Nina mashaka na maamuzi ya wa Misri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nina mashaka na maamuzi ya wa Misri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nakei, Feb 12, 2011.

 1. N

  Nakei Member

  #1
  Feb 12, 2011
  Joined: Nov 10, 2010
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wananchi wa misri wamechoka na utawala wa mubarak lakini hawana mbadala, kuna chama kinaitwa muslim brotherhood hiki chama hakikubaliki sana misri kutokana na itikadi kali ya kiislamu, wananchi wa misri wanahitaji chama chenye msimamo wa kati. Ni heri wangemuacha mubarak amalize kipindi chake ili wapate muda wa kutafakari. Nina wasiwasi nchi ya misri itaanguka kiuchumi na hali itazidi kuwa mbaya kwa sababu hakuna utawala wanaoutegemea. Kwa watanzania ingekuwa sio shida sana kwa sababu kuna chadema ambacho watu wanaimani nacho na kina viongozi wengi wasomi na wanaharakati.
   
 2. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #2
  Feb 12, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ww acha kuleta habari za uzushi hapa JF. Muslim brother hood ina wafuasi wapatao 60% ya wa egypt wote, na wao ndio tegemeo lao chama hicho kuchukua madaraka, kwani haki na usawa utashamiri sana chini ya chama hicho
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Feb 12, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280

  Mi Africa in a mawazo ya kipumbavu sana
   
 4. J

  JAY2da4 JF-Expert Member

  #4
  Feb 12, 2011
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  ya wamisri waachie wamisri,tuzungumze yetu bana
   
 5. L

  Lapton2005 Member

  #5
  Feb 12, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acha ujinga, tuzungumzie tz.
   
 6. N

  Nancy Tweed Senior Member

  #6
  Feb 12, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 123
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Alaa kumbe mlipokuwa mnashabikia mambo ya misri mlikuwa mtategemea christian brotherhood ichukue nchi? Kaanzisheni chama cha kikiristu kama chadema kule misri labda mambo yetu yatakuwa mazuri
   
 7. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #7
  Feb 12, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Under the circumstances they were in, hawakuwa na alternative nyingine!Bila mapinduzi ya uma, most of them would perish.Tanzania is in the same situation.We are slaves in our own country,watu in the millions wanakufa kwasababu ya ushenzi mwingi unaendelea nchini humu.We have to rise up and say no to this nonsense.
   
 8. K

  Kwiifoenda Member

  #8
  Feb 12, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wamisri wanajua wanachokifanya, hawajakosea hata kidogo, lile ni taifa la kiarabu ambalo watu wake wanaona mbali sana! Na misri dini si jambo la msingi wao wana evolve into liberal politics, hata muslim brotherhood siyo extremists, wanaamini katika liberal islamism! Na wamesema wanataka democrasia, utawala wa sheria, haki za binadamu, kuondoa rushwa, kuwepo ajira, nk! misri walichukia uongo wa mubarak!
   
 9. k

  kayumba JF-Expert Member

  #9
  Feb 12, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35

  Umejuaje kuwa hawana mbadala wa uongozi wakati Mubarak kaondoka jana tu!

  Muslem Brotherhood unajua kwanini haikuwa na nguvu mbele ya macho ya kimataifa wakati wa utawala wa Mubarak au unasema tu?

  Ni mapema mno kujua hali ya Misri itakuwaje uko mbele tuendako hivyo ni bora kusubiri na kuona. Kumbuka wengi walipinga kwamba Mubarak hawezi kuondoka, je si ameondoka!

  Chadema inaaminiwa na watanzania wangapi?

  Wanachadema kumbukeni: Msipokuwa makini tofauti yenu na ccm haitakuwepo, inonekana na nyie mnaanza kulewa sifa na kujisahau, badala ya kuendelea kutafuta wafuasi mnajiona nchi nzima ishawakubali; Yale yale ya ccm.........!TAFAKARI
   
 10. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #10
  Feb 12, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Misri wamejitayarisha. Wamesubiri miaka 30 na sasa wako tayari. Ama kuhusu nani wa kuongoza, mbona wapo wengi tu. Kwa sasa wanaotajwa ni Amir Mussa, Bardei, Chama cha Vijana cha 6th April*, kuna mpango wa kuunda chama kipya 25thJ Movement na hata Muslim Brotherhood. Hawa si wabaya kama ambavyo MUbarak alikuwa anawapakaz kwa maslahi yake binafsi.
  Ninachokuwa ni kimoja tu, atakayekaa yeyote itabidi achunge sana, vijana wapo!
  NB* Hiki chama kilianzishwa 2008 kupitia Facebook na kina nguvu. Dhamiri yake ya mwanzo ilikuwa kutetea maslahi ya wafanyakazi wa viwandani lakini kimekuwa cha kitaifa.
   
 11. M

  MMASSY JF-Expert Member

  #11
  Feb 12, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 225
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  NGAJA- Hakuna haja ya kuongea sana tuhamasishane watanzania kupingana na ufedhuli unaofanywa na viongozi hususani wa kutoka ccm kwa kuwaadhibu na nguvu ya umma kuanzia kwenye uchaguzi,bungeni hadi kwenye maamuzi yasiyo na maslahi kwa wananchi
   
 12. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #12
  Feb 12, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Dowans imetushinda unataka kuwaamulia wa misri mambo yao na wenye akili kuliko sisi. Kwani mmisri mmoja sawasawa na watz 5000
   
 13. M

  MMASSY JF-Expert Member

  #13
  Feb 12, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 225
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  We huna akili kweli bado una mawazo mgando,watu wanafocus kwenye maendeleo wewe unaingiza udini kiongoz yeyote lazima awe na dini ila co kigezo cha kupasua nchi kwenye misingi ya kidini
   
 14. M

  MMASSY JF-Expert Member

  #14
  Feb 12, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 225
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Chadema ni chama chenye lengo la kuwakomboa wananchi,kuwapa mwanga na dira mpya ya maisha,kung'oa mizizi ya ufisadi nchini kupunguza utofauti wa maisha kati ya mtu mmoja na mwingine.Hivyo ndugu mwananchi funguka kifikra na kimtazamo.Itazame Chadema kama mkombozi wa mtanzania mnyonge
   
 15. kinja

  kinja Senior Member

  #15
  Feb 12, 2011
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  good, hilo ndio suluhisho. Wamisri zaidi ya m8o wamechoka. Na sasa algeria
   
 16. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #16
  Feb 12, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Mbaraka ni shujaa na wamisri watakuwa hawamtendei haki kumwita kwa majina mabaya. Nina uhakika Misri itatawalika na sio kama Tunisia ambayo kwa sasa haitawaliki kwa jinsi ilivyowachwa. Misri kwa mtazamo wa watu wenye kuona kwa jicho la tatu Mubarak ameweza kujipanga pamoja na majeshi ya Misri ambalo ni jishe linalosifika kuwa ni jeshi lenye nguvu na utii barani Afrika na kwa baadhi ya nchi za kiarabu. Mubarak ni Senior Officer wa jeshi na makamu wake kadhalika alipata kuwa Mkurugenzi mkuu wa intelligence service na tangu awali yeyemwenyewe aliliagiza jeshi na askari wake wasipige watu wala kutumia nguvu kubwa kuzuia maandamano maana ni haki yao ila tu wasivunje sheria na atakaevunja sheria afunguliwe mashitaka na pia tuliona wakati wafuasi wa Mubarak walipokuwa wakirusha mabomu ya petrol jinsi walivyodhibitiwa kwa kukamatwa na Polisi. Mubarak amejipanga na amehakikisha nchi anaiacha ikiwa na uwezo wa kutawalika
  kwa Military Council naye yupo palepale nchini kama alivyosema atafia misri. Ikitokea hapa kwetu itakuwa kama tunisia ambapo vyama vya sias vinapigania kutawala nchi.!!

  Jamaa mmoja alipata kumnukuu El Baradei siku nilipokutana naye na kutoa mhadhara UDSM alisema Mubarak ni kichocheo cha umasikini nchini mwake na amejisahau kwa kupumbazwa na Marekanina washirika wake maana wanadhani Muslim brotherhood wakichukua nchi wataungana na al Qaeda na Hizbullah.

  Mwisho tusiombee hapa yatokee ya Tunisia bali ya Misri ila yatupasa kuwa makini sana maana mwisho wake ambaye hatumtaki anaweza akawa anaendesha nchi kichinichini yaani akawa na ushawishi mkubwa kama itakavyo kuwa kwa Hosni Mubarak............
   
 17. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #17
  Feb 12, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Wewe una laana na mbaguzi na mawazo yako ni kama sumu ya kobra,mwanamke gani unaleta udini? Udini hauna tija.Tuishi kwa amani na kwa kupendana uwe Muislam au Mkristo au Mhindu na nk bila kukashifiana.Ujifunze kuchangia huwezi acha.
   
 18. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #18
  Feb 12, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Yaaap! Hilo ndio la kufanya. Wamisri wenyewe wanajua wafanye nini. Tushughulikie yetu.
   
Loading...