Nina kazi lakini sina amani nayo...

Naomba kujua ni kazi ya aina gani hyo? pengine naweza kutoa ushauri kulingana na mazingira

Sent from my phone
 
Ajira ni kwa ajili ya Ujira.

Kimsingi tunapenda Ajira zetu kwa sababu ujira tunaopata.
Ujira kama haukupi unachoamini kinakustahili (bahati mbaya hakuna ujira unaotosha)
Lazima tu utachukia Ajira.

Sasa kuna haya machache ya kufanya
1. Kutafuta sababu nyingine ya kupenda na kuitahamini kazi yako(hii utaipata utakapotandaza CV na kutoitwa kwenye usaili au kuitwa kwenye usaili ila usiitwe kwenye offer.

2. Kukumbuka kuwa unafanya kazi kwa ajili ya survival na sio mahaba.
Utaacha hii habari ya kusingizia unaumwa ili tu usiende.

3. Kuzungumza na mwajiri wako akubadilishie mazingira ya kazi na akuongezee ujira maana uliona nao unaona haitoshi na haulingani na unachozalisha ( hii inategemea wewe ni wa muhimu kiasi gani kwenye nafasi iliyopo, kama kazi unayofanya inaweza tu kuwa replaced na yeyote with a just a blink of an eye, usitikise niki kiberiti.

4. Kuanzisha biashara kabla ya kuacha kazi.

5. Kuacha kazi na kuingia mtaani mazima kupambana( huku hakuna visingizio vya naumwa, ni ukilala fresh, ukiamka fresh.

6. Mwombe Mungu akusaidie kujua your life purpose.
Wakati mwingine huwa tunashindwa kueexcel kwa kuwa tunafanya mambo yasiyo yetu.
So sali buddha ujue japo kusudio lako duniani.

Mwisho kabisa MAISHA HAYAKUPI HII LUXURY KIHIVYO.

HEBU FACE THE REALITIES.
HALAFU JIPE MIAKA 5, are you seeing them anywhere from where you stand?
If not.
Rudia namba 1-6 na uzifanyie kazi.
All the best.
 
Ajira ni kwa ajili ya Ujira.

Kimsingi tunapenda Ajira zetu kaa sababu ujira tunaopata.
Ujira kama haukupi unachoamini kinakustahili (bahati mbaya hakuna ujira unaotosha)
Lazima tu utachukia Ajira.

Sasa kuna haya wachache ya kufanya
1. Kutafuta sababu nyingine ya kupenda na kuitahamini kazi yako(hii utaipata utakapotandaza CV na kutoitwa kwenye usaili au kuitwa kwenye usaili ila usiitwe kwenye offer.

2. Kukumbuka kuwa unafanya kazi kwa ajili ya survival na sio mahaba.
Ntaacha habari ya kusingizia unaumwa ili tusiende.

3. Kuzungumza na mwajiri wako akubadilishie mazingira ya kazi na akuongezee ujira maana uliona nao unaona haitoshi na haulingani na unachozalisha ( hii inategemea wewe ni wa muhimu kiasi gani kwenye nafasi iliyopo, kama kazi unayofanya inaweza tu kuwa replaced na yeyote with a just a blink of an eye, usitikise niki kiberiti.

4. Kuanzisha biashara kabla ya kuacha kazi.

5. Kuacha kazi na kuingia mtaani mazima kupambana( huku hakuna visingizio vya naumwa, ni ukilala fresh, ukiamka fresh.

6. Mwombe Mungu akusaidie kujua your life purpose.
Wakati mwingine huwa tunashindwa kueexcel kwa kuwa tunafanya mambo yasiyo yetu.
So sali buddha.

Mwisho kabisa MAISHA HAYAKUPI HII LUXURY KIHIVYO.

HEBU FACE THE REALITIES.
HALAFU JIPE MIAKA 5, are you seeing them anywhere from where you stand?
Of not.
Rudia namba 1-6 na uzifanyie kazi.
All the best.
Nashukuru sana mkuu
 
Vumilia kwa wakati huu lakini on the other side tafuta mbadala au kazi ambayo itakupa amani ya moyo, kumbuka makazini na mahali ambapo tunaspend muda mwingi kuliko nyumbani kwa hiyo kufanya kazi ambayo haikupi furaha its meaningless kwenye maisha, sema usiache kazi mpaka upate kazi nyingine
Thank you !
 
Watanzania wengi kama sio waafrika wengi tunafanya kazi inayotokea mbele yetu, wengi tunafanya kazi ambazo sio ndoto zetu ila kujikimu tu.
Hii imekwenda mpaka vyuoni watu hawasomi kwa mapenzi wanaangalia kozi ambayo ina ajira nyingi kwa wakati huo, siku za nyuma pengine mpaka sasa watu walikimbilia ualimu.
Kwahiyo hauko peke yako tuko wengi, binafsi nafanya kazi ambayo sijawahi kuvutiwa nayo na mpaka kesho siikubali wala nini lakini ukizingatia hali ya mtaani hakuna ajira na unaambiwa thamini kazi yako ukitoka nje ya kazi ndio utajua kazi yako ilikua bora
Tukizungumzia kipato, mshahara haujawahi kutosha, sasa nawaza nikitoka huko nje nataka nilipwe bei gani initoshe?
Mimi nafikiri cha msingi ni kujiboresha katika kazi hiyo hiyo, kuwa na juhudi pengine ikakuweka katika position ambayo hutakereka na kazi, pia kutumia kipato hicho hicho kujifanyia maendeleo

Mengine yatafuata baadae
 
Wakuu bila shaka hamjambo !

Aisee mimi ni mfanyakazi wa shirika moja nafanya kazi kwa kuzunguka the whole week.

Nachojishangaa hii kazi nahisi kabisa siitaki ila nafanya tu basi.

Kuna siku siendi nasingizia uongo wowote nashinda ndani. Kuna muda nahisi kama nimelogwa kabisa.

Mshahara ni wa kawaida sio wa kulipa pango na kujenga yani ni hela ya kubadili mboga na kulipa kodi.

Sasa najiuliza nitaishi hivi hadi lini, nimejitahid kubalance angalau nifungue biashara lakini wapi !!

Kiufupi sina mood na kazi hii. Huu ni mwaka wa 2 tangu niajiriwe.

Najihisi vibaya kila ikifika asubuhi.

Wakuu naweza kuwa na tatizo gani ?
Acha ndo utagundua umetupa dhahabu na uneokota jiwe
 
Kuna siku nlikua namsikiliza Sheikh mmoja hivi...Alisema mtu anaweza kuwa na kazi lakini akiamka asubuhi anapata uzito mkuubwa kwenda kazini.....Inawezekana ikawa Ni Mambo ya kichawi..

So Kama hili Ni Tatizo Basi litafutie utatuzi..
Lakini pia unaweza badilisha kazi..unatafuta sehemu Nyingine.
 
Mkuu hajarogwa kabisa,hiyo kawaida sana...na ilinitokea tena nilikuwa na shavu sana,I didn't like the job.

Nilikuwa naboreka nikiwa kazini, now nimejiajiri nakimbiza mishe mtaani.

Fanya kitu kitakachokupa furaha.
 
Hahahah umenikumbusha mbali sana, kuna kipindi nilijaribu kujiajiri nilikuwa nafungua ofisi saa tatu asubuhi nafunga saa tano usiku.Nikienda kulala naota nipo kazini naamka nimechoka tena napata ugumu kwenda kufungua ofisi.

Nikakosa furaha ikabidi nitafute ajira kwa mbinde hahahah mpaka sasa siwezi endelea na kitu nisichokipenda na moyo wangu ukiwa mzito sifanyi jambo.
 
Kuna siku nlikua namsikiliza Sheikh mmoja hivi...Alisema mtu anaweza kuwa na kazi lakini akiamka asubuhi anapata uzito mkuubwa kwenda kazini.....Inawezekana ikawa Ni Mambo ya kichawi..

So Kama hili Ni Tatizo Basi litafutie utatuzi..
Lakini pia unaweza badilisha kazi..unatafuta sehemu Nyingine.
Sawa mkuu
 
Mkuu hajarogwa kabisa,hiyo kawaida sana...na ilinitokea tena nilikuwa na shavu sana,I didn't like the job.

Nilikuwa naboreka nikiwa kazini, now nimejiajiri nakimbiza mishe mtaani.

Fanya kitu kitakachokupa furaha.
Kweli
 
Back
Top Bottom