Nina huzuni, mpwa wangu anarudi mtaani baada ya kukosa mkopo na mimi kushindwa kumlipia

warthog gun

JF-Expert Member
Aug 9, 2018
1,466
1,256
Nathubutu kusema hivyo kwakua huna ubinadam tumekukosea nini watanzania? Umefanya mambo mengi ambayo wala hujatuuliza sisi watanzania kama tunayahitaji.

Mosi, uko bize kununua hiyo mi mwewe yako kwa kodi zetu tumekwambia tunayahitaji?

Nina mpwa wangu alisoma shule ya msingi yetu yaani ya serikali, secondary amesoma private school, advanced level amesoma shule yetu/serikali, sasa yupo chuo kikuu Dsm mkopo kanyimwa sababu eti ordinary level hakusoma ya serikali, sasa nina maswali ya kukuuliza kama ifuatavyo :-

Mosi, hizo pesa za mikopo kwa ajiri ya wanachuo unatoa mfukoni mwako au ni zetu wananchi?

Mimi nilipomsomesha mpwa wangu private school ina maana nilikupunguzia mzigo kidogo lakini wajibu wako bado upo pale pale wa kusomesha hawa watoto wetu Kwa sababu pesa zinazotumika ni kodi zetu sisi watanzania wala si zako sasa kwanini unakuwa na roho mbaya iliyojaa ukatili namna hiyo? Wewe umetoka kuzimu hakika na kama hujatoka kuzimu basi utakua si mtanzania.

Sasa kulingana na jinsi vyuma vilivyokaza nimekwama kuendelea kulipa Ada ndani ya wiki hii mpwa wangu anarudi nyumbani nina hasira isiyovumilika kodi nalipa kama mtanzania kamili lakini kodi yangu inanunua mitaka taka ambayo wala si kipao mbele chetu.

Mambo ni mengi ya hovyo yanayofanyika katika awamu hii ya tano yaani hasira tu hili limenivuruga na nimevurugwa kweli kweli.
 
Ingawa maneno yako makali lakini una hoja juu ya vigezo vya kuwapa mkopo wa elimu ya juu vijana wetu.
Maisha yanabadilika uwezo wa kiuchumi wa mlezi au mzazi aliokuwa nao miaka mitatu iliyopita sio sawa na leo.
Watu wanapoteza ajira, biashara zinafilisika n.k.

Kwenye hili serikali ilipitie upya mtasababisha vijana wengi wenye vipaji wakose elimu ya juu.
Mtasababisha watoto wa maskini wakose elimu, umaskini humjia mtu wakati wowote.
 
Ukatili mwingine ni kunyimwa kwa ajira kwa watoto wawanyonge, kwani mpaka Leo hii yapata miaka mnne , huyu mtoto aliesomeshwa ,na mnyonge ajira anazisikia tu magazetini. Utasikia selkali ya mwaga ajira. Ukizifuatilia ni 4500 out of 910000 yaani ratio ya 1 out 20. Huu ni ukatili ambao hats shetani hawez kuufanya. Ila ikumbukwe kuwa Mungu hajawahi kumwacha mja wake.
 
Huyo mpwa wako hana baba yake mpaka wewe umlipie? Mmeshindwa kumudu mambo madogo ya familia yenu mtayaweza ya taifa? Kwanza mtafute baba wa mtoto alipe karo ya mwanae.
Mnaendekeza kutojali kwenye familiya yenu halafu mnasingizia Rais! Fix your own problems first.
Mkuu usiongee hivyo.
Haya maisha yana mambo ya ajabu na ya kusikitisha sana, kabla hayaja kutokea hayo mambo iwe kwako wewe au nduguyo huwezi kuamini na unaweza kuleta dharau na kejeli kubwa sana.
 
Ukatili mwingine ni kunyimwa kwa ajira kwa watoto wawanyonge, kwani mpaka Leo hii yapata miaka mnne , huyu mtoto aliesomeshwa ,na mnyonge ajira anazisikia tu magazetini. Utasikia selkali ya mwaga ajira. Ukizifuatilia ni 4500 out of 910000 yaani ratio ya 1 out 20. Huu ni ukatili ambao hats shetani hawez kuufanya. Ila ikumbukwe kuwa Mungu hajawahi kumwacha mja wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu dunia nzima hakuna serikali inayo ajiri wahitimu wote wa elimu ya juu na elimu ya kati.
Ajira ni tatizo kubwa hata nchi kubwa kama Marekani, Uingereza, n.k.
 
Back
Top Bottom