Nimrod Mkono kupoteza ubunge? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimrod Mkono kupoteza ubunge?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pdidy, Sep 2, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Sep 2, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,442
  Likes Received: 5,695
  Trophy Points: 280
  Nimrod Mkono kupoteza ubunge
  [​IMG]


  Na Mwandishi wetu - Imechapwa 25 August 2010

  [​IMG]


  MBUNGE mteule wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono ameingia katika kashfa ya rushwa ya uchaguzi na huenda akapoteza ubunge, MwanaHALISI limeezwa.


  Mkono ametajwa kutoa mlungula kwa mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika jimbo hilo, Michael Makanja ili ampe nafasi ya kupita bila kupingwa.

  Taarifa zinasema Makanja amewaeleza viongozi wa Kurugenzi ya Ulinzi na Usalama ya CHADEMA, kwamba alishawishiwa na Mkono kupokea kiasi cha Euro 1,000 ( karibu Sh. 2 milioni) ili kujitoa katika kinyang’anyiro cha ubunge.

  Fedha hizo ni sehemu ya mamilioni ya shilingi ambayo Mkono inasemekana aliahidi kumlipa mgombea huyo wa Chadema.

  Mara baada ya kupokea kiasi hicho cha fedha, Makanja alitimiza kile alichoita, “makubaliano yake na Mkono.”

  Katika kufanikisha mkakati huo, Mkono inadaiwa kuwa alisaidiwa na kiongozi mmoja wa ngazi ya juu katika chama hicho (jina tunalo) ili kumshawishi Makanja kujitoa.

  Taarifa za Mkono kushawishi Makanja, tayari zimeripotiwa kwa vyombo vya dola ikiwamo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU).

  Alipoulizwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Edward Hoseah juu ya Mkono kutajwa “kumnunua mgombea” alithibitisha kuwapo kwa taarifa hizo.

  Hata hivyo, Hoseah aligoma kulizungumzia suala hilo kwa undani kwa kusema, “Kwa sasa niko Arusha. Sina facts (taarifa) za kutosha na hivyo siwezi kulizungumzia suala hilo.”

  Alipotakiwa kueleza nani anaweza kulisemea suala hilo kwa undani, Hoseah alisema, “Watu wa Dar es Salaam wanaweza kuwa na taarifa zaidi kuhusu hilo kuliko mimi ambaye kama nilivyokwambia niko mbali.”

  Hata hivyo, vyanzo vya taarifa vinasema, Makanja alikamatwa na maofisa wa TAKUKURU baada ya kujulishwa tukio hilo na viongozi wakuu wa Chadema.

  “Baada ya Makanja kufika hapa, wanachama walimvamia wakitaka kujua nini kimemsibu. Hapo ndipo mchezo ulipobumburuka,” alisema afisa mwandamizi wa ulinzi na usalama wa Chadema, Hemed Sabula.

  Alisema Makanja aliwasili katika ofisi za makao makuu ya chama hicho kwa lengo la kukutana na viongozi wakuu wa chama, lakini kabla hajaingia ndani alikutana na kundi la wanachama waliombana aeleze ukweli wa kilichotokea hata akajitoa.

  Makanja alijitoa kugombea ubunge katika jimbo hilo, siku mbili baada ya kuteuliwa kuwa mgombea kwa kumuandikia barua msimamizi wa uchaguzi wa jimbo.

  “Wanachama wale hawakuridhika na hatua ya kujitoa kwake. Wakataka kumpa kibano, lakini aliokolewa na vijana wangu,” alisema Sabula.

  Haikuweza kufahamika mara moja, ni kiasi gani cha fedha alichoahidiwa kulipwa na Mkono. Lakini taarifa zinasema, ameahidiwa “donge nono.”

  Akieleza hatua kwa hatua, Sabula alisema Makanja aliwekwa chini ya ulinzi kwa usalama wake na baadaye kuhojiwa na maofisa wa idara ya ulinzi na usalama ya chama, kabla ya kumkabidhi kwa maofisa wa TAKUKURU.

  Katika maelezo yake kwa maofisa hao wa chama, Makanja alikiri kupokea kiasi hicho cha fedha na kuongeza kwamba fedha zilizobaki alikuwa akabidhiwe na kigogo wa chama chake ambaye alikuwa nyuma ya mpango huo.

  Aidha, Makanja aliwataja viongozi wawili – katibu wa Chadema Mkoa wa Mara, Sibitari Nyanza na mwenyekiti wa vijana wa mkoa, David Katikiro – kwamba ni wabia katika mpango huo.
  Mahojiano kati ya maofisa wa Chadema na Makanja yamerekodiwa kwa njia ya video na kwa andishi lake binafsi; gazeti hili limefanikiwa kupata nakala yake.

  Katika andishi lake hilo, Makanja anasema alishawishiwa na viongozi wake hao wawili na kigogo mmoja kuachia jimbo kwa Mkono kwa kile alichodai, “walimtisha kuwa angefukuzwa kazi.”

  Makanja ni mwalimu kitaaluma, lakini kwa sasa anasoma katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
  Juhudi za gazeti hili kumpata Mkono ambaye ni mwanasheria, ili kuzungumzia suala hilo zimeshindikana. Simu zake za kiganjani Na. 0774-333333 na 0787-763355 zilikuwa hazipatikani kwa muda mrefu hadi tunakwenda mitamboni.

  Hata hivyo, mawasiliano kati ya Makanja na kigogo huyo wa Chadema yanaonyesha kulikuwa na aina fulani ya makubaliano kati ya Mkono na kigogo.

  Kwa mfano, ujumbe wa simu ya mkononi uliotumwa kwa kigogo huyo kutoka kwa simu ya Makanja (namba tunaihifadhi) unasema, “Mzee ameshanikatia tiketi ya kwenda Dar. Sasa mhimize amalize kiasi kilichobaki, maana hali yangu kiuchumi si nzuri….”

  Mwingine ulisema, “Tumeshamaliza kama tulivyokubaliana.” Ujumbe huo ulitumwa tarehe 21 saa 8:21 mchana. Ujumbe mwingine uliotumwa juzi Jumatatu, mara baada ya Makanja kuingia “mtegoni” ulisema, “Niko makao makuu ya chama. Nimewekwa chini ya ulinzi....”

  Akijibu katika namna ya kushtuka, kigogo huyo alijibu, “Wewe nani kakwambia uende huko… Watakuua. Siwezi kuja huko kukutetea....”

  Makanja alikuwa miongoni mwa wagombea saba wa upinzani waliojitosa jimboni Musoma Vijijini kushindana na Mkono, lakini katika hali iliyoshtua wengi, wote walijitoa na kumuacha Mkono kupita bila kupingwa.

  Mbali na Makanja, mwingine ambaye ameshtua uongozi wa Chadema kwa kuamua kutorudisha fomu, ni Dk. Ben Kapwani, ambaye alikuwa mwenyekiti wa Chadema wa Mkoa wa Iringa.

  Kamati Kuu (CC) ya Chadema ilimteua Dk. Kapwani kugombea ubunge katika jimbo la Ismani, mkoani Iringa. Hatua yake ya kutorudisha fomu kwa msimamizi wa uchaguzi, imesababisha William Lukuvi wa CCM kupita bila kupingwa.

  Dk. Kapwani alijiuzulu wadhifa wake siku moja baada ya kuvuja kwa taarifa kuwa sekretarieti ya Chadema ilipanga kumsimamisha uongozi.

  Kwa mujibu wa sheria mpya ya gharama za uchaguzi, matendo ya rushwa yanaweza kunyima nafasi ya kugombea mgombea aliyeteuliwa ikiwa mpinzani wake au chama cha siasa watawasilisha malalamiko kwa Msajili wa vyama vya siasa dhidi ya vitendo hivyo.

  Taarifa zilizofikia MwanaHALISI zinathibitisha kuwa tayari Chadema kinaandaa malalamiko rasmi kwa Msajili wa vyama vya siasa dhidi ya hatua hiyo ya Mkono.

  Sheria mpya ya gharama za uchaguzi inataka Msajili mara atakaporidhika kuhusu malalamiko kumfahamisha Tume ya taifa ya uchaguzi (NEC) ambayo itamfahamisha katibu mkuu wa chama husika kuwa mgombea wake amepoteza sifa
   
 2. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #2
  Sep 2, 2010
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,993
  Likes Received: 1,001
  Trophy Points: 280
  Hiyo sehemu ya nyekundu imenichekesha sana.
   
 3. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Nini kinachoendelea sasa?
  any news following this one?
   
 4. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #4
  Sep 2, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,305
  Trophy Points: 280
  Na kigogo wa Chadema aliyehusika ni mheshimiwa sana .........
   
 5. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #5
  Sep 2, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Fedha itaongea apo!
   
 6. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #6
  Sep 2, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,373
  Likes Received: 3,135
  Trophy Points: 280
  km sio zitto cjui nani.......
   
 7. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #7
  Sep 2, 2010
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Mkuu, huyu Jamaa kakalia kuti kavu. Maana wapinzani wake wana mpaka ushahidi wa SMS kutoka line yake. Na siku hizi number zimesajiliwa sijui atachomoa vipi.
   
 8. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #8
  Sep 2, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nawaza nje ya boksi!
   
 9. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #9
  Sep 2, 2010
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kama ushahidi upo apigwe chini na asiruhusiwe tena kugombe Ubunge.
   
 10. GY

  GY JF-Expert Member

  #10
  Sep 2, 2010
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Jamani huyo kigogo wa CHADEMA aliyehusika na hili ni nani, kuna mwenye fununu?
   
 11. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #11
  Sep 2, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Hiki kibabu kinadaiwa kuiibia nchi tokea "enzi za Mwalimu" bado tu hakijatosheka kama Mfalme Jeta vile...huu ndiyo mwisho wake I hope.
   
 12. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #12
  Sep 2, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  duh kipindi cha mavuno hiki, kuzungukana mumo kwa mumo. kaz kwel kwel.

  Ila wajue Mkono maji marefu yale, kabla ya kuyaingia lazima ujipime - sheria huwa zinapinda na msumeno unaweza kukata upande mmoja tu - pesa pesaaaa... pesa ndiyo sabuni ya roho....mwenye pesaaa.......

  hata kama za wizi ni pesa tu ati...
   
 13. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #13
  Sep 2, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Hawezi kupoteza ubunge kwa malalamiko ya wahuni wa Chadema... Cheki uhuni wao hapa
   
Loading...