Nimrod Mkono aitisha CCM

Nimrod Mkono aitisha CCM

kweli ccm kushney kwani mbona kukicha vigogo wana gombea madalaka? why? kunakiongozikweli hapo?
 
Mkono ana sabaBu ya kusema kwa kutoa vitisho kwani ana mkono mrefu(kama jina lake) ndani ya magamba. Pia lazima utambue kuwa MKONO kabeba siri nzito ndani ya magamba, so lazima awe nakiburi na jeuri kubwa y kutoa vitisho bila kujari ndani ya magamba kuna itfaki ya uongozi. Anajiamini kuwa kashiriki kula mengi na magamba makubwa kwa miongo mingi.Kwa mimi ni furaha kwani HASIRA YA MKIZII..................Mpaka 2015 mtakufa kwa presha....mafisadi hayooooooooooooooooo!!!!!!!!
 
Mkono anatoa tu tahadhari kwamba kama ni mchezo mchafu usielekezwe kwake maana yeye ni mdau tena wa siku nyingi, ni dalili za wazi kwamba kila mwenye hisa nyingi CCM anakaa chonjo kwa lolote maana mfumo unayumba sana kwa sasa.
 
wamuondoe halafu wajue the real king makers katika CCM nina uhakika kama akihamia CHADEMA Mara nzima inahamia CHADEMA! Hawa CCM wana wazimu!

Mara yote ilishahamia CHADEMA na si kwa sababu ya li-Mukono hilo.Li mutu renyewe linaupendeleoo na waikizu na wazanaki tuu afu useme nini.wewe liache tu.Si lilisema litakuwa ribunge la musoma vijijini hadi kufa.
Ritashangaa this time jina lake halipiti kugombe ubunge kwa li chama la zamani.
 
Nimesikia kupitia magazeti kwamba Nimrod Mkono (Mbunge wa Musoma Vijijini - CCM), akisema kwamba ameshtushwa na taarifa kupitia vyombo vya habari kwamba jina lake limeenguliwa toka katika watu wanaogombea Uenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi. Amesema kama kweli jina lake limeenguliwa basi CCM patakuwa hapatoshi.

Hivi CCM niliyokuwa naijua imefikia kiasi cha kutishwa kiasi hicho na wanachama wake? Kweli CCM imekuwa kama kambale: Baba sharubu, mama sharubu na watoto sharubu.

Mkuu Mchambuzi CCM imefikia hatua ya kutishwa na kila mtu. Watishaji wana moral authority kweli ya kuitisha CCM au ndio kusema CCM imekosa watu wenye moral authority ya kukemea?

CCM dhaifu hivi.Ndio wanayosema wataalamu wa kuchambua mambo humu ndani kuwa chama kinapendwa.Chama kischopendwa na wanachama lets alone kujipenda kititwaje kinapendwa?
 
Short and clear wakimtema basi na hela zake wamezikosa. Hili kwa magamba haliwezekani ni lazima watatafuta namna ya kumkumbatia
 
Jamani mi naomba kujuzwa umuhimu wa CWT ni nini hasa ktk maendeleo ya nchi/chama/mtu binafsi mpaka kufikia Mh Kutamuka hayo?

Pili, wazazi ni akina nani?

Sifa na faida za kuwa mwanachama ni zipi?
 
Mkono ameelewa kuwa CCM haina uwezo wa kumfanya chochote kwa kuwa inaelekea kufa ndo maana anaitisha!
Nimesikia kupitia magazeti kwamba Nimrod Mkono (Mbunge wa Musoma Vijijini - CCM), akisema kwamba ameshtushwa na taarifa kupitia vyombo vya habari kwamba jina lake limeenguliwa toka katika watu wanaogombea Uenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi. Amesema kama kweli jina lake limeenguliwa basi CCM patakuwa hapatoshi.

Hivi CCM niliyokuwa naijua imefikia kiasi cha kutishwa kiasi hicho na wanachama wake? Kweli CCM imekuwa kama kambale: Baba sharubu, mama sharubu na watoto sharubu.

Mkuu Mchambuzi CCM imefikia hatua ya kutishwa na kila mtu. Watishaji wana moral authority kweli ya kuitisha CCM au ndio kusema CCM imekosa watu wenye moral authority ya kukemea?
 
Lazima ajiamini bse kama ela anazo za kutosha na ata wakimtosa ana pa kwenda!
 
Jeuri ya PESA, Jamaa akisema jambo, harudi nyuma. Japo na JK haziivi lakini hamwogopi kabjsaaa.
 
Kama ni Nimrod Mkono wa Mkono Advocates,basi sioni ajabu akiwachimba kwara,kwanza kaongea kiustaraab sana tu..

Nimrod Mkono anauwezo wa kuwatisha ccm na ccm haina uwezo wa kumfanya chochote.Nakushangaa mleta mada kama vile wewe unavyoshangaa!

Nimrod Mkono ana makbrasha karibia yote ya ufisadi wa ccm,sasa mtamwambia nini?hapa mimi nadhani ccm ndo wamefanya makosa.

Mwandikie JK barua uone kama hataufyata.
 
Jamani mi naomba kujuzwa umuhimu wa CWT ni nini hasa ktk maendeleo ya nchi/chama/mtu binafsi mpaka kufikia Mh Kutamuka hayo?

Pili, wazazi ni akina nani?

Sifa na faida za kuwa mwanachama ni zipi?
Iddi Simba alikuwa mwenyekiti wa ccm wazazi na ndo alipata ama kutumia nafasi hiyo wakati ule wa scandal ya EPA.Ni nafasi yenye influence,lakini yote ni mambo ya pesa na nafasi za kufisadi,that's it.
 
Mkuu Kimbunga,

Nashukuru kwa kunishirikisha katika mjadala huu. Maoni yangu yatakuwa katika sehemu kuu mbili. Kwanza ni kuhusu kushamiri kwa msuguano baina ya tycoons ndani ya CCM; na pili, ni mjadala kuhusu mapungufu ya CCM, hasa suala la Weak Internal Organization. Nitahitimisha kwa maoni juu ya nini kifanyike ili ku-rectify tatizo hili;
Nikianza na suala la tycoonization of CCM:

Tangia kuingia kwa mfumo wa vyama vingi, CCM haina tena vyanzo rahisi vya fedha kuendesha shughuli zake; hii ni tofauti na enzi za mfumo wa chama kimoja ambapo CCM ilikuwa inajichotea fedha serikali itakavyo; Kutokana na mabadiliko haya, CCM ilibidi itafute vyanzo vingine vya fedha ili kujiendesha. Mauaji ya Azimio la Arusha, hasa suala la maadili ya uongozi (leadership code), limechochea siasa zinazoendeshwa kwa nguvu ya fedha kuliko kitu kingine chochote, tena kwa uwazi/bila ya kificho. Lakini niseme tu hapa kwamba kwa maoni yangu, sioni kama tycoonization of CCM ‘Per Se' ni tatizo kwani hili ni part and parcel of any Liberal Democracy; Tatizo linakuja pale tycoonization of politics inapokosa mipaka, au nyingine inapotumika ‘to violat'e haki ya kila mtanzania ya kuchagua na kuchaguliwa katika nafasi za uongozi;

Tangia mwaka 1992, CCM imekuwa hapatoshi kwani tukianza na suala la Marehemu Kolimba, kauli yake kwamba CCM imekosa dira ilizaa repercussions kubwa sana. Awamu ya pili ya CCM ‘Hapatoshi' ikajitokeza mwaka 1995, kwani unlike miaka ya nyuma ambapo tycoons walikuwa zaidi wana fadhili chama au viongozi fulani fulani ili kujiweka vizuri na biashara zao, kuanzia mwaka 1995, wafanyabiashara wengi wakaanza na wenyewe kugombea nafas za uongozi ii na wao waingie jikoni. Miaka ya nyuma, ilikuwa ni jambo la kawaida kwa Mawaziri kwenye wizara zinazoshikilia sekta nyeti za uchumi wetu, kila mmoja kuwa na mfadhili wake (wengi wakiwa ni wahindi), lakini baadae tukaanza kushuhudia wafadhili hawa wakigombea nafasi za uongozi ili wajumuike na wanasiasa wao vipenzi huko ndani ya vikao vya juu vya maamuzi nchini kama vile Ubunge, uongozi wa Chama mikoani, na hata NEC.

Ni baada ya tycoons kuanza kuingia katika nafasi za uongozi ndio tukaanza kuona misuguano ikijitokeza baina ya makundi mbalimbali ya wanasiasa waliokuwa na wafadhili wao wenye nguvu ya fedha; mifano ni mingi lakini sio nia yangu kujadili majina; lakini kwa ujumla wake, tycoons weusi hawakuwa wanapea fursa sawa na tycoons wenye asili ya ki-asia. Muhimu zaidi hapa ni kwamba, tycoons WEUSI ‘became a big threat' kwa viongozi fulani fulani ndani ya chama kwani, tofauti na tycoons wengi wenye asili ya KI-ASIA ambao huwa na tabia ya kuyumba na kubadili misimamo, kutegemeana nani yupo madarakani wakati huo, tycoons WEUSI walikuwa ni watu wenye msimamo na wasioyumbishwa kirahisi. Kwa mtazamo wangu, huu ndio ukawa mwanzo wa mambo ambayo tunayashuhudia leo hii.

Kwa mtazamo wangu, pengine finyu, Mkono presents an interesting case kwani kwa miaka yote, yeye hajawahi kuwa mtu wa ‘mtandao'. Hata uchaguzi wa 2005, sidhani kama alikuwa kundi la mtandao. Traditionally, Mkono ni mtu wa Mwalimu Foundation, na kama tunavyoelewa, 2005 mgombea wa taasisi hii alikuwa ni Salim. Pamoja na ukweli kwamba suala la Salim limepitwa na wakati katika siasa za leo, lakini bado kuna suala la kura za kanda ya ziwa kuwa muhimu katika kumpata mgombea Urais kupitia CCM 2015; Influence ya Mkono katika hili, hata akiwa nje ya NEC mimi nadhani ni kubwa sana, na yeye kuwa ndani ya NEC ni tatizo kubwa zaidi kwa makundi yanayojipanga na wagombea wao, hasa makundi yenye nguvu kubwa ndani ya Chama.

Udhaifu wa CCM kioganaizesheni
Hili ni suala la pili nililo ahidi kulijadili. Ningependa kulijadili in the context of internal democracy. Udhaifu wa kioganaizesheni CCM ni tatizo kubwa sana linalochangia chama kuyumba. Naelewa kwamba wapo wana CCM ambao watasimama haraka sana kupinga hoja yangu hii na kuishia kujenga hoja kwamba CCM ni chama stable, organized kwa vigezo ambavyo ni WEAK kama vile CCM ina wanachama milioni zaidi ya tano; CCM ina wabunge wengi zaidi; CCM hupata kura nyingi zaidi chaguzi za Rais, n.k. Hoja hizi ni dhaifu kwani Kipimo cha Strength ya Chama (kioganaizesheni) kwa mtazamo wangu atleast mambo makuu matatu ambayo ni: (1) Internal Democracy, (2) Uwazi (transparency) na uwajibikaji (3) (accountability), hasa katika maeneo haya:


  • Urasimu ndani ya chama (bureaucracy);
  • Uteuzi wa wagombea (selection of candidates);
  • Uteuzi wa viongozi (leadership selection);
  • Masuala ya fedha (political finance);
  • Sera za chama au development ya election programme;

Kwa madhumuni ya mjadala huu, nitazungumzia suala la Uteuzi wa wagombea. Katika teuzi zetu Tanzania, vyama vya siasa (pamoja na CCM) vimejenga tabia ya kuteua wagombea kwa misingi ya ukabila, ukanda, udini na patronage (kumpa mtu cheo kwa kutegemea atakurudishia fadhila in terms of political support katika utawala/uongozi wako); Masuala haya yote yana madhara makubwa sana katika internal democracy ya vyama kwani vyama vinageuka kuwa fiefdom au domain ya viongozi fulani fulani badala ya kuwa democratic institutions na instrunments to recruit democratic leaders;

Tujiulize – Iwapo mtu anajua kabisa kwamba alipita bila kupingwa jimboni kwa mfano kwa hila na ujanja ujanja, au alipata cheo au uongozi kupitia mchakato usio democratic, Je: Yeye atawezaje kuheshimu dhana ya Democracy? Uhaba wa demokrasia ndani ya vyama vyetu lina madhara makubwa kwa mfumo mzima wa kisiasa nchini na ni rahisi sana kwa hili ‘to replicate' kwa mapana zaidi kimfumo, na hata nyingine kujenga utamaduni/tabia ya viongozi maamuzi ya kuburza buruza (undemocratic) katika masuala yanayogusa mambo nyeti ya taifa;

Baada ya kujadili suala hili la uhaba wa Demokrasia ndani ya vyama vyetu vya siasa, swali linalofuate ni JE:

CCM huwa inapata Viongozi wake kupitia Chaguzi?

Kwa maoni yangu, katika historia ya chama, ni nadra sana. Mara nyingi michakato wa kupata wagombea/viongozi ndani ya CCM haina transparency, imejaa rushwa, inatawaliwa na vitisho, na mara nyingine uingiliaj rasmi (bila aibu) wa kuvuruga au kugeuza matokeo ili tu kukidhi matakwa ya watu fulani , kinyume kabisa na dhana ya Demokrasia;

Tumeshuhudia viongozi mbalimbali wa kitaifa wakilalamikia hili. Kwa mfano, rejea barua ya Joseph Butiku kwa Mwenyekiti wa CCM (wakati ule Mkapa) iliyojaa malalamiko jinsi gani mchakato wa kumpata mgombea Urais 2005 kwa tiketi ya CCM, ulivyokuwa undemocratic; Vile vile hivi karibuni Professor Mark Mwandosya ametoa Kitabu kinachozungumzua jinsi gani kulikuwa na deliberate move ya watu fulani fulani kumwangusha kwenye kinyang'anyiro cha NEC Mbeya 2007 kwa njia Undemocratic; Suala la Mwandosya NEC 2007 na hili la Mkono linahusiana kwa namna nyingi sana;

Nadhani kufikia hatua hii, sasa tunaweza kusaidiana kuchambua na pengie kulipatia majibu swali lako muhimu lilouliza:
Mchambuzi, CCM imefikia hatua ya kutishwa na kila mtu. Watishaji wana moral authority kweli ya kuitisha CCM au ndio kusema CCM imekosa watu wenye moral authority ya kukemea?

Yafuatayo ni maoni yangu binafsi juu ya hili:
Tofauti na Professor Mwandosya ambae ameamua kuliandikia rasmi kitabu tatizo hili, au Mzee Butiku kuliandikia barua rasmi kwa Mwenyekiti wa CCM (Mkapa), naamini wote kwa nia njema kabisa ya kujaribu kukirudisha chama katika mstari, Nimrod Mkono yeye ameenda mbali zaidi pengine baada ya kuhisi kwamba utaratibu kama wa Mwandosya au Butiku hauwezi kuleta suluhu juu ya jambo hili; Sasa ukizingatia Siasa zetu uchwara ambazo haziendeshwi kwa itikadi zinazoelekewa na badala yake ushindani uliojaa hoja juu ya WATU badala ya MASUALA, lakini pia siasa zenye kujali zaidi maslahi binafsi kuliko ya wananchi, victims wa wa undemocratic practices ndani ya chama ni rahisi kwa wao kuendesha siasa za liwalo liwe kama njia to express their dissent, disapproval, dissatisfaction, or all together;

Solution ya hili tatizo kwa mtazamo wangu, ni Party Electoral and Institutional Reforms, in the context of beefing up the Political Parties ACT, kwani hivyo ndivyo tutaweza kuipeleka nchi yetu towards demokrasia ya kweli; Sheria ya sasa ya gharama za uchaguzi sio comprehensive to address mapungufu ya vyama vyetu vya siasa kioganaizesheni;
 
Back
Top Bottom