Nimsaidiaje mtu huyu?

Nimsaidiaje mtu huyu?

MamaBeata

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2013
Posts
325
Reaction score
112
Mimi ni mwanamke mwenye familia. Ndoa yetu ni changa bado. Hivi karibuni nilipata simu kutoka kwa mfanyakazi mwenzangu alieniomba nimsaidie kukaa na mdogo wake kwa siku tatu ili atafute chumba baada ya hapo angeondoka. Cha ajabu yule mtoto alikaa kwa wiki tatu akidai chumba hajapata ingawa haikua kweli vyumba vilikuepo ila yeye alitaka aendelee kukaa hapa kwangu. Nikamvumilia hadi alipoamua kuondoka na hajaenda kukaa mbali na hapa kwangu. Kilichonikera ni jinsi anavyokuja nyumbani kila mara hasa mida ya menu. Najua dada yake anampa hela ila yeye ananunulia viwalo kama mjuavyo wanachuo akitegemea kuangushia kwa mama Beata. Isitoshe mimi nina bajeti zangu nyumbani kwangu akishakuja yeye kila kitu kinaharibika. Mboga niliopanga iwe ya mchana na jioni itaishia mchana. Kingine akitaka kufua nguo, kuoga anakuja hapa kwangu kitu ambacho naona atanivunjia hata ndoa yangu maana huyu sio ndugu na hashindwi kufanya lolote na mume wangu. Hivi kweli kanikera. Naomba mnipe jibu zuri la kumwambia huyu mtoto asiizoee nyumba yangu mimi nilimkaribisha kwa heshima ya dada yake ila naona mazoea yamezidi wema wangu utaniponza. Mnisaidie wadau. Wasalaam, mama Beata
 
...mama kwakuwa ulimkaribisha kwa heshima ya dada yake haraka sana muwekee mipaka bila aibu kwa heshima ya dada yake vinginevyo ndo unaharibu. Watanzania tujifunze kusema yaliyoni kwa uwazi,sio unakufa na tai shingoni...
 
Ya Annastacia yepi? Mamndenyi. Kiukweli nahitaji ushauri mi mazoea siyapendi. Kwa nini hela yake atengenezee kucha akitegemea kuja kula kwangu? Hivi hajui maisha magumu au anajitoa ufahamu?
 
Last edited by a moderator:
...mama kwakuwa ulimkaribisha kwa heshima ya dada yake haraka sana muwekee mipaka bila aibu kwa heshima ya dada yake vinginevyo ndo unaharibu. Watanzania tujifunze kusema yaliyoni kwa uwazi,sio unakufa na tai shingoni...

asante Gefu kweli hata wahenga walisema wema usizidi uwezo. Kiukweli nimemchoka naona anamuaibisha dada yake kwa hizi tabia zake yani vituko vyake vinachefua. Akifika anataka apikiwe hata dada wa kazi hataki kumsaidia kuosha vyombo anadai ye kwao hafanyagi kazi!
 
Last edited by a moderator:
Na kushauri umwambie ukweli kuliko kuishia kulalama humu.

pengine ana hitaji neno lako japo moja ili aweze kupona na ninaamini wewe ni mtu mzima ushindwi kukaa nae chini nae na kumueleza maana wewe ni kama mdogo wako na ndio maana mwanzo ulipewa jukumu la kukaa nae.

ukweli pekee ndio uta kuweka huru.
 
Ndio tatizo letu watanzania kitu kinakukera unaishia kulalama baadala ya kufanya juhudi kumueleza muhusika unavyokerekwa na tabia zake!

kiukweli nilipata kigugumizi kwani sina asili ya uchoyo nikajua akipata chumba yataisha. Na huo mwezi alokaa kwangu hakuna bajeti ilokubali yaani mchele, sukari, unga vyote vilikata kabla mwezi haujaisha. NiKabaki naisubiri kwa hamu siku ya kuondoka kwake. Kwa sasa itabidi nivae uso wa mbuzi. Nahisi hata alivochukua nyumba ya hapa jirani ni ili aendelee kukaa karibu naa kwangu kashaniona mpole sana
 
Ongea na dada yake kama unaogopa kumwambia wewe mwenyewe. Ila dada samahani kama nitakukosea naomba tu kukuuliza swali dogo je wewe unakatabia ka uchoyo?
 
Ndio tatizo letu watanzania kitu kinakukera unaishia kulalama baadala ya kufanya juhudi kumueleza muhusika unavyokerekwa na tabia zake!

Mimi kiukweli nilipata kigugumizi kwani sina asili ya uchoyo nikajua akipata chumba yataisha. Na huo mwezi alokaa kwangu hakuna bajeti ilokubali yaani mchele, sukari, unga vyote vilikata kabla mwezi haujaisha. NiKabaki naisubiri kwa hamu siku ya kuondoka kwake. Kwa sasa itabidi nivae uso wa mbuzi. Nahisi hata alivochukua nyumba ya hapa jirani ni ili aendelee kukaa karibu naa kwangu kashaniona mpole sana
 
Last edited by a moderator:
Ndio tatizo letu watanzania kitu kinakukera unaishia kulalama baadala ya kufanya juhudi kumueleza muhusika unavyokerekwa na tabia zake!

mimi49 kiukweli nilipata kigugumizi kwani sina asili ya uchoyo nikajua akipata chumba yataisha. Na huo mwezi alokaa kwangu hakuna bajeti ilokubali yaani mchele, sukari, unga vyote vilikata kabla mwezi haujaisha. NiKabaki naisubiri kwa hamu siku ya kuondoka kwake. Kwa sasa itabidi nivae uso wa mbuzi. Nahisi hata alivochukua nyumba ya hapa jirani ni ili aendelee kukaa karibu naa kwangu kashaniona mpole sana
 
Last edited by a moderator:
mwambie ukweli haina maana kukaa kimya na anaonesha hana aibu wala mipaka atakuharibia huyo usipoangalia vizuri mkuu
 
kiukweli nilipata kigugumizi kwani sina asili ya uchoyo nikajua akipata chumba yataisha. Na huo mwezi alokaa kwangu hakuna bajeti ilokubali yaani mchele, sukari, unga vyote vilikata kabla mwezi haujaisha. NiKabaki naisubiri kwa hamu siku ya kuondoka kwake. Kwa sasa itabidi nivae uso wa mbuzi. Nahisi hata alivochukua nyumba ya hapa jirani ni ili aendelee kukaa karibu naa kwangu kashaniona mpole sana
Watu wengine wanajifanya hawajui ustaarabu..They take too much advantage of chances they get ..na wewe umepatikana kwasababu unaona utaonekana mbaya ukimwambia mkweli sometimes we have to be selfish and think about ourselves and our needs...Na suluhisho ni kumwambia ukweli tu kwamba sasa anajitegemea kwahio akija kwako mpaka kwa miadi na makubaliano...Hapo mwenzako anakucheka tu jinsi anavyokufanya kitega uchumi...:eyeroll1:
 
Ongea na dada yake kama unaogopa kumwambia wewe mwenyewe. Ila dada samahani kama nitakukosea naomba tu kukuuliza swali dogo je wewe unakatabia ka uchoyo?

Dado sina tabia ya uchoyo na mara zote nimekua nikijitahidi kuleta usawa yani hata nikinywa soda nanunua za nyumba nzima. Sema kutokana na maisha yanavyoenda mipango lazima iwepo hasa kwa sisi tunaoanza maisha. Inakua ngumu kwa wageni wasio rasmi na wanaopenda kutumia wenzao vibaya kujistarehesha wao.
 
Last edited by a moderator:
MamaBeata sio kwamba unaogopa zaidi atakuchukulia mumeo?

On a serious note, mwambie tu kiroho safey kwamba sasa ajitegemee kiujumla ikiwepo kujipikia
 
Last edited by a moderator:
Huyo si aliletwa na Dada yake usiumize kichwa
Mwambie Dada yake amuondoe!
 
Back
Top Bottom