Nina mashaka na kingo za barabara ya Tazara Flyover

Nina mashaka na kingo za barabara ya Tazara Flyover

Tuvute subira, tutapata majibu sahihi baada ya ujenzi kukamilika. Kampuni inayojenga ni ya kijapani, wana uzoefu wa ujenzi wa flyovers na interchanges. Tuwe na subira.
 
Flyover hazina taa za kuongoza magari, Tazara bridge zitakuwepo
Una uhakika na unachosema? Njia ya juu(flyover) haitakuwa na taa za kuongozea magari, ila njia za chini zitakuwa na taa, ukitoka ubungo kwenda airport utaruhusiwa na taa, likewise anayetoka city centre kwenda ubungo...
 
Nilisoma picha pale katikati zinapoungana barabara patachimbwa. Gari toka Ubungo zitapita bondeni na kuibukia karibu na TBC pale. Gari toka Ubungo kwenda Airport zitapita ktk mduara pale juu zikipinda kulia ya bonde na kuelekea airport. Gari kutoka airport kuelekea Ubungo zitapita kushoto ya bonde na kunyoosha na Mandela Rd. Bondeni ni kwa magari yanayotoka Ubungo kwenda Temeke na Temeke hadi Ubungo. Darajani ni kwa magari yanayotoka mjini hadi airport na airport hadi mjini.
Unaongelea mduara gani?
Ushawahi kupita pale tazara siku za karibuni?
Kiufupi ile pale tazara ni daraja
 
Hivi na pale huwa wanachimbua nini wasichomaliza?
 
Unaongelea mduara gani?
Ushawahi kupita pale tazara siku za karibuni?
Kiufupi ile pale tazara ni daraja
Ramani picha niliyoiona patatakiwa kuchimbwa kama vile kurasini Highway karibu na daraja. Huenda hiyo ramani imeachwa. Pale palipaswa kuchimbwa barabara ya Mandela lipatikane bonde. Barabara ya bondeni ingeanzia kwa Bakkressa pale na kuibukia TBC. Silioni hilo likiendelea. Lakini nimeona mchoro picha mahali nitautafuta. Sasa "round about" inakuwa juu level ya barabara ya sasa. Inaacha tundu hapo juu unalichungulia bonde na kuona magari toka Ubungo na Temeke yakipita na kuibukia mbele. Wewe ama unapinda kulia kwenda airport ukitokea Ubungo ama unakunja kushoto kwenda town ukitokea Ubungo tayari kukutana na magari yanayoteremka darajani yakikimbilia CBD.
 
Haha nimecheka tu nilivomkumbuka yule jamaa alompa lift rafiki yake toka moshi hadi dar na akiwa amepiga Bia(safari) si chini ya 16. Akipita tazara na huo urabu tutamkuta ananing'inia kwenye machuma .
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Mimi tatizo langu naona foleni INAHAMISHWA KUTOKA TAZARA NA KULETWA CHANG'OMBE VETA MATAA! Barabara hiyo hiyo! Sijui kama wamewaza vizuri hili!
Na mimi nilikiona hichi kitu kitambo ila nikaona labda watakuwa na njia mbadala bila hivyo wasomi wanasema workdone=0
 
Back
Top Bottom