Nina mashaka na huyu mwanaume

Nina mashaka na huyu mwanaume

Huyo mwanaume hakufai na hata wewe humfai, ungeanza kumsaidia kwa ushauri ili abadilike kisha uangalie matokeo kisha uyapime na kuchukua maamuzi
 
huyo ni brother wangu namjua vizuri anapenda mteremko huyo ndio zake na alishaoa mwakajuzi wewe humjuwi na kazi katemeshwa anawatoto wengine wanne mama tofauti
we tuharibie tu mapenzi yetu! Sikulaumu, maana ndivyo alivyochagua mpenzi wangu. Kwani mm kumuweka wazi changamoto za familia yetu imekuwa nongwa? Nimejaribu kumwomba pesa kwa kumpima tu lakini yeye licha ya kufeli mtihani huo kakimbilia kujieleza kwenye mitandao ya kijamii, kuonesha kwamba anataka tuishi kwa falsafa ya chake-chake, changu-chake. Kweli mwanamke mpumbavu hubomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe(mithali 14:1). Basi na mimi nasema nimeghairi kupeleka posa, labda aje aniombe msamaha.
 
Mbona nyie huwa mnaomba au mwanaume hatakiwi kuomba? Mkiomba nyie hamna shida akiomba mwanaume amekuwa omba omba
Huyo kaka ana kazi tena amemzidi mwenzie hela kinachomfanya aombe ni nini......kusaidiana kupo ila sio kwa style hiyo
 
Bora uwe na uhusiano na JIWE kuliko huyo asiyeridhika na mshahara, mpe mshahara wako wa mwezi huu, akipokea mteme.
 
Hakuna hasara kubwa kama kuwa kwenye mahusiano na mtu unaelingana nae karibia kila kitu!!
 
Sasa kama Mungu kakuonesha tabia yake mapema namna hiyo jee unataka sisi tukushauri nini hasa?
Sisi na Mungu nani zaidi?
 
Pole sana dada. Mwanaume ambaye awezi kuwajibika mwanzoni mwa mahusiano huyo atakusumbua mbeleni. Wanaume wengi kipindi hiki wanapenda kuhudumiwa. Fikiria mwanaume anatafuta mchumba wa kuoa anaulizia anafanya kazi gani? za kuambiwa changanya na zako. Atakusumbua mbeleni.

Fanya maamuzi mapema.
Asante kwa ushauri
 
Huyo sio mwanaume anakuona wewe mama yake mzazi ndio maana kila wakati anakulilia lilia shida, piga chini Mimi sikushauri kua na mwanaume dhaifu kama huyo !! Atakusumbua sana na usikute pesa anapelekewa mwenzio
 
Ndio lakini sikumpa, anachonikera analialia njaa kila uchwao shida yeye hazimuishi
Lakini kunako 6 kwa 6 vipi anakukojoza ipasavyo mpaka maji wayaita mma au na huko pia ni goigoi??

Tuanze hapo kwanza bibie,
 
umekua nae na umeridhia akatoe posa meaning unampenda kama alivyo..haya mapungufu yapo kwa kila binadamu...unaweza ukasema umuache ukaangukia kwenye moto zaidi....je hayo matatizo anayosema yapo kweli? ushawai kuhakiki?
kama ishu ni kipato hio ni changamoto kwa wengi sio yeye tu, cha msingi ni muwe wabunifu kuongeza kipato ili hizo changamoto mzimudu kwa pamoja.
be careful not jump from a frying pan into th fire...
 
Kuna kusaidiana katika mahusiano but not to that extent kama huyo mkaka

yote tisa, pesa ya mwanamke huwa ni ngumu...watakaokupa hela kirahisi maybe ndugu wa kike na mama mzazi ila demu wako akupe hela thubutuu, atakachonunua maybe msosi wa buku, akijitahidi sana sana ataishia kukununulia vest na vipafyumu Curious gal
 
Back
Top Bottom