Nina hasira za karibu. Naachaje hii tabia?

Nina hasira za karibu. Naachaje hii tabia?

Humayra

Senior Member
Joined
Apr 25, 2020
Posts
130
Reaction score
152
Salam wapendwa, nina hii tabia ya kuwa na hasira za karibu (short tempered), na nikichukia huwa sipati subra ya kukaa kimya yaani naropoka maneno makali mno, mpaka kuna muda siamini kama ni mimi ndo nimeongea hayo maneno, tatizo nimelijua.

Sasa nawezaje kujicontrol maana najikuta narudia rudia kosa nakuja jutia baadaye. Nimemropokea mubebe once, this time kaninunia.

Naombeni ushauri nifanye nini niepuke hii hali wakuu, nijicontrol vipi eti?

Wasalaam!
 
Mm hua naachia machozi ili kujizuia kuongea maana ukiongea unaweza kuta mtu kakukata mapanga

Na short tempered hua husubiri mtu amalize kucall, beep tu inatosha kupandisha morali
 
Punguza tu kimbelembele cha kuongea na kila mtu... Pesa inaongea, itumie ikusaidie kuongea na hao wanawake...Akinuna mnyime, akikufuruhisha mchape sana pesa, ukifanya hivyo hatakukasirisha tena.Na utapunguza watu wanaokufanya ukasirike. Nadhani hao ndo wanaoongoza.
 
Punguza tu kimbelembele cha kuongea na kila mtu... Pesa inaongea, itumie ikusaidie kuongea na hao wanawake...Akinuna mnyime,akikufuruhisha mchape sana pesa,ukifanya hivyo hatakukasirisha tena.Na utapunguza watu wanaokufanya ukasirike.Nadhani hao ndo wanaoongoza.
mimi ni KE mkuu
 
Mm hua naachia machozi ili kujizuia kuongea maana ukiongea unaweza kuta mtu kakukata mapanga

Na short tempered hua husubiri mtu amalize kucall, beep tu inatosha kupandisha morali
Muda huo nalia huku simu ipo mkononi natuma msg heavy.
 
Kila mtu ana njia ya kutoa maumivu yake moyoni, hivyo wewe kuropoka kwako ndiyo njia yako ya kutoa ya moyoni kwa maana ya kuwa usipofanya hivyo lazima utapata shida kubwa kihisia kwa kutunza vitu ambavyo hujavitoa.

Lakini kwa kuwa njia hiyo unaona siyo nzuri kwako inabidi utafute njia nyingine ya kutoa hisia zako kwa kuwa huwezi kukaa na kitu moyoni vinginevyo utadhurika zaidi.

Kuna njia nyingi kwa kutaja chache...
1. Kulia kiasi cha kutoa machozi
2. Kwenda mbali na eneo ambalo linakufanya ukasirike.
3. Kufanya kitu ambacho huwa kinakupa furaha au faraja kama kusikiliza muziki, kucheza games, kuangalia movies, kufanya mazoezi ya mwili nk.

Ukishapata njia mbadala kati ya hizo au yoyote utakayoona inafaa, anza kuitumia kila unapokubwa na hisia hizo. Inaweza kuchukua muda mrefu lakini si kuwa haiwezekani.

Asante.
 
mimi ni KE mkuu
Pole sana. But njia rahisi ni kujifunza the art of being understanding. Utaweza vipi, everytime unakutana na situation ngumu ku handle look on the positive side. Mume amekunyima hela ya kufanya jambo flani...try to think pengine ana save kwa ajili ya kufanya jambo la maana zaidi kwa ajili yenu. Usianze kuwaza unanyanyasika...utaishia kupayuka hovyo na kumboa mwenzio.

Mume amechelewa kurudi home, badala ya kuanza kuwaza alikuwa kwa mchepuko ukaanza kujinunisha na kumropokea mineno ya kishenzi, anza kwa kuuliza you never know gari ilipata hitilafu au alipata emergency nyingine njiani. Maelezo atakayokupa yapokee positively achana na maswala ya kumchimba chimba.

Ofcourse we Men make mistakes kama binadamu ila wengi wetu huwa hatupendi makelele, once we explain something to you tunapenda mchukulie positively. It sucks mtu anapaza sauti ana blow out kama tanker la petroli lililolipuka msamvu,the moment unamwambia kitu ambacho hakutaka kusikia hata kama hujamaliza sentensi.

The only reason i keep some matters to myself ni hio mikelele but naishiaga kupewa lawama why hiding things up! I do it because nikikushirikisha utaanza kubwatuka like shit!!!🤣🤣🤣

Aftermath ya hio tabia kama si kuachwa mazima ujue deile utakuwa unachitiwa na nyumbani utaspend mda mwingi ama mwenyewe au na wanao tu. Lazma kuwe na nyumba ndogo ya kupunguza machungu ya mumeo.
 
Tunaziita "HASIRA MKURUPUKO".

Mara nyingi huwa zina majuto tena ipo siku utajutia zaidi. Au zitakupelekea kuishia pabaya sana.

Mara nyingi huwa mnakuwa wakorofi. Kila kitu ukiguswa tu, basi unawaka.

Ila kwakuwa umelifahamu tatizo lako , utajitahidi kuji-contro.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom