Nina mashaka na huyu mwanaume

Nina mashaka na huyu mwanaume

Hivi mnaposema mtu "mpambanaji" na mtu ambaye si mpambanaji huwa mnamaanisha nini hasa?!
 
Wanawake mnaongoza kwa kulialia njaa na shida mkishapata mabwana! Kumbe pesa inauma eeh... Pambana tu si umependa au?
 
Aisee! Kwaakili zangu ndogo na upeowangu finyu huyojamaa hakupendi anapenda helazako,na hatakama anamipango nawewe ataanzaje kutumia pesa pasipo na mipangilio?
 
yote tisa, pesa ya mwanamke huwa ni ngumu...watakaokupa hela kirahisi maybe ndugu wa kike na mama mzazi ila demu wako akupe hela thubutuu, atakachonunua maybe msosi wa buku, akijitahidi sana sana ataishia kukununulia vest na vipafyumu Curious gal
Mimi huwa nikiwa na boyfriend na nikajua ana shida akaniomba hela huwa natoa kwa moyo mmoja sema lazima nikuulize lini utairudisha hela yangu
 
Piga hesabu muda ulikaa kutafuta mume alafu kama vipi muache, ila kila mtu ana weakness, kuna za kuvumilia na kurekebisha. Maoni ya wadau ukichanganya na akili zako utapata jibu
 
Poleni na majukumu wana MMU, naomba niende kwenye Mada moja, kwa Moja Nina mahusiano na mwanaume mmoja, Mimi ni mfanyakazi Na mwenzangu ni mfanyakazi pia,mishahara yetu haitofautiani Sana japo yeye ananizidi kidogo, Cha kushangaza toka nimekuwa nae kwenye mahusiano haishi kulalamika hana hela(sina tabia ya kumuomba hela)amekuwa na tabia ya kunililia shida kila siku,kosa akiona hela nyingi kwenye pochi lazima aombe, niliwahi kuzungumza nae kuhusu tabia yake na future yetu akadai ana majukumu huko kwao ndo maana hela yake haikai. Ana mpango wa kwenda kutoa posa mwaka kesho,naombeni ushauri wenu jamani niko njia panda, huyu mtu akinioa ataihudumia familiar ipasavyo kweli? Tatizo lake jingine sio mpambanaji kabisa, hata ukimuomba ushauri wa jambo la kujenga majibu yake ni zero,naombeni ushauri wenu jamani huyu mwanaume kweli atanifaa iwapo tutaingia nae kwenye ndoa?
Umelamba dume suruali.
 
Dada kimbia mbio huyo anakutumia kwa hela zako ukija kushtuka anamuoa mwingine
 
Sasa mpenzi umeona suluhu ni kuja kuniabisha humu JF aisee, sio vyema kabisa...kama una sababu ya kuniacha ungesema tu kuliko kuja kunianika humu..ila asante nashukuru
 
Sasa mpenzi umeona suluhu ni kuja kuniabisha humu JF aisee, sio vyema kabisa...kama una sababu ya kuniacha ungesema tu kuliko kuja kunianika humu..ila asante nashukuru
Hahahahaha acha ubahili sasa...kweli hela unapeleka kusaidia kwenu au unapeleka kwa mkeo na watoto halafu unamdanganya huyo dada kwamba utamwoa mwakani....

Dada hebu jaribu kukaa na kuyaongea kwa kina bora kuelewa mapema wengine hawarekebishiki kamwe
 
Haha...yaani nyie wanawake watu wa ajabu kweli...kisa jamaa kakuomba hela ndo unataka kumuacha...je? hizo sababu alizokupa zinazomfanya asiwe na pesa ni za kweli?..kwa nn kama kweli wewe ni wife material usijaribu kumshauri namna ya kuongeza kipato?Familia zinatofautiana..kuna ambazo wanawake ndo wanakua ingini ya maendeleo kwa kuwashauri na kuwatia moyo waume zao na kuwasaidia ktk budget?.au husikiagi watu wengi wakidai kwamba baada ya kuoa...mambo yanaanza kwenda vizur hadi kiuchumi....??KAMA KWELI UNAMPENDA KAA CHINI UONGEE NAE KWA UWAZI ujue pesa zake zinaenda wapi?
Kuwa source ya maendeleo au mabadiriko ya huyo jamaa yako..ili akipata mafanikio huko mbele akujumbuke daima...Tulia acha kubabaishwa
 
Si mnapenda 50% 50%, mbona vitu vidogo kama hivi vinawashangaza sasa??
 
Hahahahaha acha ubahili sasa...kweli hela unapeleka kusaidia kwenu au unapeleka kwa mkeo na watoto halafu unamdanganya huyo dada kwamba utamwoa mwakani....

Dada hebu jaribu kukaa na kuyaongea kwa kina bora kuelewa mapema wengine hawarekebishiki kamwe
Sawa Dada nitafuata ushauri wako[emoji41] [emoji41]
 
Ndiyo wakati wako wa kumtengeneza. Ndiyo maana Mungu alikufanya uwe msaidizi wako. Hakuna ready made man utampata. Hebu komaa na huyo jamaa ako he can become better like others only if you blv and you can invest your time, mind and effort on moulding him. Don't let him go.
Let one day the guy be proud of you.

What else you are going to help him if you can't make him a better man of your life?!

Kazi kwako kubadilisha mashine au kutengneza uliyopewa na Mungu
 
Back
Top Bottom