Mwenye makosa ni nani? Mke au mume?

Mwenye makosa ni nani? Mke au mume?

vanilla

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2012
Posts
448
Reaction score
360
Wapendwa nimesoma hiki kisa nikaona sio vibaya kushare.Kwa wale wenye Ndoa, kuna ambae amewahi kuwa kwenye situation ya namna hiyo? Je ulisolve vipi?

Inaanza hivi...
Nimeolewa miaka 7 iliyopita. Na kujaliwa watoto 3. 6 and 3. Wote wasichana. Familia niliyoolewa ni ile familia ambayo imeshikana sana. Wanapendana wao wenyewe tuu. Na ambao mmeolewa ama kuoa humo hamtambulikani kabisa. Na kama kuna mwanandugu atahitaji msaada basi familia nzima itachanga.
Sikuwa naumia kwa nini wanapendana la hasha. Ila kwa nini wanarutenga.
Yani mama mkwe anakuwa anajua jambo la mume wangu kabla sijajua.
Nakumbuka siku moja Mr alinujua shamba. Na ni shamba kubwa na zuri. Lakini shahidi na mdhamini wa shamba hilo no mdogo wake wa kike anayesoma chuo.
Tena alilipiwa nauli aje kusign. Nilishangaa sana.
Lakini sio kwa sababu ni shahidi hapana.
Ni kwa sababu nilikuwepo na ningeweza kuwa shahidi lakini sikuonekana wa maana.
Swala hilo likikuwa linaniumiza sana .
Yani nakumbuka tena wifi yangu alikuwa na graduation lakini mpaka nguo zake kaka yake ndiye alinunua. Mimi siambiwi kitu. Nakuja kushtukiza tuu wameshaambiana.
Familia hii ikawa inanikwaza sana.
Nikaona kwa nini iwe nongwa?nami nikaanza kufanya mambo yangu peke yangu.
Nakumbuka niliamua kumkomoa.
Nikakopa pesa na kununua gari. Haria. Nilinunua hiyo gari bila kumuambia. Ikaja nyumbani akashangaa sana. Nikamuona kakasirika. Alikuwa kakaa sebuleni wakati naingiza gari. Akaniambia gari ya nani?nikamwambia yangu.
Akaniambia tangu lini unafanya vitu bila kuniambia?
Sikuwq na sababu ya kufikiri jibu. Yani jibu likikuwa chini ya ulimi. Ni kama nilikuwa nahua atauliza ama kusema hivyo.
Sikuchelewesha jibu. Hapo hapo nikigeuka tu nyuma. Nikiwq nimeshikilia funguo za gari na kumwambia...
"Kiwanja cha tegeta uliniambia?
Nyumba ya Kibamba uliniambia?
Gari uliyompa Nancy ukiniambia?alimnunulia mdogo wake gari.

Mr alikuwa kama ana jini la Ububu. Maana alifura hatari. Wakati huo nilikuwa naongea kwa ujasiri sana.

Akaniambia nilifanya hivyo kwa sababu pesa ni zangu.
Sujui ni nini kilitokea ila nilijikuta nacheka na nikamwambia Kwani hili gari nimenunua na pesa yako????
Nikishtukia tu kibao. Ngumi mtama na kupigwa zaidi.
Alinipiga sana.
Na tukazozana sana .
Nikichukia kwa kweli.Akaniambia kama unataka kukaa hapa hilo gari nisilione humu ndani. Chagua gari liondoke ubaki. Ama uondoke na gari yako.
Mh.. niliumia kwa kweli.
Sikusema kitu. Nikanyamaza. Ila nikasema kama ni kuniua utaniua. Ila gari sitoi na siondoki.
***************
Kuanzia hapa maisha yakawa ya ugomvi. Kutoelewana. Alikuwa na frame mahali anauza soda za jumla akampa kabisa mdogo wake moja kwa moja. Hiyo pesa ya hapo tulikuwa tunaipokea kila mwezi tunaiweka kwenye account za watoto. Akasema haihusu tena watoto.
Maisha yakawa hivyo. Hakuna amani kabisa.
Akaanza kutokuwahi nyumbani.
Akaacha kutoa watoto out.
Akaacha kuwapeleja shule.
Akaacha kutoa matumizi.
Kisa tuu Nimenunua gari. Nikikaa nikawaza na kujilaumu sana. Lakini upande mwingine sistahili kujilaumu. Kwani nilihitaji pia usafiri binafsi kunirahisishia kuwahi kazini. Magari yapo nyumbani.. ila moja lake. Lingine kampa kaka yake anaanyia taxi. Na lingine Nancy. Mdogo wake. Yeye anaenda kazini saa moja. Mimi naondoka nyumbani saa kumi na moja na nusu.
Hivyo hayuko tayari kunipa lifti. Nikiumia lakini nikasema potelea mbali.
Akaanza kunisema kwa ndugu zake.
Nakumbuka mama aliugua.
Mama alivyougua wakaambiana kwa siri sana. Mama akaja Dar. Akawa anakaa kwa wifi yake. Na sikuambiwa. Nimekuja kugundua mama mgonjwa baada ya mtu aliyekuwa anamtaka mr ampe pesa za dawa yuko pharmacy. Alipomkosa Mr ndo akanipigia. Ndo nikajua mama mgonjwa. Tena serious. Mgojwa wa operation.
Nikishangaa sana. Yani mama kalala kitandani siku 9 sijaambiwa. Nafichwa.
Nikasema na mimi sihangaiki. Watajijua. Maana wako kama wachawi.
Nikampigia mr simu kumwambia atume hizo pesa dawa za mama zinunuliwe.
Kwanza akitahayari sana.
Lakini hakujali. Kwa sababu hata jioni alipokuja hakuniambia kitu.
..Hivi mnaficha ugonjwa hamjui kifo huumbua?
Nikimwambia tu kwa methali. Nikijua anaelewa.
Dah.. nilijuta. Nikitukanwa mnoooo. Akanifukuza. Akaniambia mwanamke mchawi wewe. Unasema mama yangu afe. Mchawi mkubwa.
Alinitukana sana. Niliumia sana.
Usiku huo huo akaniambia nitoke kwake.
Nikasema natoka. Lakini badae nikasema hapana.
Akampigia dada yake akamwambia niliyosema. Dada yake akamwambia akija happ nitamtambua. Nikaanza kutumiwa msg za matusi.
Nikasema ni gari tu ama?
Nikawa siwajibu nanyamaza.
Akawa yani akitoka kazini anaenda kwa mdogo wake wa kike. Anakaa huko wee mpaka saa tano ama saa sita ndo anakuja.
Nikamuuliza hivi unakaaje kwa mdogo wako wa kike mpaka usiku hivi?yani nilimsema tu ya kawaida.
Akaniambia nimenuambia anatembea na mdogo wake.
Hapa ndipo nilijuta. Familia nzima ikaanza kunijadili. Wakanisema sana.
Mpaka wakapanga kuwe na kikao. Kikao kijatafutiwa tarehe.
Siku ya kikao tukasafiri na kufika .
Kikao kizima ni mimi nilikuwa nasemwa.
*********************
Walinisema sana. Mnoo.
Mwisho wakasema pesa ndizo zinanipa kiburi.
Hivyo ni lazima niamue mambo yafuatayo.
1. Kuacha kazi.
2. Kuuza gari pesa zifanye maendeleo ta familia.
3. Kama siwezi hayo basi ndoa inaweza kufa.
Nikiwaangalia sikuwamaliza.
Ni kweli mume nampenda. Japo sio ta kivileee kwani ananikera. Ila kuvunja familia ama ndoa sikuwa tayari. Sio kwa sababu ni nzuri noo. Ila kwa sababu nilijengwa kuachika ni Aibu.

Nikiwaambia nitawapa jibu.
Mr akaniambia nimpe kadi ya gari. Nikasema nimeiacha nyumbani.
Wakasema lazima niache kazi.
Kikao kikafungwa. Na nikaomba msamaga sana.
Nikarudi nyumbani.
Mr akaniambia gari iuzwe. Mh.....nikamwqmbia hakuna mteja.......

From Irene Mbowe Facebook page...story inaendelea.

Japo kisa hakijaisha lakini kwa upande wangu naona hapo makosa ni madogo sana yaliyopelekea kuzaa kitu kikubwa mno.

1. Reaction ya mke baada ya kuona hashirikishwi mambo na mumewe. Nadhani alipaswa kumueleza kwamba angependelea kushirikishwa then aone kama kuna marekebisho au la kwasababu mara nyingine watu hufanya makosa pasipo kujua kwamba ni kosa na wakiambiwa hujirekebisha. kunyamazia kitu huku ukijua utalipiza baadae sio jambo la busara

2. Mume kuwa too attached na familia yake. Si jambo baya kuwa na ukaribu na familia ila baada ya kuoa Mke wako ndio huja kwanza kabla ya mtu yeyote kwenye chochote kile. Hapa mume hakumpa mke nafasi anayostahili. inaonekana bado hakua ameungana na mkewe kuwa "mwili mmoja". Kwa wale wanaoamini kwenye maombi kuna namna ya kuomba ikitokea mwenza wako bado yupo attached na familia yake maana "mambo mengine hayawezekani isipokuwa kwa kufunga na kuomba"

3. Both do not communicate well with each other. Katika NDOA mawasiliano ni muhimu sana kuliko chochote. mawasiliano yakiyumba tu every aspect ya Ndoa itayumba maana kila mtu atafanya vitu kwa perception yake bila kumshirikisha mwenzie ama kumuuliza maana hakuna mawasiliano..ukaribu unapungua...kutafuta namna ya kulipiza kisasi kama njia ya kufikisha ujumbe...

wewe umeona mapungufu gani kwa wawili hawa? una kipi cha kujifunza? so far who is at fault here?Mwenye makosa kuifikisha hii NDOA kwenye hali iliyopo ni nani?
 
Haya mambo yapo sana.ingawa njia aliyoitumia mwanamke haikuwa ya busara.angejaribu kuongea na mume wake kiupole kuhusu kuwashirikisha sana ndugu kwenye mali hasa for the sake of the childs.
Kuna leo na kesho huwezi kujua!
Kuna maana nyingi katika familia hasa mwanaume kuwa remoted na ndugu zake.imani pia ya ndugu kwamba mwisho wa siku mali zote zitakuwa za mke na watoto hii huwapa wakati mgumu sana ndugu kuona watakuja kufa maskini!lakini mwisho wa siku watoto wako mwenyewe ndio watateseka na kutaabika we ukiwa unachomwa moto jehanam
 
Hii tabia ya ndugu kuwaza Mali za kaka yao mwenye Mke na watoto sijui huwa inatoka wapi. Ila naamini ndugu hawawezi kuingilia Ndoa yako kwa namna yoyote ile hata Mali zako isipokuwa wewe mwenyewe umewapa mwanya/ruhusa ya kufanya hivyo.
 
Wanaume wengine ndio mana wanagongewa wake zao... Sasa huyodada hayo anayopitia akipata wakumliwaza nje si ndoa itakuwa kama sehemu yakutunzia watoto tu....

Hapo sasa
 
HUYO MDADA ATAKUWA MBUMBUMBU AKIKUBALI HAYO MASHARTI.

KIUFUPI TATZO NI HUYO JAMAA ANA TABIA ZA KIKE.

1. GUBU
2. UGOMVI
3. KUDEKA

NI TABIA ZA KIKE, KAMA MKE HANA UMUHMU ANGEKAA SNGLE.

KUNA WANAUME MNATUAIBISHA SANA, NDYO TATZO LA KUWA MTOTO WA MAMA.. KAMA VP OENI DADA ZENU WANAUME WOTE WENYE TABIA HZ NI WANGESE.

EBU ONA, MTU ANAGHAIRI KUTOA HUDUMA KWA WATOTO KISA MKEWE KAMCHUKZA, SASA HAPO ANAMKOMOA NAN? UJNGA MTUPU
 
Usiache kazi
Baada ya Mungu Mkuu
Nikazi yako ndugu yangu
Pia kama ndoa yako sio Amani mwambie Mume wako unaomba upumzike angalau mwaka ukiwa pekee yako ukitafakari kuhusu ndoa yenu
Nb..angalia vyakula unavyokula na kunywa kwako kukuwekea sumu hao nirahisi
 
Mkuu umeandika kwa hisia sana duh!!
Tuseme tu huyo mume is not matured enough kujua nini anapaswa kufanya kutatua tatizo badala ya kukomoana
 
Apumzike ukimaanisha kila mtu aishi kivyake? Naona watazidi kutengeneza gap kubwa kati yao na kuua Ndoa kabisa
 
Apumzike ukimaanisha kila mtu aishi kivyake? Naona watazidi kutengeneza gap kubwa kati yao na kuua Ndoa kabisa
Hapana sio kuachana kila mtu atafakari kwanza umuhimu wa ndoa yao wakiwa mbali
Ndipo mume wake atajua ubora wa mke wake
 
kusema ukweli communication hapa ndio tatizo, pili wanawake wengi hufikiri hazii atabadilika with time, naamini alikuwa hivyo tangia wakichumbiana ila bibie hakuona tatizo. Ushauri wangu ni kwamba watu tuangalie mapungufu na kuyarekebisha kabla hatujaingia ndoani; na incase mapungufu yamejificha yakija onekana tuulizane kulikoni na kupata suluhu.
Wakati mwingine ukisoma story kama hizi ndo unajikuta kusema bora uwe tu single maza uishi maisha ya raha mustarehe katika dunia hii Mungu alotupatia.
 
Hapana sio kuachana kila mtu atafakari kwanza umuhimu wa ndoa yao wakiwa mbali
Ndipo mume wake atajua ubora wa mke wake

Huu umbali sasa unaweza kuzaa talaka. Wakiwa mbali ndugu si ndio watapata nafasi ya kushauri wanachotaka wao kwa interest zao?
 
Mkuu umeandika kwa hisia sana duh!!
Tuseme tu huyo mume is not matured enough kujua nini anapaswa kufanya kutatua tatizo badala ya kukomoana

YANI ANGEKUWA KAMWOA DADA YANGU, HIYO NDOA INGEKUFA SAA 4 ASUBUHI, WANAONEKANA KABISA HAWANA NIA NZURI NA HUYO JAMAA HAJIELEW NA ANA TABIA ZA KISHOGA
 
kwan vip mbona sijaona ambapo mwanamke anaongelea kuhs familia yake yy hana wazazi wala familia ya kumsikiza!!kuna point umeongea kwamba mwanamk ndio huja mbele kabla ya familia yako hapo si ungan na ww nasema hivi mwanamke ana haki yake na familia ina haki yake kwako pia!!!weka hio kichwan itakusaidizaa!!
 
ukishaoa Mke wako ndio priority maana ndio mnayetengeneza nae maisha. Ndugu wana nafasi yao ila hawatakiwi kumzidi Mke. Kama hulijui hilo then bado hujakua kuelewa nafasi ya Mke ni ipi.

Mwanamke ndio angekua anaweka familia yake muhimu zaidi kuliko mume ungesema kwamba anafanya sawa??
 
Huyo mwanamke amechangia kiasi kikubwa kukuza huo mgogoro. Anaona tatizo anakaa kimya anaanza mchezo wa kukomoana.
 
ukishaoa Mke wako ndio priority maana ndio mnayetengeneza nae maisha. Ndugu wana nafasi yao ila hawatakiwi kumzidi Mke. Kama hulijui hilo then bado hujakua kuelewa nafasi ya Mke ni ipi.

Mwanamke ndio angekua anaweka familia yake muhimu zaidi kuliko mume ungesema kwamba anafanya sawa??
Hapo umetoka kinyume na mada sabb mkuu alivo ongea ni kwamba mke huja ju ya familia mana ak familia ni baba ,mama,dada, kaka...wew una anza anza aj kumpa nafas kubwa mkeo zaidi ya mama yako!???kuwa wew uelew nacho kiongea itapendeza zaid!!
 
Naona hujanielewa kwenye upande wa priority. Kwahiyo unanunua shamba unaanza kupiga simu kwa mama yako kumueleza huku mkeo uliyelala nae kitanda kimoja hujamwambia hiyo ni sahihi hiyo? Ukiambiwa Mke Ana nafasi ya muhimu zaidi ya Mama haimaanishi kwamba yuko juu ya Mama yako. Ukielewa hapo tunaweza kwenda Sawa, otherwise you may not be matured enough kutofautisha nafasi ya Mke Na nafasi ya ndugu/wazazi wako.
 
Wanaume wengine ndio mana wanagongewa wake zao... Sasa huyodada hayo anayopitia akipata wakumliwaza nje si ndoa itakuwa kama sehemu yakutunzia watoto tu....

NAOMBA NIKUSALIMIE TU KAKA
 
Back
Top Bottom