Nina harisha damu lakini sina maumivu ya tumbo

Picha tuone
20240121_153212.jpg
 
Pole mkuu miaka ya tisini niliwahi kuharisha damu ilikua mbaya sana aisee mama yangu mdogo kuna dawa akanipa ni ya kuchuma ni kama majani unayakamua yanakua kama uji aisee kesho yake tu ilikata hiyo dawa nilileta fujo ipo home moshi mpaka leo

Ila kwa ushauri tafuta hospitali kubwa kama rabinsia au muhimbili

Pole ila wahi hospitali
 
Tangu jana nimekuwa nikiharisha damu. Sina maumivu yoyote ya tumbo na wala sipandishi homa.

Leo nimeenda hospitali wamenipa dawa za minyoo. Je minyoo inaweza kusababisha uharishe damu?

Au ndio nimekutana na daktari kihiyo?
Una posibility kubwa ya kuanza bawasili
 
Kuharisha damu ni swala moja ila tumbo kutokuuma hilo ni swala tofauti kabisa.

Kwa uzoefu wangu utotoni niliwahi kuumwa Amoeba ila sikufika hatua ya kupata choo chenye damu lakini tumbo lilikuwa linauma kwa kukata mpaka unaenda chooni unatembea ukiwa umeinama, hivyo kwa maelezo yako sidhani kama ni Amoeba.

Pia sidhani kama ni Ulcers maana mpaka muda huu ninaandika ninazo na huwa zikichachamaa tumbo linauma unaweza kupiga ukelele wa kuomba msaada, pamoja na hayo sijawahi pata choo chenye damu hivyo sidhani kama ni Ulcers.

Kuhusu kichocho sina uhakika kwa sababu sina experience nacho ila ninachojua dalili moja wapo nikutoa mkojo uliochanganyika na damu kwa sababu wataalamu wanadai kichocho ni UTD's (Urinary Transmitted Disease) kwa mantiki ni kwamba zinaaffect njia ya mkojo sasa kwa haja kubwa sijajua, labda tusubiri wataalamu.
 
Pia sidhani kama ni Ulcers maana mpaka muda huu ninaandika ninazo na huwa zikichachamaa tumbo linauma unaweza kupiga ukelele wa kuomba msaada, pamoja na hayo sijawahi pata choo chenye damu hivyo sidhani kama ni Ulcers.


Usicheze na ulcers kabisa, ukifika stage ya kuharisha au kutapika damu ujue ndio stage ya mwisho kifuatacho ni aidha kifo au kansa ya utumbo.

Jitibie harakaaaaaaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom