Nimueleweje huyu mwanamke?

Mkami Lum

JF-Expert Member
Feb 23, 2013
414
95
Mwajionaje hali ndugu zangu,

Kuna dada mmoja nilitokea kumpenda sana, na nampenda sana mpaka sasa.Mahusiano yetu yalianza kibahati mara baada ya kumsaidia mambo fulani.Nikiwa Tanga yeye akiwa Iringa, aliniambia yeye kapata kazi wilaya moja wapo ya mkoa wa Tanga na akaniambia anapokuja kuripoti ataomba nikampokee na awe mgeni wangu na hapo ndipo nitaanza kulifaidi tunda kwani toka tuanze sijamla nikafurahi kusikia hivyo.

Cha ajabu alipokuja Tanga akaesema kasindikizwa na dada yake hivyo kuonana ni ngumu, akaniomba msamaha kwa kutofanikisha mpango wetu, nami nikamsamehe.Baada ya yeye kuja kuanza kazi rasmi huko wilayani, mimi nikapata kazi Kahama na ikanibidi niondoje tena bila kuonana nae.

Nikiwa kahama amekua akiniomba niende kwake, nikamwambia nasubiria off ndio nitakwenda.Siku zikasogea nikapata off yangu ya wiki mbili, nikamwambia nakuja, akasema wewe njoo mme wangu nipo kwa ajili yako.

Nikiwa safarini (Singida) huku tukiwa tunawasiliana akaniambia ratiba ya kazini kwao imebadilika kwa hiyo wiki hii atakua busy anaona sitafaidi sana...
Ghafla nikaona safari yangu imekua chungu, nikaamua niteremkie hapa dodoma ili nisalimie ndugu.

Usiku wa leo sijalala kwa raha kila nikishtuka namuwaza yeye tu.Kwa hasira nikampigia simu nikamwambia sitaenda tena kwake ila akiwa likizo yeye ndio aje kwangu. Akasema likizo ni mbali, anahamu na mimi sana huku akiwa analia akanisihi niende wiki ijayo.

Kiukweli nimekua simuelewi, ananipenda au ananizuga?

Naombeni mnishauri
 
Wewe wa ajabu sana.
Kitu chenywe kimejificha unataka upewe kirahisi hivo??
Embu acha kulia lia kimbilia hapo City boys Mpesa kamtumie kama 200,000 kwa ajili ya shopping ya pweza ukifika ukute supu tayari

mmh kumbe kimejificha....
 
Wewe wa ajabu sana.
Kitu chenywe kimejificha unatklaupewe kirhisi hivo??
Embu acha kulia lia kimbilia hapo City boys Mpesa kamtumie kama 200,000 kwa ajili ya shopping ya pweza ukifika ukute supu tayari

Hii laki mbili ya Zimbabwe au ?
nyie masista duu mnajionaje kwani?
mnajiona mna thamani ya samsung s2 au sio ??
 
Hahahahahahahahahah d a aiseee hilo ni jaribu la aina yakipekee mmmm hata kama ni uga hiyo ni aina mpya ya zuga ____- Hapo naona hatari tupu tena unabahati hajakutia mikononi ________ Hilo ni jaribu aisee hapana toa nafas kubwa ivo mtu acheze na feeling's zako mmm
 
Angalia isiwe anasita kwa kukuonea huruma iwapo akuachia kale kaugonjwa kama bado huna. Kazi kwako.
 
kifupi ni kwamba huyo lady hayupo Tanga, na siku alipokwambia amefika tanga alikudanganya.. hiyo mizinguo haiishi mpaka siku atakayokuomba umtumie hela, kama huamini we nenda tanga halafu umwambie umefika uone atakavyoanza kutunga uongo mwingine ili tu msionane ... siku chache zijazo atakuomba pesa na huo ndio utakuwa mwisho wa mchezo
 
Back
Top Bottom