Nina mashaka na kingo za barabara ya Tazara Flyover

Nina mashaka na kingo za barabara ya Tazara Flyover

magari yanapita juu na mengine chini hyo ndo maana ya fly-over.
nilichogundua watu wengi wanachanganya kati ya flyover na interchange.
zile mnazona mabarabara marefu yanapishana juu kwa juu huku yakiwa wamezungukazunguka ni interchange.
flyover ni barabara inayopita juu ya mwenzie hata kama ni ya mita 10
Google kuelewa zaidi
Halina tofauti na daraja la manzese. Tumepigwa changa la macho
 
Nimekuwa nikiangalia sana kingo za pembeni za barabara ya Tazara Flyover zinazojengwa nikilinganisha na barabara za juu za nchi nyingine hata ring road za Kenya tu hapo kwenye barabara ya Thika super high way napata mashaka sana kuwa kuna siku ikishafunguliwa tutazipata gari zingine zikiacha njia na kutumbukia nchini.

Wenzetu huko majuu hayo maeneo ya pembeni huwa wanaweka zege hasa kwa urefu reasonable lakini hapa Tazara naona zege fupi kiasi then wameunganisha na mabomba ya chuma kama kingo sasa sijui kiukweli kama baadhi ya madereva wetu wahatapata dhahama.

Hata pale Daraja la Nyerere Kigamboni kingo ni ndefu na imara sana ukilinganisha na hapo Tazara.

Sijui labda ndo viwango vya kimataifa wanavyovijua mainjia wetu mimi sio injinia.
Uzi huu bila picha ni kuwaacha watu wa mikoani empty kabisaaaaaa.

Naona kasi kubwa ya watu hao kuja Dar kuangalia maajabu mengine baada ya daraja la Kigamboni.
 
mleta mada unaleta mambo ya expansion joint tena shauri yako
 
we jamaa kitu ninachokupendea kwenye mada na reply zako hata kama umejibwa povu hua hupanik wala kujib pumba. Keep it up bro ukiwa marked in that way it sounds much, unaweza uone kawaida ila inakujengea picha nzur sana, bora usibadilike mana pressure ya humu kui handle n kaz,
 
mleta mada unaleta mambo ya expansion joint tena shauri yako
Hakuna hilo hapo mkandarasi ajiulize mara mbili mbili kuhusu hizo kingo za pembeni mwa barabara kama zinakidhi itakapotokea ajali huko juu
 
we jamaa kitu ninachokupendea kwenye mada na reply zako hata kama umejibwa povu hua hupanik wala kujib pumba. Keep it up bro ukiwa marked in that way it sounds much, unaweza uone kawaida ila inakujengea picha nzur sana, bora usibadilike mana pressure ya humu kui handle n kaz,
Thanks kwa ushauri yako na mtazamo wako kwangu
 
Uzi huu bila picha ni kuwaacha watu wa mikoani empty kabisaaaaaa.

Naona kasi kubwa ya watu hao kuja Dar kuangalia maajabu mengine baada ya daraja la Kigamboni.
Tunawapa uchu wa kuja mjini kufanya utalii pia....tunahimiza utalii wa ndani
 
Mimi tatizo langu naona foleni INAHAMISHWA KUTOKA TAZARA NA KULETWA CHANG'OMBE VETA MATAA! Barabara hiyo hiyo! Sijui kama wamewaza vizuri hili!
haya mambo serikali haiwezi kuyamaliza yote kwa maramoja. so ni hatua kwa hatua taratibu yataish. but pale tazara na ubungo mataa ndo zilikuwa sehemu mbaya sana kwa dar. bado mnazi mmoja huwa mida ya saa tano pale mambo si shwari kabisa
 
Tanzania hakuna fly over.
Ile ya Tazara ni daraja kama daraja la pale mtoni mtongani reli inapita juu na magari yanapita kwa chini.

Tumieni maneno sahihi kwa vitu vinavyostahili na msichanganye na kuleta upotoshajai.

Ila muwe makini ili msije mkafa chadema wakakosa kura
Nilisoma picha pale katikati zinapoungana barabara patachimbwa. Gari toka Ubungo zitapita bondeni na kuibukia karibu na TBC pale. Gari toka Ubungo kwenda Airport zitapita ktk mduara pale juu zikipinda kulia ya bonde na kuelekea airport. Gari kutoka airport kuelekea Ubungo zitapita kushoto ya bonde na kunyoosha na Mandela Rd. Bondeni ni kwa magari yanayotoka Ubungo kwenda Temeke na Temeke hadi Ubungo. Darajani ni kwa magari yanayotoka mjini hadi airport na airport hadi mjini.
 
Tunawapa uchu wa kuja mjini kufanya utalii pia....tunahimiza utalii wa ndani
unakutana na expansion joint, daraja la Mwalimu Nyerere...meanwhile unaenda kule uelekeo wa kampuni ya BAM inayopanua uwanja wa MAPIPA yaendao ng'ambo ndio kwa kushoto unaangalia juu unakutana na hizi kingo za barabara ambazo mwanzisha uzi huu amesema haziamini.

[HASHTAG]#OyeeUtaliiWaNdani[/HASHTAG]
 
Ni kweli lile ni kama daraja lolote lazima kingo ziwe madhubuti nimekuwa na mashaka siku nyingi kuusu uwezo wa injinia anaye jenga pale maana hata ujenzi wake ni wakonokono miaka mitatu ni mingi sana pale palitakiwa pakamilike ndani ya mwaka mmoja tu
Wqnaojenga pale ni wachina
 
Nimekuwa nikiangalia sana kingo za pembeni za barabara ya Tazara Flyover zinazojengwa nikilinganisha na barabara za juu za nchi nyingine hata ring road za Kenya tu hapo kwenye barabara ya Thika super high way napata mashaka sana kuwa kuna siku ikishafunguliwa tutazipata gari zingine zikiacha njia na kutumbukia nchini.

Wenzetu huko majuu hayo maeneo ya pembeni huwa wanaweka zege hasa kwa urefu reasonable lakini hapa Tazara naona zege fupi kiasi then wameunganisha na mabomba ya chuma kama kingo sasa sijui kiukweli kama baadhi ya madereva wetu wahatapata dhahama.

Hata pale Daraja la Nyerere Kigamboni kingo ni ndefu na imara sana ukilinganisha na hapo Tazara.

Sijui labda ndo viwango vya kimataifa wanavyovijua mainjia wetu mimi sio injinia.
Labda wayaweka matuta huko juu
 
Back
Top Bottom