa uchumi ukianguka tutashangaa vipi hapo?