tatum
JF-Expert Member
- Jan 16, 2018
- 5,786
- 4,494
Nimekuwa nikiangalia sana kingo za pembeni za barabara ya Tazara Flyover zinazojengwa nikilinganisha na barabara za juu za nchi nyingine hata ring road za Kenya tu hapo kwenye barabara ya Thika super high way napata mashaka sana kuwa kuna siku ikishafunguliwa tutazipata gari zingine zikiacha njia na kutumbukia nchini.
Wenzetu huko majuu hayo maeneo ya pembeni huwa wanaweka zege hasa kwa urefu reasonable lakini hapa Tazara naona zege fupi kiasi then wameunganisha na mabomba ya chuma kama kingo sasa sijui kiukweli kama baadhi ya madereva wetu wahatapata dhahama.
Hata pale Daraja la Nyerere Kigamboni kingo ni ndefu na imara sana ukilinganisha na hapo Tazara.
Sijui labda ndo viwango vya kimataifa wanavyovijua mainjia wetu mimi sio injinia.