Wananchi wa misri wamechoka na utawala wa mubarak lakini hawana mbadala, kuna chama kinaitwa muslim brotherhood hiki chama hakikubaliki sana misri kutokana na itikadi kali ya kiislamu, wananchi wa misri wanahitaji chama chenye msimamo wa kati. Ni heri wangemuacha mubarak amalize kipindi chake ili wapate muda wa kutafakari. Nina wasiwasi nchi ya misri itaanguka kiuchumi na hali itazidi kuwa mbaya kwa sababu hakuna utawala wanaoutegemea. Kwa watanzania ingekuwa sio shida sana kwa sababu kuna chadema ambacho watu wanaimani nacho na kina viongozi wengi wasomi na wanaharakati.