Nimvumilie mume huyu au nimuache? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimvumilie mume huyu au nimuache?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by dadamnyonge, Nov 22, 2011.

 1. d

  dadamnyonge Member

  #1
  Nov 22, 2011
  Joined: Nov 22, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mm n msichana nna miaka 26,nmeolewa na nna mwaka wa 4 sasa katka ndoa.mume wangu amenipita kama miaka 12 hiv
  Tatzo ni mume wangu ana wivu sana,asisikie kitu hana haja ya kufatilia km n kweli au lah ye ananihukumu tu.ameshanitoa kwake zaid ya mara 3 nami narudi home, baada ya miez kadhaa huwa ananifata na kutaka nirud tukaish sote.

  Nikirud matatizo n yaleyale, hana muda wa kuwa nami hata kidogo, akitoka asbh kurud usiku saa 8 au 9. Had ss cjabahatika kupata mtoto nahc kutokana na stress na hata tendo la ndoa n nadra sana kwetu kwan amehama chumba yapata miez 6 sasa,so ukitaka game had umfate na anaweza akakubal au akaushe.matuc ni jambo la kawaida kwake na gubu ,nyumba yangu, ktanda changu n maneno yake had inakuwa kero.
  kila siku ni kuninyanyasa. yan nakosa raha ya kuwa na mwenza,hakuna hata muda wa kupga story na hata akitoka haagi kabsa.
  Nampenda sana mume wangu nmejaribu kukaa nae na kuzungumza hakuna unafuu wwt had sasa.

  Nmebahatka kumaliza degree ya kwanza chuo cha UD,nawaza nitafute kaz ili niondoke nikaanze maisha yangu upya, nnachowaza ndoa yangu n ya kanisan na kama mjuavyo ugumu wake, lakin upande mwingine nataman nam niwe na maisha ya furaha na mtu atakaenijal, kuniheshimu na kunipenda kwa dhat ,na ukizingatia umr wangu mdogo bado ntamvumilia for hw long!

  Naomba mnisaidie kwa ushaur*
   
 2. Black Rose

  Black Rose JF-Expert Member

  #2
  Nov 22, 2011
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 243
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  OH! Mungu weeeeeeeeeee!! Unafanya nini huko kwa huyu mtu mbaya ivi?
  Ndoa yenu ni ya kupangiwa..... au mlipendana wenyewe?
   
 3. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #3
  Nov 22, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  pole sana
  km nimimi kwakweli ningechapa mwendo....as my husband kahama adi chumba wat does min?
  unyumba mpaka ukamgongee mlango...john naomba leo tufanye ahhhhhgggghhh ova my ded body apana.stak,nakataa hali hiyo.

  ongea na wazee kwa mara ingine waambie kinachokusibu labda wanaweza wakamweka sawa

  life is to shooot jaman kwanini umfanyie ivo mwenzako dah so sad...
  yaan unajaribu kujipendekeza kwa mmeo mambo yaende sawa lakin ye wapppp haon wala hatambui ...LAKIN KUNA WATU WANAPENDA KUWAFANYA WENZA WAO WAWE KTK HALI YA UNYONGE yaan uwe nyenyemaaa juu yake apo ye ndo anaona yap...anapata raha zote

  mwenzangu umri wako bado mdg na km nionavyoa apo misingi yote ya ndoa akuna...jamaa uenda ana mahusiano mengine wew anakufanyia visa usepe..mwandikie barua ndefu mwekee kitandan kwake ..mwambie km bado anakuitaj au akuitaj ...tel hm 2b frank n honest km kakuchoka aseme lakin si kuleta visa km panya mwenye fistula ahh yan nataman nimpe ya chembe

  mbaya zaid et anakusimanga..kitanda changu,nyumba yangu,meza yangu,kikombe changu...ahh apo apana..ningevumilia yote bt not manyanyaso apo apana...afu mbaya zaidi una mtaji wa elimu ..iyo dgree tumia vzur mama.tafuta kazi .tafuta chumba ukapange afu mwambie m stl yrs siku ukijiskia kuwa MUME WA MTU MWENYE KUJUA MAJUKUMU NA WHAT IT TAKES TO B IN MARRIAGE PLS LET ME KNW I WL B BAK..naend akupanga mwenge .mtaa mpakan.ur welcome any time..akikuona una msimamo na wwala aumtetemekei tena ATAAMKA KDG toka usingizin


  NDOA NI MAELEWANO.HESHIMA NA UPENDO km hakunaga izo mambo basi hakunaga ndoa.
  kwan auwez kuish bila ndoa?sepa mwaya...ila akijirud mpokee asi unajua tena altare ilishawaunganisha? sema angaza 1st.

  pole mami i fl wat u fil lakin ngumu dahhh iki kitanda changu....chooo changu ahhh mistak.
   
 4. Tausi.

  Tausi. Senior Member

  #4
  Nov 22, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mmmmhhhhh kweli ndoa ina mitihani,
  Muda wote umesubili nini mdogo wangu, maisha yenyewe haya mafupi saaaana, kisa cha kujipa taaabu ni nini na huyo gumegume anayeondoka asubuhi na kurudi saa tisa????? Hiyo sio ndoa dear, achana nae unakasoro gani wewe, kwa nini usismame imara, kisa ndoa ya kanisani? Mpeleke basi kwa padri aliyewafungisha ndoa labda atajirudi. Wengi wanawake wananyanyasika, hawajawa educated lakini hata wewe, Plizzzzzzzzz zama hizi sio za kulia lia. Hebu wasikilize na wadau wengine.
   
 5. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #5
  Nov 22, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,499
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160
  Kumbe umesoma yaani una bachelor???? Anza kutafuta kazi haraka sana. Ukiwa na kazi yako utaheshimika! Usisubirie kuwa golikipa kwani huyo mwanaume anakuona wewe una dhiki sana na bila ya yeye huwezi kuishi. Na hii ni dhana potofu!!!

  Acha kuwa mnyonge wa kuonewa kila siku. Wazazi wako walikusomesha ili uje kuwa na maisha mazuri na sio mtu wa kulialia kilasiku.

  Kuhusu huyo mumeo na tabia zake nenda ukaongee na viongozi wako wa dini au ndugu zake nahisi watakusaidia kama bado wampenda mumeo. Ila kuwa makini kama mume hajatulia atakuletea gonjwa UKIMWI! kuwa mwangalifu!!!
   
 6. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #6
  Nov 22, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  wazo la kuoana ulilitoa au alilitoa yeye?
  mlikaa mda gan b4 ndoa?
   
 7. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #7
  Nov 22, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  wazo la kuoana ulilitoa au alilitoa yeye?
  mlikaa mda gan b4 ndoa?
   
 8. bht

  bht JF-Expert Member

  #8
  Nov 22, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  ndoa ya kanisani....so what?
  'tendo la ndoa'....unapewa kwa msimu
  'unasimangwa'....kila kitu chake
  'hakuamini'.....ulishampa sababu za kutokukuamini?
  Binti hebu kwanza 'jishughulishe'...fanya kazi umsaidie mumeo kujenga familia, maisha ni magumu, hata yy ni binadamu, pengine ana mengi yanamsonga na hivo anaishia kumalizia hasira kwako....
   
 9. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #9
  Nov 22, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  rose........................... naona umekuwa mkali kweli..................... mwache mwenzio aendelee kuvumilia bana............. maisha marefu sana haya, mambo yake yatajipa yenyewe mbele kwa mbele.................
   
 10. N

  Nsuri JF-Expert Member

  #10
  Nov 22, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 997
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 60
  Hiyo tofauti ya umri pia tatizo..na huyo mume wako inawezekana ana mwanamke mwingine, haiwezekani mtu uhame chumba bila sababu ya msingi. Nakushauri tafuta kwanza kazi ukishapata uanze kujitegemea..Huyo hafai kuwa mume coz alitakiwa kusema kama kuna tatizo na co kuhama chumba na kugombana kila mara
   
 11. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #11
  Nov 22, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  He yaani mpaka kahama chumba?? Bado umekaa tu unasubiri nini???
  Anarudi saa 8 or 9 usiku are you serious?? Ni mlevi?? Je! anakuwa anatoka wapi??
  Mahusiano ya nje?? Unajua??

  We chukua hatua si mpaka kwa hisani ya watu wa marekani ndo uelewe
  Chapa mwendo Ndoa ndoa ndo nini??? Waliachana kina Winie Mandela ije kuwa wewe??
  Yanini ujipe matezo duniani wakati bado unajipenda?? Tena una degree halafu unailalia
  Tu kitandani?? Halafu we mwanamke wa wapi wewe bado umelala mpaka leo
  Eti unanyanyaswa umekaa tu?? Hivi husikii hata wanaharakati wanavyosema??
  Wanawake wanaweza??? Hebu funguka macho wewe acha kulegea ahhh
  Cha uzembe kama huo bana............
   
 12. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #12
  Nov 22, 2011
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Pole sana kwa matatizo uliyonayo,hapa unaweza kupata ushauri wa kumuacha huyo mwanaume ila bado hatujui ya ndani zaidi yaliyofanya mpaka mkafikia hivi,kwangu mimi naona kuna mambo ambayo yalisababisha mpaka mmefikia hapa na ambayo huwezi kutuwekea hapa kwa undani.
  Kwa kuwa umekwishaona kuwa kuna matatizo basi tumia vizuri kitchen party uliyoipata,au ndio siku hizi umeifanya fasheni yaani unashereheka tu bila kujua ni nini mwanaume anataka katika ndoa?
  Angalia unavyoona inafaa kulingana na maisha ambayo uliyapanga na haijalishi una degree au phd maisha ni namna unavyoyaendesha si elimu uliyoipata ndiyo itakayoamua mustakabali wa maisha yako zaidi ya kukusaidia tu katika kuyaendesha.
   
 13. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #13
  Nov 22, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Hata mie nimeshangaa sana kha???
   
 14. d

  dadamnyonge Member

  #14
  Nov 22, 2011
  Joined: Nov 22, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  n yeye ndie alitoa na akafata taratibu zote
   
 15. R

  Rukiko Senior Member

  #15
  Nov 22, 2011
  Joined: May 5, 2009
  Messages: 199
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  dada yangu, unaposema ndoa kumbuka kuwa kuna changamoto zake!
  kusoma na kupata degree na kazi nzuri si kigezo cha kuvunja ndoa!
  pamoja na kumueleza yote unayotaka kufanyiwa, nakushauri pia ujitathmini ni kipi kinachomfanya kutoka kwako ahame chumba na kurudi usiku.
  mara nyingi huwa tunapenda kuwanyooshea wengine vidole kuwa wana makosa huku ya kwetu tukiyaziba yasionekane.
  umesema ndoa ni ya kanisa-je mmekuwa na maombi mfano ya pamoja na ya kwako mwenyewe ukimwombea mumeo??au tu kwa sababu uliolewa kanisani basi. nafikiri una wajibu wa kufanya kuilinda nyumba yako.
  pengine pia nikuulize dhamira yako ilikuwa ni nini wakati mnaoana?kuachana mbele ya safari au kuishi pamoja katika shida na raha??

  ushauri:

  • Zungumza nae;
  • ondoa kiburi na mambo yasiyofaa unayomfanyia mumeo ambayo hayapendi;
  • mwombee kwa Mungu(Mungu asipolinda nyumba alindae hulinda bure);
  • timiza ndoto zako ambazo ulikuwa nazo wakati wa uchumba na ndoa-
  • tafuta kuwa na ndoa yenye mafanikio-(to run awaya from the problem is not the way of solving the problem).watu makini hutafuta suluhisho......
   
 16. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #16
  Nov 22, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Ongea ae kwa upendo na unyenyekevu kabala hujaamua kuchukua hatua yoyote!
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Nov 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Samahani kidogo, kama tukimpata huyu mwenza wako na kumuuliza aseme kuhusu wewe na anavyoona unafikiri atatuambia nini kuhusu kiini cha tatizo?
   
 18. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #18
  Nov 22, 2011
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Haraka sana mpe kadi ya njano mwekee kitandani kwake na akiuliza mwambie usipojirekebisha inafuata kadi ya pili, na baada ya hapo piga nyekundu anza maisha ya useja mpaka utakaporidhika kuwa kakoma ushenzi wake,Je mmeo ni Mchaga au kabila gani vile?
   
 19. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #19
  Nov 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  hilo jina kwa kweli linaonyesha u myonge sana
  pole kwa misuko suko iliyokupata
  1. je mmebahatika kupata watoto , wangapi??
  2. je anatabia ya ulevi??
  3. umehjaribu kushirikisha watu wa karibu??
  4. ulipokuwa unaongea nae alikuwa anaonyesha kuelewa usemacho??
   
 20. M

  Mpemba asilia Member

  #20
  Nov 22, 2011
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Isije ikawa ulimlazimisha akuoe sasa anatafuta utimke mwenyewe
  Kaaaaazi kwelikweli
   
Loading...