Nimrod Mkono aitisha CCM

Mkono alitia mkono wake kwenye daftari la Zitto pale mjengoni. Asishangae atakapoona hata uenyekiti wa mtaaa hapati. Ndiyo uzuri wa magamba. Ukileta fyokofyoko unaadhibiwa immediately. Wanachotaka wao ni wanachama kuendelea kuwa royal kwa viongozi hata kama hawaridhiki na utendaji kazi wao.
 
Huyu si ni mmoja wa wafadhili wa magamba na ana kiburi cha fedha (jeuri yake anaijua Maregesi Abiud-Mwenyekiti mstaafu wa Jumuiya ya Wazazi CCM pale alipojaribu kupenyeza jina kugombea kupitishwa na CCM kugombea ubunge Musoma Vijijini). Huyu mzee CCM wanamgwaya, watamuomba radhi tu maana ni GAMBA gumu
 
Nimrodi siyo tu amekula fedha za Umma akisaidana na CCM, bali anajua madudu mengi ya CCM na viongozi wake. Mkwara huu ni kama ule wa Lowassa kule kikaoni Idodomya! Sasa wakimwaga ugali (kumwengua) atamwaga mboga (kuanika mabaya yao), kitu ambacho sidhani kama CCM wako tayari!
 
Nimrodi siyo tu amekula fedha za Umma akisaidana na CCM, bali anajua madudu mengi ya CCM na viongozi wake. Mkwara huu ni kama ule wa Lowassa kule kikaoni Idodomya! Sasa wakimwaga ugali (kumwengua) atamwaga mboga (kuanika mabaya yao), kitu ambacho sidhani kama CCM wako tayari!

Hi wakati wa ujio wa vyama vingi Mkono alikuwa wapi?
 
Kwako Mchambuzi, heshima mbele.

Nimeridhika sana na ukomavu na weledi wako katika kujibu hoja za mleta mada husika.

Mimi sio gamba na wala sijawahi kuwa gamba; mimi nilkuwa mmoja wa wale waliokuwa wanatia alama ya vema kwenye kivuli/giza (in general elections) enzi zile za chama kushika hatamu!

Ila uliyobainisha ni mapungufu ya muda mrefu sana NDANI ya CCM na kwa ujumla ya demokrasia nchini Tanzania toka awamu ya kwanza. Athari za ukosefu huo tuliziona mapema wakati wa mchakato wa kura za maoni za vyama vingi 1990-92. Sheria nyingi na mienendo ya serikali haikuashiria ukunjufu wa moyo ktk kukubali mfumo shindanishi wa vyama vya siasa. Ndio maana yale mambo muhimu sana ya Tume ya Nyalali yalipuuzwa. Kifupi ghiliba na hiana vilionekana na madhara yake ni kuwa na sheria mbovu za vyama vya siasa na ile ya uchaguzi.

Ila nitaomba kutofuatiana nawe kidogo kuhusu mirija ya mapato CCM kupata fedha. CCM kwa kuliona hilo na kwa hila nyingi walijimilikisha mashamba, miradi ya umma, majengo na hata viwanja vya michezo kwa lengo moja la kuhodhi mirija ya mapato. Baada ya siasa chafu za fedha na makundi kushika kasi (kama ulivyoeleza kwa ufasaha), siasa ndani ya CCM zikawa ni uwekezaji (investment politics) wenye lengo la faida na mrejesho (profit and return on investment basis).

Na kwa vile mchezo/mfumo wa fedha (haukuweza) kuthibitiwa na uongozi wa CCM (kwa sababu tofauti tofauti) ikabaki kuwa ni "demokrasia ya fedha". Muda huo watu walijua kuwa hakuna "fair ground" kuwawezesha kutimiza malengo yao ya kisiasa ndipo "mwanya na mfumo wa ufisadi tunaouona ukaasisiwa rasmi". Yote ni ktk kuongoze upana wa mirija ya mapato ya CCM, EPA, KAGODa ni mifano michache.


Iko sababu nyingine nitaitaja bila kuielezea, kuporomoka na kufa kwa mfumo wa kijamaa na hasa USSR. Hii ilkuwa na impact sio tu ktk vyama bali chumi na nchi zilizokuwa zimeegemea upande. Hilo lilibadili kwa sehemu itikadi na msimamo wa baadhi ya wajumbe......ndio maana walipoenda Z'bar kilifuata ni historia. Lakini wale wajumbe hawakubadilika walipokuwa Z'bar, bali walihitimisha tu kilichokuwa mioyoni mwao
 
Nimrod Mkono ni mmoja wa ma King Makers wa CCM. Kama 'Amepigwa chini' basi mjue hata hao ma King Makers wana mpasuko


Remember the thread kuna kundi jipya la urais....Na akina makongo mahama's kesi..Nchi hii kizungu zungu kweli! Watu wanapunguza vihunzi....Ukizoea kula nyama za watu hutaacha Nyerere said..Akubali tu zamu yake imefika
 
si ni huyu mzee alisign hoja ya zitto kwamba waziri mkuu ni dhaifu.... kashasahau? haya ndiyo matokeo yake - tena akiwaudhi zaidi watamfirisi.
 
Niliwaambia hali ilivyo CCM wana kitendawili cha kutengua( ama mgombea awe mzigo ama chama kiwe mzigo ama vyote kwa pamoja) na si vinginevyo.CCM ndio kifo cha jumla.Kam na huyu mzee naye yumo sijui watamshawishi vipi asubiri miaka mingine kuanzia 5 na kuendelea.Kila mtu umri wake umemtupa mkono na hawana hakika ya kuikuta CCM baada ya miaka 5.

Wapo wapi akina pasco na mchambuzi na Mkandara waje na big theory(doing things right,doing right thing).Siku zinavyoenda CCM inagain momentuma kuelekea to the hell wazee wanamchawasha (akina 6),chadema wana uhuru wa kuwapisha au wawapishe na kuwaongea rollon/spin ili wawahi kuzimu.
 
Niliwaambia hali ilivyo CCM wana kitendawili cha kutengua( ama mgombea awe mzigo ama chama kiwe mzigo ama vyote kwa pamoja) na si vinginevyo.CCM ndio kifo cha jumla.Kam na huyu mzee naye yumo sijui watamshawishi vipi asubiri miaka mingine kuanzia 5 na kuendelea.Kila mtu umri wake umemtupa mkono na hawana hakika ya kuikuta CCM baada ya miaka 5.

Wapo wapi akina pasco na mchambuzi na Mkandara waje na big theory(doing things right,doing right thing).Siku zinavyoenda CCM inagain momentuma kuelekea to the hell wazee wanamchawasha (akina 6),chadema wana uhuru wa kuwapisha au wawapishe na kuwaongea rollon/spin ili wawahi kuzimu.

There is no FUTURE for CCM, there is only PAST & PRESENT;
 
There is no FUTURE for CCM, there is only PAST & PRESENT;

Nawe umeona hilo,ila bado wanaevolve cha kusubiri ni how watabadilika na jinsi gani watakuja kuanza safisha damages kabla uchaguzi haujafika.Pia kuweza reebisha mioyo ya wataokosa.

By the way JK muda unayoyoma,unakuja ule muda wa panic kila kitu hakijakaa sawa ili kujiandaa kuondoka ikulu.hakuna tena nafasi ya kujenga nchi wala kumalizia ahadi zaidi ya kuja pga watu porojo kuwa fulani atamalizia.CDM watakuna na game itakayowafanay wananchi wajisikie guilty kwa kupigia CCM hata pale Dr. slaa alipowaonye kuwa watajutia sana uamuzi wao.
 
Mkuu Kimbunga,

Nashukuru kwa kunishirikisha katika mjadala huu. Maoni yangu yatakuwa katika sehemu kuu mbili. Kwanza ni kuhusu kushamiri kwa msuguano baina ya tycoons ndani ya CCM; na pili, ni mjadala kuhusu mapungufu ya CCM, hasa suala la Weak Internal Organization. Nitahitimisha kwa maoni juu ya nini kifanyike ili ku-rectify tatizo hili;
Nikianza na suala la tycoonization of CCM:

Tangia kuingia kwa mfumo wa vyama vingi, CCM haina tena vyanzo rahisi vya fedha kuendesha shughuli zake; hii ni tofauti na enzi za mfumo wa chama kimoja ambapo CCM ilikuwa inajichotea fedha serikali itakavyo; Kutokana na mabadiliko haya, CCM ilibidi itafute vyanzo vingine vya fedha ili kujiendesha. Mauaji ya Azimio la Arusha, hasa suala la maadili ya uongozi (leadership code), limechochea siasa zinazoendeshwa kwa nguvu ya fedha kuliko kitu kingine chochote, tena kwa uwazi/bila ya kificho. Lakini niseme tu hapa kwamba kwa maoni yangu, sioni kama tycoonization of CCM ‘Per Se’ ni tatizo kwani hili ni part and parcel of any Liberal Democracy; Tatizo linakuja pale tycoonization of politics inapokosa mipaka, au nyingine inapotumika ‘to violat’e haki ya kila mtanzania ya kuchagua na kuchaguliwa katika nafasi za uongozi;

Tangia mwaka 1992, CCM imekuwa hapatoshi kwani tukianza na suala la Marehemu Kolimba, kauli yake kwamba CCM imekosa dira ilizaa repercussions kubwa sana. Awamu ya pili ya CCM ‘Hapatoshi’ ikajitokeza mwaka 1995, kwani unlike miaka ya nyuma ambapo tycoons walikuwa zaidi wana fadhili chama au viongozi fulani fulani ili kujiweka vizuri na biashara zao, kuanzia mwaka 1995, wafanyabiashara wengi wakaanza na wenyewe kugombea nafas za uongozi ii na wao waingie jikoni. Miaka ya nyuma, ilikuwa ni jambo la kawaida kwa Mawaziri kwenye wizara zinazoshikilia sekta nyeti za uchumi wetu, kila mmoja kuwa na mfadhili wake (wengi wakiwa ni wahindi), lakini baadae tukaanza kushuhudia wafadhili hawa wakigombea nafasi za uongozi ili wajumuike na wanasiasa wao vipenzi huko ndani ya vikao vya juu vya maamuzi nchini kama vile Ubunge, uongozi wa Chama mikoani, na hata NEC.

Ni baada ya tycoons kuanza kuingia katika nafasi za uongozi ndio tukaanza kuona misuguano ikijitokeza baina ya makundi mbalimbali ya wanasiasa waliokuwa na wafadhili wao wenye nguvu ya fedha; mifano ni mingi lakini sio nia yangu kujadili majina; lakini kwa ujumla wake, tycoons weusi hawakuwa wanapea fursa sawa na tycoons wenye asili ya ki-asia. Muhimu zaidi hapa ni kwamba, tycoons WEUSI ‘became a big threat’ kwa viongozi fulani fulani ndani ya chama kwani, tofauti na tycoons wengi wenye asili ya KI-ASIA ambao huwa na tabia ya kuyumba na kubadili misimamo, kutegemeana nani yupo madarakani wakati huo, tycoons WEUSI walikuwa ni watu wenye msimamo na wasioyumbishwa kirahisi. Kwa mtazamo wangu, huu ndio ukawa mwanzo wa mambo ambayo tunayashuhudia leo hii.

Kwa mtazamo wangu, pengine finyu, Mkono presents an interesting case kwani kwa miaka yote, yeye hajawahi kuwa mtu wa ‘mtandao’. Hata uchaguzi wa 2005, sidhani kama alikuwa kundi la mtandao. Traditionally, Mkono ni mtu wa Mwalimu Foundation, na kama tunavyoelewa, 2005 mgombea wa taasisi hii alikuwa ni Salim. Pamoja na ukweli kwamba suala la Salim limepitwa na wakati katika siasa za leo, lakini bado kuna suala la kura za kanda ya ziwa kuwa muhimu katika kumpata mgombea Urais kupitia CCM 2015; Influence ya Mkono katika hili, hata akiwa nje ya NEC mimi nadhani ni kubwa sana, na yeye kuwa ndani ya NEC ni tatizo kubwa zaidi kwa makundi yanayojipanga na wagombea wao, hasa makundi yenye nguvu kubwa ndani ya Chama.

Udhaifu wa CCM kioganaizesheni
Hili ni suala la pili nililo ahidi kulijadili. Ningependa kulijadili in the context of internal democracy. Udhaifu wa kioganaizesheni CCM ni tatizo kubwa sana linalochangia chama kuyumba. Naelewa kwamba wapo wana CCM ambao watasimama haraka sana kupinga hoja yangu hii na kuishia kujenga hoja kwamba CCM ni chama stable, organized kwa vigezo ambavyo ni WEAK kama vile CCM ina wanachama milioni zaidi ya tano; CCM ina wabunge wengi zaidi; CCM hupata kura nyingi zaidi chaguzi za Rais, n.k. Hoja hizi ni dhaifu kwani Kipimo cha Strength ya Chama (kioganaizesheni) kwa mtazamo wangu atleast mambo makuu matatu ambayo ni: (1) Internal Democracy, (2) Uwazi (transparency) na uwajibikaji (3) (accountability), hasa katika maeneo haya:


  • Urasimu ndani ya chama (bureaucracy);
  • Uteuzi wa wagombea (selection of candidates);
  • Uteuzi wa viongozi (leadership selection);
  • Masuala ya fedha (political finance);
  • Sera za chama au development ya election programme;

Kwa madhumuni ya mjadala huu, nitazungumzia suala la Uteuzi wa wagombea. Katika teuzi zetu Tanzania, vyama vya siasa (pamoja na CCM) vimejenga tabia ya kuteua wagombea kwa misingi ya ukabila, ukanda, udini na patronage (kumpa mtu cheo kwa kutegemea atakurudishia fadhila in terms of political support katika utawala/uongozi wako); Masuala haya yote yana madhara makubwa sana katika internal democracy ya vyama kwani vyama vinageuka kuwa fiefdom au domain ya viongozi fulani fulani badala ya kuwa democratic institutions na instrunments to recruit democratic leaders;

Tujiulize – Iwapo mtu anajua kabisa kwamba alipita bila kupingwa jimboni kwa mfano kwa hila na ujanja ujanja, au alipata cheo au uongozi kupitia mchakato usio democratic, Je: Yeye atawezaje kuheshimu dhana ya Democracy? Uhaba wa demokrasia ndani ya vyama vyetu lina madhara makubwa kwa mfumo mzima wa kisiasa nchini na ni rahisi sana kwa hili ‘to replicate’ kwa mapana zaidi kimfumo, na hata nyingine kujenga utamaduni/tabia ya viongozi maamuzi ya kuburza buruza (undemocratic) katika masuala yanayogusa mambo nyeti ya taifa;

Baada ya kujadili suala hili la uhaba wa Demokrasia ndani ya vyama vyetu vya siasa, swali linalofuate ni JE:

CCM huwa inapata Viongozi wake kupitia Chaguzi?

Kwa maoni yangu, katika historia ya chama, ni nadra sana. Mara nyingi michakato wa kupata wagombea/viongozi ndani ya CCM haina transparency, imejaa rushwa, inatawaliwa na vitisho, na mara nyingine uingiliaj rasmi (bila aibu) wa kuvuruga au kugeuza matokeo ili tu kukidhi matakwa ya watu fulani , kinyume kabisa na dhana ya Demokrasia;

Tumeshuhudia viongozi mbalimbali wa kitaifa wakilalamikia hili. Kwa mfano, rejea barua ya Joseph Butiku kwa Mwenyekiti wa CCM (wakati ule Mkapa) iliyojaa malalamiko jinsi gani mchakato wa kumpata mgombea Urais 2005 kwa tiketi ya CCM, ulivyokuwa undemocratic; Vile vile hivi karibuni Professor Mark Mwandosya ametoa Kitabu kinachozungumzua jinsi gani kulikuwa na deliberate move ya watu fulani fulani kumwangusha kwenye kinyang’anyiro cha NEC Mbeya 2007 kwa njia Undemocratic; Suala la Mwandosya NEC 2007 na hili la Mkono linahusiana kwa namna nyingi sana;

Nadhani kufikia hatua hii, sasa tunaweza kusaidiana kuchambua na pengie kulipatia majibu swali lako muhimu lilouliza:


Yafuatayo ni maoni yangu binafsi juu ya hili:
Tofauti na Professor Mwandosya ambae ameamua kuliandikia rasmi kitabu tatizo hili, au Mzee Butiku kuliandikia barua rasmi kwa Mwenyekiti wa CCM (Mkapa), naamini wote kwa nia njema kabisa ya kujaribu kukirudisha chama katika mstari, Nimrod Mkono yeye ameenda mbali zaidi pengine baada ya kuhisi kwamba utaratibu kama wa Mwandosya au Butiku hauwezi kuleta suluhu juu ya jambo hili; Sasa ukizingatia Siasa zetu uchwara ambazo haziendeshwi kwa itikadi zinazoelekewa na badala yake ushindani uliojaa hoja juu ya WATU badala ya MASUALA, lakini pia siasa zenye kujali zaidi maslahi binafsi kuliko ya wananchi, victims wa wa undemocratic practices ndani ya chama ni rahisi kwa wao kuendesha siasa za liwalo liwe kama njia to express their dissent, disapproval, dissatisfaction, or all together;

Solution ya hili tatizo kwa mtazamo wangu, ni Party Electoral and Institutional Reforms, in the context of beefing up the Political Parties ACT, kwani hivyo ndivyo tutaweza kuipeleka nchi yetu towards demokrasia ya kweli; Sheria ya sasa ya gharama za uchaguzi sio comprehensive to address mapungufu ya vyama vyetu vya siasa kioganaizesheni;

Mchambuzi: Asante sana kwa maelezo mazuri yanayotia moyo kuwa bado kuna matuamini ya kubadilisha hii hali ya kisiasa iliyopo hapa nchini. Kama ulivyosema matatizo yote matano uliyoainisha yanasababisha nchi kuyumba. CCM kama chama kikubwa na chenye uzoefu kilitakiwa kiwe mfano wa kuigwa na hivi vyama vingine vya siasa lakini hali ni tofauti kabisa. The problem with this is the ill political residual effect that is within the nation. Siyo rahisi kuzalisha viongozi wa kisiasa wazuri hata katika vyama vya upinzani kwa kuwa wananchi wamelelewa katika huu mfumo mchafu. Hata kumlaumu Kikwete kuwa uongozi wake una matatizo ni kumwonea because the system is sick. What can he do as an individual in a ruined political environment??

Siku isiyo na jina na ije ili viongozi wanasiasa wakae pamoja wakubaliane kuwa ile sheria ya uchaguzi ibadilishwe ili ifanye kazi katika misingi ya haki na kweli vinginevyo ni shida tu
 
Mkuu Mchambuzi nashukuru kwa hoja mujarabu. Nilijua tu nitapata kitu toka kwako. Umenena vyema kuhusu matycoon wa CCM ambao inaonekana ndio wanakivuruga chama. Lakini nakumbuka kwamba matycoon walikuwepo tangia enzi za TANU wakichangia Chama lakini hawakuwa wakikemea na kuvuruga chama. Hivi watu kama akina Rupia enzi hizo si walikuwa matycoon ambao walifikia hata kumapatia mwalimu nauli ya kwenda UNO pamoja na kumpangia nyumba ya kuishi jijini lakini hawakuwa na makeke kama haya? Akina Al nuur Kasum vipi wao hawakuwa wachangiaji wa chama kweli?

Haya tukija miaka ya tisini ndipo hapo nakumbuka wale pace makers nao waliamua kuingia kwenye chungu kuona kuna nini humo. Kumbuka yule pace maker wa Ifakara akiitwa Abbas Gulamali na akina Biku mbona wao hawakuwa kama hawa wa sasa? Nadhani kuna shida nyingine kubwa zaidi ya huu utycoon. Hivi tunaweza kusema kwamba CCM ina mkemeaji ambaye anaweza kusimama na kukemea na watu wakamsikia siyo kwa ukali wa sauti yake bali kwa historia na usafi wake?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mchambuzi nashukuru kwa hoja mujarabu. Nilijua tu nitapata kitu toka kwako. Umenena vyema kuhusu matycoon wa CCM ambao inaonekana ndio wanakivuruga chama. Lakini nakumbuka kwamba matycoon walikuwepo tangia enzi za TANU wakichangia Chama lakini hawakuwa wakikemea na kuvuruga chama. Hivi watu kama akina Rupia enzi hizo si walikuwa matycoon ambao walifikia hata kumapatia mwalimu nauli ya kwenda UNO pamoja na kumpangia nyumba ya kuishi jijini lakini hawakuwa na makeke kama haya? Akina Al nuur Kasum vipi wao hawakuwa wachangiaji wa chama kweli?

Haya tukija miaka ya tisini ndipo hapo nakumbuka wale pace makers nao waliamua kuingia kwenye chungu kuona kuna nini humo. Kumbuka yule pace maker wa Ifakara akiitwa Abbas Gulamali na akina Biku mbona wao hawakuwa kama hawa wa sasa? Nadhani kuna shida nyingine kubwa zaidi ya huu utycoon. Hivi tunaweza kusema kwamba CCM ina mkemeaji ambaye anaweza kusimama na kukemea na watu wakamsikia siyo kwa ukali wa sauti yake bali kwa historia na usafi wake?

Gulamali alikuwa muuza na mtumia unga chini ya ulinzi wa CCM.Mkono ni mwanasheria wa deal zote halali na haramu chini ya serikali ya CCM.Yaani anayo Carrot and Stick .CCM wachague.

Ningependa issue za Nyerere kuchangiwa nauli sijui na suti zisiwe issue sana,kwani kila mahali tunaambiwa hayo.Hata Ndesa alichanga...ila iliingia TANU halafu chama kikapanga,na huu ulikuwa mchango wa matajiri na masikini kama itolewavyo sadaka.Hizo za kupeana pembeni huwezi jua km Nyerere alitumiaje.
 
Back
Top Bottom