Mkuu
Nguruvi3 uchambuzi mwingine mzuri sana. Umenikumbusha mambo mengi hasa kuhusu reforms ambazo tulikuwa tunategemea kuletwa na Secretariat mpya baada ya ile ya Makamba kuenguliwa na kuingia Mkama na akina Nape na Mwigulu. Ukweli inaonekana kana kwamba Katibu Mkuu Mkama amekata tamaa na ameamua kukaa kimya kama vile hayupo. Afdahali hata wakati wa Makamba kwa kuwa alikuwa akipiga vikelele.
Sasa mkuu inaonekana matycoon wamekimiliki Chama, utawaondoaje ili kuleta mageuzi? Naona kama ndio sasa wanataka kujiimarisha kwenye vyombo vya maamuzi ndani ya Chama.
Kiranga na hapo ulipouliza ndipo tatizo lilipo haswaa!
Labda nikumbushe kuwa hizi mbio za NEC, jumuiya za chama n.k. ni sehemu ya kujipanga.
Haitoshi tu kuwa mjumbe wa NEC ili mtu awe salama. Ni lazima awe na kundi litakalosimama naye. Hapo ndipo unaona fedha inapofanya kazi kwa sasa huko UVCCM, Wazazi, UWT n.k
Kosa kubwa walifanya CCM miaka mitano iliyopita. Ilipobainika kuwa chama kimetekwa nyara na tycoons, 'vijana' watiifu wa mwalimu waliiomba kikao cha NEC kifanyike Butiama ili kuondoa 'mzimu' unaokitafuna chama.
Katika kikao kile kulikuwa na kila ushahidi wa kuwatuhumu na kuwahukumu wanaokichafua.
Nakumbuka wazee walliamu vinara wa genge hilo wafukuzwe uanachama. Ile ndio ilikuwa nafasi pekee iliyojitokeza ya kusafisha chama ili mageuzi yafanyike. Mwenyekiti alikataa si kwasababu ya masilahi ya chama ni kwasababu wote waliopaswa 'kuchinjiliwa baharini' ndio waliompa huo uenyekiti.
Ni baada ya kosa kosa hiyo tycoon wakapata mwanya wa kuwarudi wanaoleta 'vurugu' dhidi yao.
Kwa bahati mbaya wale waliotaka kusafisha chama hawana nguvu ndipo tukashuhudia wabunge wakitoswa kiaina.
Hilo tu likavunja nguvu ya wapigania mgeuzi na wale waliojaribu wameshapewa onyo.
Unakumbuka pia NEC iliyopita ilitaka mageuzi ndani ya sekretariati mpya. Maana ya hii ni kuwa umiliki wa tycoon haukuwa kamilifu na wanataka kuhodhi kila kitu kwa asilimia mia moja. Na ili kuhakikisha kuwa hakuna mabaki ya Nyerere ndani ya chama chao, vijana wa Mwalimu wameundiwa kitu kinaitwa baraza la ushauri. Baraza hili halina nguvu ya kisheria ndani ya chama. Kwa utaratibu huo safisha safisha imekamilika, sasa hivi tycoons wanajpanga katika maeneo muhimu 'strategic position' ili kukidhibiti chama kikamilifu kuanzia bungeni, ndani ya chama na serikali.
Kwasasa hivi hakuna njia ya kukisafisha chama ndio maana nasema kitakachoisafisha CCM ni 'natural death'
Historia inafundisha kuwa vyama vilivyoondoka madarakani kwa mtazamo wa kiCCM kama KANU, UNIP vimetokomea katika ulimwengu wa siasa.
Pamoja na hayo kuna nafasi moja tu ndogo iliyobaki. Wazee wa chama kusimama kidete.
Hili ni gumu lakini likifanyika mapema na kumshinikiza mwenyekiti ambaye ni kikwazo kingine cha mageuzi, wanaweza kurudi 'mwaisela' . Kwasasa wapo ICU wanapumulia mashine.