Nina kazi lakini sina amani nayo...

nnavyopenda kazi za kuzunguka/kusafiri!

pole sana mkuu,labda jaribu kutafuta kitu una passion nacho ufanye nje ya kazi
 
Hahahah umenikumbusha mbali sana, kuna kipindi nilijaribu kujiajiri nilikuwa nafungua ofisi saa tatu asubuhi nafunga saa tano usiku.Nikienda kulala naota nipo kazini naamka nimechoka tena napata ugumu kwenda kufungua ofisi.

Nikakosa furaha ikabidi nitafute ajira kwa mbinde hahahah mpaka sasa siwezi endelea na kitu nisichokipenda na moyo wangu ukiwa mzito sifanyi jambo.
Yaani inakera moyo sometimes naamua kunywa mtungi nijipoze najikuta naanza kuleta stress
 
Yaani inakera moyo sometimes naamua kunywa mtungi nijipoze najikuta naanza kuleta stress
Sema inahitaji maamuzi magumu...anza kutuma maombi ya kazi sehemu nyingine au anza kutafuta connection ya kazi nyingine au uwe muwazi uongee na uongozi wa hilo shirika wakubadilishie majukumu hayo ulonayo umeyazoea huna cha kujifunza
 
Yeah yan sometimes nakosa ufanisi kabisa lakini wao wananiamini sana kwamba hii kazi naiweza.
Sema inahitaji maamuzi magumu...anza kutuma maombi ya kazi sehemu nyingine au anza kutafuta connection ya kazi nyingine au uwe muwazi uongee na uongozi wa hilo shirika wakubadilishie majukumu hayo ulonayo umeyazoea huna cha kujifunza
 
Usifungue biashara! Save kidogo kidogo, bana kidogo matumizi. Baada ya mwaka acha kazi, Fanya mambo mengine ikiwemo biashara!

Km unamshahara mdogo Na ukataka kufungua biashara unaweza jinyonga bure
 
Duuuh na biashara yenyewe sina uzoefu nayo means sijawahi fanya.
Usifungue biashara! Save kidogo kidogo, bana kidogo matumizi. Baada ya mwaka acha kazi, Fanya mambo mengine ikiwemo biashara!

Km unamshahara mdogo Na ukataka kufungua biashara unaweza jinyonga bure
 
Mimi pia miezi kama 6 nimekuwa napitia hali kama yako. Lakini baada ya kusikia watu wangu wasio na ajira wanavyo sota mtaani kipindi hiki, nimejirudi sasa kazi yangu naipenda sana. Nilikuwa nimesha pata mtaji ili nianze biashara lakini niliposikia mambo ya TRA nimeufyata.
 
Nipe hiyo mechanism ya kurufisha mori mkuu
 
Mkuu hajarogwa kabisa,hiyo kawaida sana...na ilinitokea tena nilikuwa na shavu sana,I didn't like the job.

Nilikuwa naboreka nikiwa kazini, now nimejiajiri nakimbiza mishe mtaani.

Fanya kitu kitakachokupa furaha.
Trust me motivation speakers tunawaomba kwenye huu uchumi wa kati/awamu ya kishindo msiwajaze watu upepo wa kuacha kazi watakuwa vichaa na hii laana itawahusu.
 
Tafuta faida za hiyo kazi,Inatunza familia yako,inakuweka mjini, basi ipende. Pia siku hizi maisha yamekuwa magumu,ajira hazipatikani,hata ukianza biashara kuna changamoto zake. Unalipa kodi hata kabla ufungue biashara,hujui italipa au la. Fanya kutunza kidogo kidogo,usitumie mshahara wote.
Nipe hiyo mechanism ya kurufisha mori mk
 
Mkuu pole sana ... ni kawaida watu wengi wanafanya kazi ambazo hawapendi ila ni maisha tu inabidi ukomae. usiache kazi bila kazi maana utajua ni jinsi agani ilivyo kazi kuwa na stress wakati huna kazi.
Si unajua duniani usipojifunza utafunzwa, lakini usipojitunza hakuna atakayekutunza.
Kuwa kama binamu usifanya move mpaka uwe na plan mkuu

Au ninasema uongo ndugu zangu?
Tewalaa
 
Back
Top Bottom